Pre GE2025 Tamaa ya Tundu Antipas Lissu, Kuutaka uwenyekiti wa CHADEMA taifa ni utashi wake binafsi au shinikizo kutoka nje ya nchi kwa wanao mbackup!

Pre GE2025 Tamaa ya Tundu Antipas Lissu, Kuutaka uwenyekiti wa CHADEMA taifa ni utashi wake binafsi au shinikizo kutoka nje ya nchi kwa wanao mbackup!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Gentleman,
ni muhimu sana ukawa mtulivu na kwakweli mstahimilivu katika kupata elimu na kuongeza uelewa na ufahamu wa kibobevu kutoka kwenye hoja mahususi ninazowasilisha humu jukwaani kwa hiyari,

Muhimu ni kuacha uvivu katika kusoma na kupata content mahususi.

kwa kuhitimisha,
ni muhimu sana wadau wa JF kujua na kuelewa hii taama na uchu wa Lisu kuutaka uenyekiti wa Chadema Taifa hauna shinikizo la kimataifa hasa kutoka kwa mabwenyenye ya magharibi yanayombackup?

Lakini pia,
hii ni fursa muhimu sana kwa wadau kujifunza kati ya hawa mafahali wawili, nani anatumia sayansi ya siasa na nani anakurupuka katika kufikia azma zao za siasa?

mambo haya ni muhimu sana gentleman kuliko mihemko 🐒

Huna hoja mkuu! Sioni content yenye maana zaidi ya ule uapodomia aliousema Mtikila (RIP).

Ulipata lecture ya siasa toka Mlimani city jana lakini? Mama alikuwa anasikiliza somo kwa umakini toka kwa Simba
 
Hao mambwanyenye ndo wamemsanua kua chairman ni pazia pale,Akili ipo CCM mwili upon CDM, intelligence ya hao mabwanyenye bado ni ya kutilia shaka???
Chairman tangu 2015 wanachama na raia wengi wameendelea kutathmini huyu mtu ni WA aina gani,yupo sawa kweli?
Gentleman,
nadhani kitendo cha kutangaza kugombea umakamu mwenyekiti taifa, halafu ghafla tena kutangaza kuutaka uenyekiti wa Chadema Taifa ndicho hasa cha kutiliwa shaka kitaalamu.

Nini kimetokea hata hata kumchochea huyu muungwana kutamani vyeo vyote viwili?

amesense nini hasa?🐒
 
Huna hoja mkuu! Sioni content yenye maana zaidi ya ule uapodomia aliousema Mtikila (RIP)
Relax gentleman,
na upunguze mihemko utaona giza katika kila hoja mahususi.

kua mtulivu tafadhali 🐒
 
Gentleman,
nadhani kitendo cha kutangaza kugombea umakamu mwenyekiti taifa, halafu ghafla tena kutangaza kuutaka uenyekiti wa Chadema Taifa ndicho hasa cha kutiliwa shaka kitaalamu.

Nini kimetokea hata hata kumchochea huyu muungwana kutamani vyeo vyote viwili?

amesense nini hasa?🐒

Kutiliwa shaka na ccm? Hizi nyuzi zote za nini uvccm kuhangaika na chama kilichoshinda 1% ya kura wiki jana tu? Mnateseka sana na nyuzi mpya kila dakika kuhangaika na chama kilichokufa?

Kina influence gani wakuu mbona taharuki ni kubwa sana? Maisha yetu yametishwa na ujio wa Simba?
 
Chairman wa sasa wa Chadema Taifa, Freeman Aikaeli Mbowe, akizungumzia kusudio la Tundu Antipas Mughwai Lisu kugombea uenyekiti wa Chadema Taifa, kwa namna yoyote ile atakua ameingia kwenye trap au mtego wa kisayansi alotegwa na kukoleza au kuzidisha joto, uhasama na vita ya madaraka ndani ya chadema hususani dhidi ya nafasi ya uenyekiti wa Chadema Taifa.

Tundu Lisu akijibiwa azma yake hiyo na chairman Freeman Mbowe, atakua amefanikiwa kumuingiza mbowe mtegoni, na ndipo sasa mambo na madudu mengine mazito zaidi na muhimu sana dhidi ya chairman Mbowe yataibuliwa na kuwekwa hadharini.

Na hilo ndilo lengo hasa la Tundu Lisu. Na huo ndio utakua mwanzo wa safari ya kujiengua chadema na kuelekea kwingineko kula maisha au kupata nafasi na fursa ya kugombea urasi uchaguzi mkuu ujao Oct 2025, endapo hoja na tuhuma zake dhidi ya chairman Mbowe zitapanguliwa kwa ufasaha.

