Nimezaliwa na kukulia Mjini, ila wakati wa likizo ya mwezi wa 6 na 12 ningewasumbua Wazazi kuwa nataka kwenda kumsalimia Babu Kijijini, kilochokua kinanifanya nipende kwenda kwa Babu sio kingine ni Kuchunga Ng'ombe, Mbuzi na Kondoo!
Nikienda Kijijini kwa sababu ya umri wangu mdogo, nilikua napewa Mbuzi, Kondoo na Ndama wadogo kwenda Kuchunga!
Hii siku ambayo sitaisahau, siku hiyo kulikua na Dalili za mvua muda mrefu, nikiwa Polini nikichunga, ghafla nikaona Wanyama wote Wameacha kula Majani wamesimama, kama kuna kitu wanasikiliza, baadaye nikaona Wanyama wote wanakimbia kumfata Dume la Kondoo, Lile Dume liko kwa mbele, Wanyama wote wapo nyuma yake!
Dume la Kondoo limekaa Mkao wa kupigana!
Kwa Utoto wangu nikawa na nashangaa nikijiuliza maswali mengi, kilichowafanya hawa Wanyama wakae nyuma ya Kondoo Dume ni nini?
Kumbe Babu yangu Baada ya kuona hari ile ya Dalili za Mvua (Sijui kama nae alihisi Radi itapiga)
Akaanza kunifata Machungani....!
Nikawa nimemuona akiwa umbali kama mita 100 hivi, na kundi lile la Wanyama lipo umbali kama wa Mita 20 toka nilipo, nikiwa Bado nashangaa, namwona Babu anajaribu kukimbia kuja nilipo huku akiniambia kwa Sauti kubwa "Kimbia kakae nyuma ya Kondoo"
Mimi nikaona huyu Babu anazingua, sasa nikakaae nyuma ya Kondoo ili iweje...!
Babu akarudia kauli yake safari hii ikiwa na msisitizo na Kitusi juu!
Basi ikabidi nitoke mbio nikaenda kusimama nyuma ya lile Kundi ambalo Kondoo alikua mbele yetu, Babu akasema "Chuchumaaaaa"
Nikachuchumaa, nikaona Babu kasimama umbali kama mita 50 hivi akitazama!
Baada ya Muda nikaona Kondoo kaweka Kichwa Vizuri, akasogea mbele kidogo, ilipiga Radi sijawahi kuona!!!
Japo ilipiga kwanza Mwanga, tukawa kama tumemulikwa na Tochi, then ndo Sauti ikaachia!