Taifa la washangilia Misiba na Visasi

Waliopata nafasi na support ya 100% kutengeneza Taifa la Tanzania ni wawili tu. JKN na JPM, ila kiuhalisia hawa ndio walileta "unintended consequences" nyingi na kulivuruga Taifa kuliko hao wanne waliobaki.

Ukitengeneza Taifa la chuki lazma utengeneze Taifa la visasi. Chuki huzaa visasi na visasi huzaa chuki.

JPM alitengeneza Taifa la chuki na visasi kupita kawaida. Kwa vyovyote vile, ukiwa na chuki au kisasi na mtu, utamuombea mabaya. Hivyo kusema, akifikwa na mabaya, utafurahia. Viongozi wakuu wana nafasi kubwa sana katika kutengeneza Taifa. Nape alitolewa pistol mchana kweupe mbele ya macho ya camera. Kiongozi mkuu wa nchi badala ya kukemea jambo lile, alikemea media zilizoandika jambo lile. Clouds ilivamiwa mbele ya macho ya CCTV camera, kiongozi mkuu badala ya kuacha vyombo alivyoviunda vifanye kazi yake, alivizuia "kiishara".

Kwa mfano, kuna tetesi kuwa sera mpya ya elimu ni kufundisha kwa lugha ya kiswahili kuanzia primary hadi tertiary education. Utekelezaji wa sera hii utakuja kuleta visasi na chuki miongo kadhaa ijayo huko mbele. Kwanini? Kwasababu, kuanzia walioandaa sera, watakaoisimamia na watakaoitungia sera hakuna hata mmoja anayeamini hivyo. Wote wanapeleka watoto wao kwenye english medium schools. Mambo ni mengi ila jambo la msingi hapa, mliosoma na kupata dhamana ya kulitumikia Taifa hili fanyeni haki na uadilifu.
 
to be honest Mimi ni mmojawao. na ni maombi yangu wale wote waliomsumbua na kufurahia kifo Cha magufuli wakakufe wote hata saa hii.
Dunia hii kila anapokufa mtu kuna watu watafurahi na kuna watakaohuzunika. Kama aliyefariki alikuwa mtu mbaya wengi watafurahi. Na kama alikuwa mtu mzuri wengi watasikitika. Magufuli aliua watu kwa makusudi ndiyo maana wengi walifurahia kifo chake.
 
Pumbavu vzao acha mbwai iwe mbwai wafe wao tufe sisi tuendelee kuzikana kwa awamu walianzisha, Pumbavu Mungu habagui dadadadeki kitu hicho, imoooo imoooo goooooal
Hahahah
 
Ni vile tu sio pigo zangu kufurahia kifo cha mtu... ila kauli za kejeli wanazotoaga kwa kifo cha jembe JPM (lililotupelekaga uchumi wa kati) waga zinanipa hasira kinooooomaaa!!!
 
Walishangilia kifo cha Magufuli wakafikiri wao hawatakufa ,na bado siku ya Mboe itakuwa balaa kwa kushangilia.
Mbowe anahusika vipi na matatizo yenu ya huko CCM. nyie malizaneni wenyewe huko msituingize kwenye bifu zenu.

Embicile
 
Hili suala lilitengenezwa awamu ya 5, kwa ufupi.. Kilifanyika kikao cha siri cha viongozi wa juu wa chama..

Lengo la kikao hiko kilikuwa ni kupunguza nguvu ya vyama pinzani..

Mwenyekiti wa wakati huo CCM hakutaka ushindani hasa kutoka upinzani... Na alifanikiwa kuwanyamazisha kwa nguvu za kidola na kijasusi.... Na kuwalazimisha wengine kuunga juhudi zake...

CCM walifurahi sana... sasa baadae Mwenyekiti akahakikisha pia anashughulikia baadhi ya CCM wenzake.. Wengine walikuwa na makosa.. Wengine walionewa..

Baada ya upinzani kupunguzwa nguvu kidola... Wakabaki CCM wenyewe...

Hapa ndipo shida ipo.... CCM wanataka kujilipua wenyewe... Na chanzo ni kwamba hakuna wakuwapa changamoto.... Labda sheria za uchaguzi zibadilike..
Maridhiano yanahitajika CCM wenyewe kwa wenyewe...

Siasa za kuumizana.. za awamu ya 5 hazifai tena
 
Kwani nani hatakufa? Wote tutakufa ila katika mipango tofauti kadri Mungu alivyo tupangia ukiogopa kifo basi hukuzaliwa
 
Walaumiwe wao " walioanzisha" walidhani hawatokufa huku wakihanikiza kejeli kwa wafu wengine.

Kiko wapi? Mmoja wao chaliii!
Wakati unashangilia kupigwa risasi Kwa Lissu na kuweka updates Kila baada ya nusu saa kwamba amekufa uliona fahari?
 
Dunia hii kila anapokufa mtu kuna watu watafurahi na kuna watakaohuzunika. Kama aliyefariki alikuwa mtu mbaya wengi watafurahi. Na kama alikuwa mtu mzuri wengi watasikitika. Magufuli aliua watu kwa makusudi ndiyo maana wengi walifurahia kifo chake.
nitajie watano waliouawa na Magufui wapi na lini, ambao ulishuhudia Kwa macho Yako na ukiwa na aKili timamu kabla hujanywa pombe, hujavuta bangi na au hujalala na mwanamke huku ukiwa umekula umeshiba.
 
Aliyelipasua Taifa Hili ni Yule aliyelala yoo kule Chato... Mungu amrehemu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…