Ndugu salaam,
Kama mlivyoshuhudia kuwa Rais Magufuli alilieza taifa na chama chake kuwa akishamteua MTU cheo chochote basi aridhike na cheo hicho, kauli hiyo ilikuwa na lengo la kuwakataza wateule kutoingia majimboni kusaka ubunge.
Kufuatia agizo hilo baadhi wametii hasa wale waoga na ambao hawana ukaribu sana naye. Wale wenye ukaribu naye hawajatii tamko hilo kwani wamejitokeza majimboni na pia JPM kama anavyopenda kuitwa aliongeza kuwa kama mtu aliyemteua akikaidi agizo hilo basi aombe siku ya kupitisha majina akute siku hiyo ameamka vizuri la sivyo atakatwa jina.
Baada ya baadhi kukaidi si kwamba hawa waliokaidi wamepata baraka zake? Na kama hawajapata baraka zake watakatwa?na kama wakipita bika kukatwa hii haionyeshi kwamba huyu jpm ni mbaguzi? Mbaguzi Kwa maana wengine atakuwa amewaachia wajinafasi ili wengine amewafungia kwenye chupa.
Lakini pia, hawa watia nia waliodharau agizo la JPM wametia nia na makada wengine ambao sio wateule, ikitokea kada kamzidi mteuliwa jeuri je atapitishwa?na kama asipopitishwa atakubali kupigia tarumbeta chama miaka nenda rudi ili hali hathaminiki?
Achilia mbali Malaya wa kisiasa waliojiuza, nao atalazimisha wapitishwe walipwe fadhila? Na kama wakipitishwa kwa lazima, hawa makada waliojenga chama kwa jasho na damu wataridhika kukatwa sababu ya wahamiaji?
Naiona kauli halisi ya mwalimu Nyerere Kwa mbali ikijongea chamani kwenye kijani kuwa "Upinzani wa kweli utatoka ndani ya kijani"
CCM mtatoboa October 2020?
Swelana.