Tabia ya kuwaamini watu na kuwa na huruma ya kupitiliza badala yake wanaharibia mambo yangu mengi. Kwa kweli hii tabia sijui taicha lini. Kuna kipindi nilipokea mtu anashida kweli kweli kwao hawana kitu baba hayupo mama anamtegemea yeye ikabidi niwe nafanya nae kazi shambani kwangu huku nampa viposho vya kusaidia familia yake yaani mama yake.
Mara ya kwanza alikuwa mtiifu sana na alikuwa anakuja shamba kwa wakati. Alipoanza kuzoea akaanza kuchelewa akaanza kuja kazini amelewa nikamwambia aache tu kazi akasema sawa nikampa hela kidogo alizokuwa ananidai tukaachana mbele ya mwenyekiti wa mtaa. Hazikupita siku tatu akatuma sms akaomba msamaha akasema bro nisamehe zile zilikuwa ni pombe mimi nkamwambia siwezi kufanya kazi na mlevi akasema ataacha pombe nikamwambia sawa njoo. Akaanza kupiga kazi nampa hela yake anasepa haikupita wiki moja akarudia pombe akawa hafanyi kazi nikamtimua. Akaondoka baada ya siku mbili akanitumia sms ananidai nikamwambia kijna unanidai shilingi ngapi, akasema elf 20 ikabidi nimpigie simu nimuulize kama kweli ananidai isije ikawa mtu katumia simu yake, akapokea simu akiwa amelewa nikamwambia subiri pombe iishe kesho ndio unipigie, kesho yake hakunitafuta.
Akakaa siku kama tatu hivi akanitumia sms akasema bro nakudai elf 10 mimi nikanwambia kijana naona unanisumbua akasema sawa, baada ya dakika chache nikapigiwa simu kituo cha polisi nikafika, kufika namkuta dogo amekaa amelewa chakari, polisi wakauliza unamjua huyu nikasema yes, wakasama anakudai shilingi ngapi nikasema hanidai na tuliachane naye kwa amani mbele ya viongozi wa mtaa tena wakishuhudia, police wakasema mpe laki moja na nusu yake anayekudai loooooh! Nilistaajabu sana nilimtazima yule dogo na jinsi alivyokuwa amelewa aliwezaje kuwashawishi wale polisi kuwa ananidai laki na nusu nao wakaamini. Nilichokifanya niliwaambia polisi ngoja nimpigie kiongozi wa mtaa aje aamue hili swala maana yeye anajua A to Z wakasema hawataki huo ushahidi pale sio mahakamani. Wakasema kama hutotoa hiyo hela tutakuweka ndani kisha kesho muende mahakamani. Nikasema kwa heshima niliyojijengea hapa mtaani siwezi kwenda mahakamani kupiginia kesi ya laki na nusu, kwa heshima pia ya kazi yangu siwezi kwenda mahakamani sio kwamba siwezi kulala ndani ila talalaje ndani kwa kesi ya namna hii.
Nikasema kwa kuwa kuna mazingira ambayo sijayaelewa elewa na kwa kuwa mimi bado natafuta hela na hii ni ajali katika utafutaji, hiyo hela nitaitoa yaliyobaki namwachia Mungu aamue. Niliitoa ile hela yote nikaagana nao nakuwatakia kila lakheri nikaondoka. Nikipata muda tawaletea case ya pili ambaye nimeshatabiri inaweza kutokea the same kama hii bado nafuatilia situation kwa karibu.