TAKUKURU Mwanza tafadhali kamateni na zikagueni upesi sana Simu za Mchezaji Adeyoum wa Geita Gold FC na Mratibu wa Yanga SC Bhinda

TAKUKURU Mwanza tafadhali kamateni na zikagueni upesi sana Simu za Mchezaji Adeyoum wa Geita Gold FC na Mratibu wa Yanga SC Bhinda

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Hii Michezo tumeshaicheza mno mpaka pale tulipoamua Kustaafu na Kutubu Dhambi kwa Mwenyezi Mungu hivyo Timu zingine zikifanya Michezo hii akina GENTAMYCINE huwa tunaishtukia na Kuigundua haraka sana hivyo tukisema Watu fulani Wachunguzwe upesi huwa tunakuwa tumeshatonywa na Vyanzo vyetu aminika ndani ya Kambi zao na Mipango Ovu ya ile Janja Janja Company yenye Ofisi zake Jengo refu kiasi Posta..

Tafadhali sana Uongozi wa TAKUKURU Mkoani Mwanza upesi sana Kamateni Simu za Mchezaji wa Geita Gold FC Adeyoum Saleh ( ambaye ni mwana Yanga SC lia lia Moyoni na Rohoni ) kisha na ya Mratibu Mwandamizi wa Yanga SC Mohammed Bhinda na baada ya hapo ( Kuzikagua Kiumakini ili mjiridhishe )) mtajua muanzie wapi juu ya Shutuma za Upangaji Matokeo ( Match Fixing ) katika Soka Tanzania kwani tumeshachoka baada ya Kuuvumilia Upuuzi kama siyo Uhuni huu.

Watendaji wa TAKUKURU Kazi Kwenu.
 
Siku hizi Janja Janja Company yenye Ofisi zake Jengo refu kiasi Posta limeacha Kuhonga Timu nzima kwakuwa wameshaishiwa Pesa na pia wanaogopa Kushtukiwa na badala yake Wanahonga Wachezaji Wachache wenye Mahaba ya Wakosa Kombe kwa Miaka Minne FC.

Nimetonywa kuwa Kesho kati ya Mmoja wao Yondani na Nyosso ( au hata Wote tu ) watacheza Faulo ( Rafu ) za Makusudi ili watolewe kwa Kadi Nyekundu, Timu idhoofu na Washindwe hata Kucheza nao tena katika Michuano ya ASFC ambayo ni Konzi Nje ( Unafungwa na Kutolewa ) kabisa.

Beki David Kameta Kesho Wakazie tu.
Kwahiyo na simba na yenyewe ilinunua ile mechi ya biashara?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Mwaka huu mmekuwa kama wanawake wajane kila siku kulalamika halafu hatuoni hata hatua mnazochukua. Hii inadhihirisha kuwa msimu huu mmejikita zaidi kwenye propaganda. Hayo madai yangekuwa yanaukweli basi tungeona mkifungua kesi kwenye mahakama ya michezo
 
Yanga inacheza kama Simba miaka 4 ya nyuma au kama Man city, atasare au kufungwa na timu kubwa zote ila vidagaa anameza vyote bila kutafuna. Simba ya mwaka huu ni Simba ya mihemko na mipasho na ndio hii unayoiona mwaka huu.
Hii Simba haina mfungaji na historia ya Ligi letu mara zote timu inayotoa mfungaji bora ndio timu inayobeba kombe. Pengo la Kagere na Boko ameziba Mayele na jumla ya magoli yote ya Simba NBC league yanamenyana na magoli ya Mayele. Kiufupi Mayele ni zaidi ya fowad wote wapuuzi wapuuzi pale Simba. Mayele>Mugalu+Boko+Kibu Nyamizi
 
Back
Top Bottom