Kiukweli kabisa mimi na hao sekretarieti ya ajira sina hamu nayo kabisa,mwenye wa 5 walituita kwenye usaili ambao tuliitwa elfu 3 lakini tuliohudhuria tulikuwa kama elfu 2,tumeingia kwenye usaili Dodoma udom kiukweli kabisa ni kichekesho na maajabu niliyoyaona kwa macho yangu,
mtihani wa writing ulivuja tena sana nilikaa na jamaa pembeni yangu yaani alikuwa anajua kila kitu aliingia na karatasi ya majibu,kiukweli niliishiwa nguvu ya kuendelea na mtihani.
Mamlaka za juu wanatakiwa waichunguze hii tume ya ajira kiukweli kabisa haina maana kuita watu kila pembe ya nchi ilihali wanajua saili wanazofanya hazina maana,heri waite watu wao tu na wawape kazi kuliko mausumbufu kama haya