Mkuu
Liability pole kwa yote uliyopitia. Naomba usinipige mawe kwa nitayoandika hapa. Jambo lililokumba linaweza kabisa likawa ni kosa la kibinadamu tu na sio RUSHWA kama unavyodhani. Ukiangalia katika issue yako hakuna shaka yeyote katika hatua zote za awali (Usaili, kutangaza matokeo na uteuzi) unayoweza kuuelekeza TUME ya ajira. Ukiangalia kwa umakini utaona kwamba kilichotokea hapo ni kukosekana kwa mawasiliano mazuri kati ya maafisa wachache wa Tume ya Ajira na sio nia Ovu kama unavyodhani.
kilichotokea hapo ni kwamba Afisa mmoja anaita Interview ya nafasi fulani na Afisa mwingine anaangalia katika Database ya TUME na kumteua mwajiriwa wa nafasi ambayo watu wameitwa kwa interview. Unaweza usiniamini nilichoandika hapa lakini kama ukienda katika baadhi ya Taasisi za Serikali ukiwa kama raia wa kawaida jambo kama lako sio la ajabu.
Katika kujisomea kwangu kama mwananchi wa kawaida na ninapotembea banda la Utumishi katika maonyesho mbalimbali kuna kitu wanakiita maadili ya Watumishi/Utumishi wa Umma ambayo yamenifanya nipende kubakia tu Sekta binafsi na sio kukimbilia huko kwao. Kwa ulivyoandika hapo juu nachelea kusema kwamba huna maadili ya kuwa Mtumishi wa Umma. Nakushauri tu uungane na sisi katika Sekta binafsi.
Samahani kama nimetumia Lugha kali sana LAKINI hayo ndiyo mawazo yangu.
Ahsante