TAMKO: Baraza la Maaskofu Katoliki walaani mauaji Kibiti na shambulio kwa Tundu Lissu

TAMKO: Baraza la Maaskofu Katoliki walaani mauaji Kibiti na shambulio kwa Tundu Lissu

Kaka mbona unauliza maswali ya kipuuzi? Leo tu polisi wamejibu kuhusu kachero wao aliyekuwa NRB Kenya, nani aliwapekekea habari? Si wamezitafuta mtandaoni! Ni kazi yao kufanya upelelezi. RPC Dodoma ameomba wenye taarifa waisadie polisi! Makonda alikuwa na taarifa za Roma, kwanini hakuhojiwa? Press conference aliyofanya ilivamiwa na Mwakyembe ili kumfunga mdomo [emoji22][emoji22][emoji22]

Sent using Jamii Forums mobile app
Police lazima wakanushe uvumi unaowachafua...ila tuhuma za jinai lazima ziripotiwe Police ili zifanyiwe kazi
 
Hii ni Taasisi yenye heshima hivyo haifai kukurupuka kama unavyotaka. Kulaani bila kujua nini kinafanyika sio uungwana.
 
Wamechelewa sana....
Mkuu sema hujafikiri mara mbili,ungepata jibu,Kanisa katoliki ni Taasisi,sio mali ya mtu mmoja,,,Askofu mmoja yuko tunduru masasi mwenzake yuko kagera.....mwingine yuko Lindi mwenzake yuko arusha,,,,,,je hawa wote ili watoe TAMKO la TEC,kumbuka wako maaskofu zaidi ya 35,wanaweza kuwa fasta kama gwajima na saccos yake,ambaye hasubiri yeyote kujadiliana nae, na by the way gwajima anayatumia haya matukio kupata Kiki,nani angemjua gwajima kama asingemtukana Pengo, sasa kanisa katoliki halifuati upepo,,,,linapima jambo kabla halijazungumza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna maswali ambayo sijapata majibu hadi leo kuhusu viongozi wetu wa dini. Iko hivi: Kwa wakristo waumini huitwa kondoo na kiongozi huitwa mchungaji. Kwa maagizo ya Yesu ni kwamba mchungaji anapaswa kuwachunga kondoo, kuwalisha, na kuwapigania na ikibidi hata kutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. Ndivyo alivyofanya Yesu ambaye ndiye mfano wa utumishi kwa wakristo. Ajabu ni kwamba viongozi wetu wa dini hawajishughulishi na matatizo ya waumini wao. Wao hutaka tu kuwaona waumini wao kwenye nyumba za ibada na baada ya hapo hawa viongozi hawana habari na muumini wao nje ya nyumba ya ibada. Hii ni kinyume kabisa na Yesu aliyekuwa akienda hadi nyumbani kwa kondoo wake kutatua matatizo mbalimbali na kutoa huduma za kimwili na kiroho. Wakristo watakumbuka jinsi Yesu alivyojishughulisha sana na matatizo ya wafuasi wake na watu wengine wengi. Kwa ujumla viongozi wa dini wa sasa hawajishughulishi na waumini wao kwa matatizo wanayokumbana nayo. Sana sana akifa watapelekewa taarifa tu na kuja kuzika na kuondoka. Hata hospitalini hawaendi kumjulia hali.

Najiuliza, je, kwa mfano sote tunajuaTundu Lissu ni mkristo mzuri wa dhehebu la Katoliki. Hatujamwona kiongozi wake hata mmoja pale hospitali Dodoma. Sasa huwa najiuliza, ina maana kiongozi wangu wa kiroho anakuwa ni kiongozi wangu ninapokuwa salama tu au hata nikikutwa na matatizo? Kwa nini muumini akipatwa na matatizo viongozi wake wa kiroho hujificha? Kwa nini wanajitenga na masaibu wapatayo waumini wao? Mbona viongozi wakubwa wakubwa kila siku tunawaona wakiwaombea?

Siyo Lissu tu, wapo watu wengi sana wameumizwa na kuteswa na kupotezwa lakini tunajua watu hawa wana viongozi wao wa kiroho ambao wapo kimya kana kwamba kondoo wao ni salama tu. Kuna nini? Au kama alivyosema Mkuu wa Kaya nao ni sehemu ya serikali na wametumwa tu kujifanya ni viongozi wa kiroho kumbe wamepandikizwa kwa kazi maalum na wengine ndio wang'oa kucha wakubwa. Hiyo dhambi mtaibeba msipo tubu na kubadilika.
Mkuu umenena vyema.
Siwezi kuongelea madhehebu mengine, lakini wakatoliki wamenikwaza sana
Nikiri kuwa Mimi ni mkatoliki lakini yanayoendelea Kwa kanisa katoliki hasa Tanzania wamenikwaza.
Ni imani ambayo inawasubiri watu wake kupata matatizo? Naondoa hiyo dhana. Ni imani unavyosubiri kuzika ? Iko wapi injili ya kuhusu ubinadamu na namna Bora ya kuishi?
Ni hivi alivyofundisha Yesu? Naogopa kwamba tunaacha kuangalia maisha ya watu sijui ni hofu au kuna agenda nyingine.
Nimeona tano la TEC kuhusu, Lisu na yanayoendelea lakini mbona mko kimya. Si kinachoendelea ni sawa na maandiko yaliyokuwa ukutani? Vipi mliyaona ya JK na sasa hamuoni?
Nasikitika kuwa miongoni mwenu.
Get well Tundu Lissu the people's watchman.
 
Maaskofu mutatuangusha sisi wakatoriki, acheni mahaba yenu kwa baba jesca la sivyo mnatuharibia kanisa

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa akili finyui Hivi Heri uamie kwa Gwajima. Nikwambie iwe Leo Au kesho. Kanisa Katoliki haliwezi kujiunga na siasa za maji taka. Kupinga tu. Ndo mana nakushauri Uhame. Huku hukumu huja kwa ushahidi Sio pumba za kiflash. So mtukane tu maaskofu wetu mana Ndo akili mliyo nayo. Kwenu Demokrasia ni kuwa upande Wa Chadema
 
Rais magufuli amezungumza hayo wakati akizindua radar katika uwanja wa ndege wa JK nyerere leo hii,pia amesema kuwa uchumi wa nchi yetu imekua kwa asilimia saba.
 
Rais magufuli amezungumza hayo wakati akizindua radar katika uwanja wa ndege wa JK nyerere leo hii,pia amesema kuwa uchumi wa nchi yetu imekua kwa asilimia saba.
Ndio maana nimeshauri hawa viongozi wa serikali wanyamaze au watafute meza ya mazungumzo na kada mbalimbali.

Sasa kama ni kweli raisi kayasema hayo,basi hii nchi inahitaji raisi mwenye upeo wa kuona mbali.
 
Back
Top Bottom