Najua baadhi ya watu hawataki kabisa kusikia haya majina manne kwasababu ya madhaifu yao, ila ukweli hakuna mwanadamu asiyekuwa na mapungufu. Ukimkataa mtu kwasababu ya udhaifu wake umekataa na nguvu/karama au kipawa ambacho Mungu amekiweka ndani yake.
Jambo moja ni kweli na limehakikishwa kabisa, huwezi kupenda sukari peke yake maana ujue si kila wakati utatumia sukari, kuna wakati chumvi unayoichukia wakati wa kulamba sukari nayo utaihitaji.
Binafsi hawa wanasiasa wanne nawaona kama chumvi, wanaweza kutumika kama chachu ya kuleta mabadiriko katika uongozi wako kama watajirekebisha kidogo, wakipunguza baadhi ya vitu kama kujitukuza, wakijinyenyekeza watatufaa sana watanzania kwasababu wana uthubutu pia ujasiri wa kusimamia wanachokiamini.
Nimalize kwa kusema kuwa hata kama unapenda sukari namna gani huwezi kuiweka kwenye mboga. Pls Mh Rais wape nafasi ya kututumikia watanzania.