Nadhani Tundu Lisu ana mambo mengi mno moyoni dhidi ya uongozi wa chadema Taifa, hata hivyo, mpaka kufikia uamuzi wa kutaka awe mwenyekiti wa Chadema Taifa. Tundu Antipas Mughwai Lisu, anahitaji mambo mawili tu kwenye vita hii. Ni awe mwenyekiti wa Chadema Taifa, au kujiengua chadema na kutafuta fursa za kisiasa kwenye vyama vingine vya siasa nchini.

Na hili linaweza kua ni shinikizo kutoka nje ya nchi, hasa kutoka kwa wale wanao wanaombackup yeye na familia yake huko ughaibuni. Ni dhahiri awali alionekana hayupo serious.

Kukaa kimya kwa Freeman Aikaeli Mbowe, kutampasua kichwa na kutamdhoofisha sana Tundu Lisu anaetamani majibizano, na hapo mbowe atakua ameupiga mwingi zaidi, akiendelea na harakati zake za kutetea kiti chake cha uenyekiti wa Chadema Taifa, kadiri ya mipango mikakati yake na ratiba zake, bila kumzungumzia Lisu hata kidogo.

Kwa kufanya hivi, Freeman Mbowe atakua amemkwaza Lisu, na kumlazimisha amchokonoe zaidi zaidi au kujaribu kupaint uongozi wa Mbowe kama kitu ambacho kiliidumaza chadema na kwamba uongozi wake uligubikwa na sintofahamu nyingi sana.

Na Mbowe akiendelea kukaa kimya zaidi bila kujibu chochote, atakua amemchanganya zaidi Lisu na kumjaza hofu ambayo itamfanya atathmini upya mpango na mtego wake huu wa kumchefua chairman Mbowe ili eti yeye aonekane bora zaidi.

Kiufupi,
katika mpambano na mgawanyiko huu ndani ya chadema, kama wadau wa bobevu, tunajifunza na tutabaini wazi nani miongoni mwa mafahali hawa wawili ndani ya chadema, anatumia sayansi ya siasa kufanya siasa na nani anatumia mihemko, chuki na kukurupuka katika kutafuta uongozi wa kisiasa ndani ya chadema.

Unadhani ni nani aliemshinikiza Lisu kuachana na kugombea umakamu mwenyekiti wa Chadema Taifa, na kuamua kumendea uenyekiti wa Chadema Taifa?

Je, ni shinikizo kutoka ndani ya nchi au nje ya nchi?🐒

Mungu Ibariki Tanzania.
Binafsi ninaamini kuwa ndani ya Chama, kwa sasa wajumbe wengi wanatamani kumalizana na Uongozi wa Freeman Mbowe. Ila tu ni nani wa kumfunga Paka Kengele ndiye aliyekuwa anasubiriwa. Kama ni shinikizo basi uwezekano ni mkubwa kwamba Lissu amepata shinikizo kutoka kwa Wajumbe ambao ndiyo wapiga kura..

Ukweli ni kwamba wakati wa Uongozi wake, Mbowe amekikuza sana Chama na kukipatia Umaarufu kilio nao sasa, ni jambo la kumshukuru. Lakini pia tukubaliane na ukweli mwingine kuwa sasa ni vyema akapisha mawazo mapya yaongoze Chama. Wakati wake umepita.

Kuendelea kung'ang'ania uongozi kuna hatari ya Chama kumfia huko mbeleni.
 
Ajabu kwa kweli ,mwanaccm wewe unaionea huruma CHADEMA LISu akigombea ...kweli!

4R yenu ,ilikuwa ni rushwa kwa chairman kumpoza baada ya kumkarisha rumande mwakamzima
 
Anajua lakin anachotaka?
umakamu mwenyekiti au uenyekiti Taifa au vyote kwa pamoja?

sio tamaa na shinikizo la mabwenyenye ya magharibi yanayombackup kama kibaraka wao Africa kwa mgongo wa Chadema Tanzania,kweli?🐒
Acha chuki. Tundu Lissu alishasema amemwandikia barua katibu mkuu wa chama kwamba hana nia tena za kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
 
Kutiliwa shaka na ccm? Hizi nyuzi zote za nini uvccm kuhangaika na chama kilichoshinda 1% ya kura wiki jana tu? Mnateseka sana na nyuzi mpya kila dakika kuhangaika na chama kilichokufa?

Kina influence gani wakuu mbona taharuki ni kubwa sana? Maisha yetu yametishwa na ujio wa Simba?
Gentleman,
mimi ni mbobevu muandamizi makini, huwa sibabaiki hata kidogo.

Ikiwa jambo au hoja ni ya CCM nitaizungumzia CCM, na ikiwa jambo linahusu Chadema nitaizungumzia chadema bila mbambamba yoyote.

