Tahadhari: Tatizo la Lissu ana "MUKU" ya MIUNGU Ukimdhulumu lazima ufe.

Tahadhari: Tatizo la Lissu ana "MUKU" ya MIUNGU Ukimdhulumu lazima ufe.

Inashangaza sana watu humu ndani wanavyosifia mtu kuingia mkataba wa kulindwa na majini.

Maana MUKU ni kulindwa na majini, watu wanazidi kumuweka mbali Mungu, na hawana haja Naye.

Na narudia hakuna MUKU yoyote maana ingekuwa ni MUKU hakuna Risasi ingemuingia.

Hizo ni Kinga za kawaida basi.
MUKU ninayoifahamu mimi ni ile ambayo haiombwi na wala haitafutwi bali yenyewe huja kwa yule aliyetunukiwa !
Wakati mwingine hata yeye mwenyewe huwa hajui !
Ila yawezekana MUKU ikawa ina maana tofauti tofauti kwa imani tofauti tofauti !
 
We muongo na vitisho vyako, Muuaji au hitman ahitaji cv ya mtu ili amuue, anahitaji picha yako na unaishi wapi, basi.

Hitman cv yako inamsaidia nini?
Huyo Lisu, hana cha muku wala alama yoyote.

Atashindwa, na atabaki chadema au ataondoka na wahuni wake, chama kitajengwa upya.

Ndio maana nikasema Professional Killer
Kila mtu anaweza kuwa muuaji lakini sio kila mtu anaweza kuwa Professional Killer
 
Mwaka hauwi mbaya kwa maneno ya binadamu mitandaoni
Mwaka utaisha salama salmini na utaufuta huu uzi wako wa ajabu ajabu hapa

Mungu hamilikiwi na kikundi cha watu,Mungu ni wa viumbe wote

Au kwa akili yako ilivo ndogo unaona Mungu anakusikia wewe sana kuliko Binadamu wengine?

Kusikia kwa kenge Mpaka .....
Tusiandikie Mate wakati Wino upo.
Fanyeni Uhuni alafu tutarejea kwenye huu uzi kabla ya 31december
 
Haya.
Tukutane Kwanza 21
Alafu mlete ujinga wenu.
Imeandikwa wapi lazima lisu ndio ashinde nyie?yani akishinda mwingine eti Rushwa😀mnachekesha

Ccm inashinda miaka yote mbona hizo laana zenu hazifanyi kazi

Wapumbavu tu kama nyie ndio mnaoamini ujinga
 
Mbona unaumia sana,kila muda unaandika andika mambo ya chadema,yanakuumiza kichwa kuliko wajumbe wenyewe,yanakuhusu?achana na Mambo ya watu
Chama cha Mbowe kikifa,wewe inakuhusu nini?pambania familia yako.
Nazuiwa na Katiba?
Au kuna Sheria yoyote inanizuia kufanya haya?
 
Imeandikwa wapi lazima lisu ndio ashinde nyie?yani akishinda mwingine eti Rushwa😀mnachekesha

Ccm inashinda miaka yote mbona hizo laana zenu hazifanyi kazi

Wapumbavu tu kama nyie ndio mnaoamini ujinga

Mbona kama umeogopa?
Mshinde Lisu kwa kutumia hizo mbinu za CCM ziwe haramu alafu Mpaka December 31 tutarudi kwenye huu uzi.

Vichwa ngumu kama wewe hamwezi kuelewa mambo madogo kama haya.
 
Mbona kama umeogopa?
Mshinde Lisu kwa kutumia hizo mbinu za CCM ziwe haramu alafu Mpaka December 31 tutarudi kwenye huu uzi.

Vichwa ngumu kama wewe hamwezi kuelewa mambo madogo kama haya.
Utarudi labda kwa familia yako ndio afe mtu ila sio kuombea wengine wafe,utakufa wewe
 
Wana bodi!

Mimi kama Kuhani Katika Hekalu Jeusi ambaye ninaufahamu wa mambo mbalimbali ya Kiroho. Nimeona niwajulishe hili.

Kwenye huu Ulimwengu kuna watu walichorwa Alama na miungu ambayo alama hiyo kwao ni ulinzi. Ukiwagusa unapasuka wewe.

Kwenye Biblia mtu pekee aliyeripotiwa kuwekewa Alama na Mungu ni Kaini ambaye aliwekewa Alama kwenye paji la Uso wake. Ili watu wanaotaka kumuua wakiiona wasimuue. Na yeyote atakayethubutu kumuua basi Mungu atampasua na kumuangamiza.

Alama za namna hiyo huitwa MUKU.
Kwenye Ngumi mtu aliyechanjiwa MUKU akikutwanga Ngumi Moja kwenye ule Mkono wake wenye chale(Alama za miungu) unaweza kuzima au kukata Moto.

Au kuna wale Mwalimu ukimchapa mwanafunzi mwenye MUKU Mwalimu unavimba Mikono au unaumwa Mkono.
Haya mambo wengi hawayajui kwa sababu sio Elimu maarufu

Lissu anaweza kuingia kwenye kundi hilo la watu Wachache wenye MUKU.

Ukimdhulumu uwe umejipanga haswahaswa maana Hapana Shaka miungu iliyompa hiyo MUKU utacheza nayo vilivyo.

Kwa professional Killer, lazima anapotumwa Kuua mtu lazima awe na CV ya mtu anayeenda Kumuua. Na kama atagundua mtu huyo anaalama za miungu, MUKU ambayo inamlinda Basi professional Killer huweza kumshauri aliyemtuma Njia nyingine mbadala mbali na kumuua huyo mtu.

Pia kuna watu ambao Miili yao wameilaani na kuisomea Dua kuwa yeyote atakayeudhuru mwili wake kwa kuuua Basi Laana na majanga atakayoyataja yampate huyo Muuaji.

Miili hiyo inajina lake na ibada zake hufanywa na mtu mwenyewe mbele za mizimu, makuhani wa Nguvu za Giza, waganga au Majini.

Sisi bado ni watazamaji
Mbona Bashite hajafa?
 
Back
Top Bottom