Taifa letu ni Salama na lenye utulivu kisiasa Kwa sababu ya hawa Majenerali Pichani. Wanasiasa na viongozi Mnajifunza Nini hapa?

CCM ndio chama kilichobeba matumaini ya mamilioni ya watanzania na kilicho na uchungu na maisha ya watanzania
 
Mwananchi ndiye alikwenda akapigana vita vya uganda na Tanzania?wananchi ndiye anakesha usiku kucha akilinda mipaka yetu? Mwananchi ndiye anakesha akipambana na Magaidi yenye silaha za kivita?
 
Mwananchi ndiye alikwenda akapigana vita vya uganda na Tanzania?
Aisee unadhani nani alipigana vita vya Uganda ? Mercenaries kutoka nje ya nchi ? Kwa taarifa yako vita vikitokea mgambo na hata watu wenye umri zaidi ya miaka 18 mnaanza kukusanywa na kwenye kupigwa msasa wa muda mchache tena ikibidi nyie ndio mnatangulia kama chambo..., Tatizo watu Vita mnavisikia au kuviangalia kwenye sinema au mnadhani ni kama kucheza playstation
wananchi ndiye anakesha usiku kucha akilinda mipaka yetu?
Unadhani bila mwananchi kuwa macho ya nchi akija mtu asiyeeleweka mtaani ni nani atapata taarifa ? Au unadhani inteligensia huwa inatoka kwenye computer fulani au karai la mpiga ramli ? Unadhani leo mwananchi akiamua kwamba waliopo hapo hawafai kuna wa kumfukuza ? Unadhani bila mwananchi kuwa calm and collected baada ya JPM kufa, kusingetokea power struggle ?
Mwananchi ndiye anakesha akipambana na Magaidi yenye silaha za kivita?
Hivi hata unajua maana ya gaidi ? Magaidi wanatokea mitaani wala hawahitaji silaha za kivita akivaa tu bomu tena la kutengenezea nyumbani kwa kutumia mbolea ya ammonia anaweza kuingia sehemu na kuua watu lukuki..., ni macho ya mwananchi au wananchi kuishi kwa upendo ndio maana hakuna ugaidi wala chuki baina ya watu na watu hivyo badala ya watu kupigana makofi wanagonga cheers na kuchekeana kwa upendo... (Solidarity)

Ila narudia tena hawa walamba asali wanataka kuondoa Utaifa wetu wanaharibu kazi kubwa sana iliyotengenezwa na waasisi kwa kuleta Ujangiri kwenye mali ya common mwananchi...
 
Uchawa
Uchawa pia ni kazi sema intweza utu
 
CCM ndio chama kilichobeba matumaini ya mamilioni ya watanzania na kilicho na uchungu na maisha ya watanzania
Kina uchungu wa kuteka na kuuawa kwa sababu wananchi haohao ndio wanaotekwa na kuuawa na kulazimishwa kuongozwa na viongozi ambao hawakuwachagua.
 
Somo la Botswana wamelielewa, subirini mwakani πŸ€”πŸ€”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…