Huwa sina mawenge kujichanganya kama ambavyo unajaribu kujiconfuse na kujicontradict mwenyewe..

Sinaga mihemko wala makasiriko yoyote dhidi ya mtu au chama cha siasa..

Ni muhimu kua watulivu na kujifunza mambo muhimu kwenye vyama vya kisiasa hasa nyakati hizi za chaguzi. Itawasaidia sana. Makasiriko na gubu havina maana 🐒
 
Binafsi ninaamini kuwa ndani ya Chama, kwa sasa wajumbe wengi wanatamani kumalizana na Uongozi wa Freeman Mbowe. Ila tu ni nani wa kumfunga Paka Kengele ndiye aliyekuwa anasubiriwa. Kama ni shinikizo basi uwezekano ni mkubwa kwamba Lissu amepata shinikizo kutoka kwa Wajumbe ambao ndiyo wapiga kura..

Ukweli ni kwamba wakati wa Uongozi wake, Mbowe amekikuza sana Chama na kukipatia Umaarufu kilio nao sasa, ni jambo la kumshukuru. Lakini pia tukubaliane na ukweli mwingine kuwa sasa ni vyema akapisha mawazo mapya yaongoze Chama. Wakati wake umepita.

Kuendelea kung'ang'ania uongozi kuna hatari ya Chama kumfia huko mbeleni.
sasa kama ni hivyo kulikua na haja gani kutangaza kutaka kugombea umakamu mwenyekiti, tena kwa mbwembwe na majigambo, huku akiapa kutopambana na Mbowe kwenye nafasi yoyote ya uongozi ndani ya Chadema?

Nini kimebadilika ghafla,
tena kwa dhihaka na kejeli nyingi sana kutamani kugombea uenyekiti wa Chadema Taifa?

ni uchu wa madaraka, tamaa ya vyeo au shinikizo za wanaomfadhili kutoka ng'ambo?

Kama unadai kapata shinikizo la wajumbe wa chama, ni wangapi hao wajumbe na shinikizo lilianza lini?🐒
 
Mbowe akiendelea kung'ang'ania kiti atazidi kupoteza credibility yake.

Siasa ni mahesabu, ni game of attractions, kwa sasa mwenye amsha amsha na anayependwa mtaani ni Lissu.

Wakimpa Lissu CHADEMA itajipatia uhai mpya ambao unaweza kuing'oa Kijani mwakani.

Kijani mkimuweka mama kama mgombea na Lissu awe ndiyo mwenyekiti, basi tegemeeni yasiyowezekana.
Hawajui
 
Acha chuki. Tundu Lissu alishasema amemwandikia barua katibu mkuu wa chama kwamba hana nia tena za kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
Gentleman,
siwez kumchukia mtu ambae nafaa kumuhurumia.

Nia ya awali ya kugombea umakamu uenyekiti ilitoka wapi, na sasa tamaa ya kuutaka uenyekiti kamili Taifa imetoka wap?

alisense nini kule kwenye umakamu uenyekiti, na amenusa nini kwenye uenyekiti Taifa, hata kukosa msimamo?🐒
 
Ajabu kwa kweli ,mwanaccm wewe unaionea huruma CHADEMA LISu akigombea ...kweli!

4R yenu ,ilikuwa ni rushwa kwa chairman kumpoza baada ya kumkarisha rumande mwakamzima
Gentleman,
habari ya huruma hapa hakuna, japo ni muhimu kumuonea huruma lisu kwa kuamua kuonja sumu kwa ulimi.

hata hivyo,
ni muhimu sana kujifunza kati ya mafahali hawa wawili wa kisiasa Chadema, nani anatumia sayansi na nani ana kurupuka katika kufikia azma yake ya kisiasa ndani ya chama hicho 🐒
 
unamanisha mbowe aendelee azima yake bado(20 yrs of )
 
Gentleman,
Yapo mambo muhimu sana kujifunza

kwanza,
ni muhimu kujifunza kwenye hili, Je, ni tamaa au shinikizo la nje, Lisu kuacha kugombea umakamu mwenyekiti na kuutaka uenyekiti Taifa?

Jambo la pili,
Ni muhimu sana kujifunza, kati ya mafahali hawa wawili nani anatumia sayansi ya siasa na nani mkurupukaji katika kufikia azma zao za kisiasa?

Jambo la meisho,
makasiriko si muhimu sana kwenye hoja hii ya maana mno asubuhi hii, kua muungwana 🐒
Tunakuja na Lissu!
Dume linalotembea na risasi mwilini,he has nothing to loose, siasa nyepesi hazitaipeleka hii nchi mahali!
 
Back
Top Bottom