TAKUKURU Mwanza tafadhali kamateni na zikagueni upesi sana Simu za Mchezaji Adeyoum wa Geita Gold FC na Mratibu wa Yanga SC Bhinda

Yaani watu wakishindwa kwasababu ya uwezo wao mdogo ndio useme wamehongwa?

Hao mabeki unaowasifia, timu yao iko nafasi ya ngapi? Yanga iko nafasi ya ngapi?

Aisee weee bwana, unakerwa sana na mafanio ya Yanga. Hiyo ni roho ya Mfalme Zumaridi na Makerubi wake ndio inakusumbua
 
Tatizo simba wanadhani wao walishaandikiwa LIFETIME CHAMPIONSHIP, ni upumbavu kudhani wewe tuu ndio una haki ya kushinda siku zote.
 
Unajulikana kuwa wewe ni pumbavu na jinga kabiasa humu JF
 
Nikimheshimu mtu huwa nashindwa kabisa kumvunjia heshima hata akiharibu na wakati mwingine nawaachia wengine washughulike naye. Lakini kwa tabia hii ambayo kila mechi ya watani zako lazima uje utuhumu kuhongwà au kuhujumu bila ushahidi si jambo zuri. Juzi Simba kashinda na hata baadhi ya magoli mtu asiye mwanasoka angeweza kuyatilia shaka kama lile la Back pass ya Mangalu, lakini wenye damu ya soka wanajua Soka ni mchezo wa makosa ni lazima yatokee. Lakini nyie kila siku hasa wewe na Mightier na kapuuzi kengine kameibuka kanaiga uandishi wako sijui kanaitwa kaKENGE nako ovyo tu. Kwenye kikosi cha Biashara alikuwemo mchezaji mwandamizi wa Simba miaka michache iliyopita Redondo, kwa hiyo tuseme miamala ilipitia kwake? Hatuwezi kuwa Great thinkers kwa kuzushazusha mambo huku tukijiona Pure talented. Ni talent gani hii ya kuzusha mambo ambayo kesho viongozi wa timu wasio na subira wanaweza kukuamini na kupelekea kutoa adhabu kwa mchezaji na hivyo kumwaribia maisha yake. Umesahau mashabiki wa Pamba walivyokwenda kuharibu nyumba ya Juma Mhina na hata kaburi la mama yake kwa sababu ya tuhuma kama hizi Pamba ilipofungwa na Malindi na kukosa ubingwa wa Muungano? Juzi Miongoni mwa Magolikipa bora kabisa kuwa kutoa Tanzania Mohamed Mwameja(Tanzania One halisi) alieleza jinsi alivyonusurika kuuawa na mashabiki wa Simba kisa tu shabiki mmoja kasema Mwameja, Masatu na Masha wameonekana ofisini kwa Azim Dewji wakichukua fedha ili wauze mechi na Stella Artois kuepusha Dewji kuwanunulia Canter wachezaji wote wa Simba kama wangechukua kombe uwanja wa Taifa mbele ya Rais Alli Hassani Mwinyi mwaka 1993?
Uchezaji ni ajira ya vijana hawa mnaowazulia usaliti kila siku, lakini kwa vile nyie hakuna mnachogharimia mnaona sawa tu kuropoka lakini wenzenu wanaumia. Nani anaweza kuvumilia kumlipa mchezaji anayeuza mechi? Hata tuhuma zile za Mwanza zilisababisha Juma Mhina kukosa kabisa nafasi timu ya Taifa wakati alisitahili. Mwaka juzi Metacha Mnata akaingizwa kwenye Kashfa ya usaliti mechi ya Yanga dhidi ya Coast Union na mpaka Leo timu kubwa ikitaka kumsajiri kama ilivyokuwa kwa Simba dirisha dogo maneno yanazuka kuhusu uuzaji mechi timu zinaghairi.
Kama hatuna ushahidi tukae kimya. Allegations zisizoweza kuthibitika zinaharibia watu image wakati ile ni ajira kwao. Kama una tuhuma wapigie TAKUKURU moja kwa moja ili kama hazina ukweli zisimchafue mchezaji kuliko hii tabia ya ovyo ambayo Mods nao wanaiacha tu iote mizizi.
 
Labda Geita Gold ndo wamenunua wachezaji Yanga..
Saidoo na wenzake lakn kwa Yanga hii hakuna haja ya kununua mechi na haijawahitokea.
Kama Simba huwa anapita njia hizo usidhani na Yanga anapita huko.
 
Kama kumbukumbu zangu zipo sawa nakumbuka humu kuna uzi humu jf ulikiri kabisa wazi wazi kuwa Gentamycine ni miongoni mwa watu unaowakubali sana. Sijui ilikuwaje umemkubali mtu mwenye ujinga mwingi humu JF.
 
Mmejaa uoga uoga tu timu Kama uwezo wake mdogo itafungwa tu hakuna Cha rushwa Wala nini Kwahiyo hata Ile mechi ya ngao ya hisani Simba ilipofungwa Kuna wachezaji wa Simba walipewa hongo kuweni wakweli tu Yanga mwaka huu Wana kikosi Bora yatasemwa mengi lakini huo ndio ukweli
 
Mtoa uzi ni mpuuzi sana chezeni soka achen porojo mambo ya hovyo unaandika kuchafua watu vijana wa ufipa mna akili za hovyo sana
 
Mpira si vita. Mpira ajira. Mchezaji akivunjika shingo unapata faida gani wewe Kolo popoma Mfawidhi mwandamizi?
 
Wangeanzia uchunguzi kwenye mechi yenu na berkane mseme vizuri zile beki zenu zilivuta mlungula kiasi gani mpaka mkatiwa mbili kavu, wakimaliza uko wageukie mechi ya biashara itajulikana mliwapa bei gani kwa yale magoli ya mchongo, maana aiwezekani umpigie mayowe anayecheza soka la kitabuni na aliyesajili vizuri wakati huo huo unamuacha anayecheza soka la kubahatisha na kuvizia, yanga akishinda leo ni matokeo ya usajili bora walioufanya na si vinginevyo unavyotaka kuwaaminisha watu
 
Utopolo wazee wa bahasha washafanya yao,usijisumbue kwenda kibanda umiza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…