Duuh mtu unakopa bilioni kwa ajili ya shughuli,
kuna kipindi tulifanya biashara ma mama mmoja wa kariakoo, anauza nyumba yake, tumepambana sana kwenye terms, akaanza kupambana na madalali hataki kuwalipa chao, mpaka wanaelewana ni saa kumi na nusu jioni, hapo tumesign makubaliano ya kuuziana inabidi tuwaekee chao, option zilizopo ni transfer kupitia TISS, (Mfumo wa kuhamisha hela kwa mabank ya ndani siyo ile taasisi ule wa kuhamishia kwenda nje unaitwa TT), kwa huo muda wangeipata siku inayofuata ambayo isingewezekana pia kwa sababu ni sikukuu na siku zinazofuatia ni weekend, Cheque same same, Cash withdrawal kwa amount wanayostahili hamna namna tukawaambia hapa hadi sikukuu iishe, tuchane mikataba, kama mna wasi wasi.
Yule mama aliangua kilio anapiga magoti anaomba apewe chochote ameshaahidi msikitini atalisha watu biariani na wameshaomba kibali cha kufunga mtaa, anahitaji milioni 15 nyingine 5 anazo, busara ikatumika akapatiwa 10 pale pale kutoka kwenye jopo hapo hadi mwanasheria wake na wetu alitoa...Binafsi nikajiuliza mtu unauza nyumba milioni 260, unatumia zaidi ya 20M kwenye sherehe na kuwapa ma sheikh ni akili au matope, hujalipa madalali 10% yao, bado ndugu hawajakuandama lazima uwatoe kidogo...daah
Baada ya biashara kukamilika mtoto wa mama akavuta subaru, kazama dubai kuagiza spear za magari, yule mama ni tajiri wa mali alizoachiwa na mumewe ila hana akili ya kucontrol mali, hapo kariakoo anapokaa ni kwenye apartment wamenunua ni zile za kulipia service charge, nikajuuliza yani wanauza nyumba nzuri mbezi ambapo wangeweza kuweka garden nzuri matunda na mboga mboga, wanakaa kariakoo sema vioo vinawasaidia kelele, hamna parking hamna ustaarabu, ukisema hata ufungue kioo ni matusi tupu....mimi nasema wacha wapigwe kwa kweli, hadi akili iwakae sawa