Tamko kuhusu JamiiForums kuendelea kuzuiliwa kupatikana nchini Tanzania

Tamko kuhusu JamiiForums kuendelea kuzuiliwa kupatikana nchini Tanzania

Hadi hapo vinyago aina ya Gerson Msigwa na Mkurugenzi wa TCRA vitakapodhibitiwa tusitegemee kamwe kuwepo na uhuru wa vyombo vya habari.

Vinyago hivi hapo wakati utakapowadia ni lazima vjijibu mchango wao katika ukandamizaji wa waTanzania. Hawa ni viungo muhimu katika uovu wanaofanyiwa waTanzania.
 
Kwa watumiaji ambao hampendi kutumia VPN(kosa kisheria).Tumia JF web version pia tumia operamini kama browser(ukiingia usifute browsing history au ku-clear cache) ndio salama yako na utaipata JF wakati wowote
Watazingua na huku hawa TCRA kwanini umetoa boko wewe f hujui hao makenge namaanisha hao TCRA wanachofikiria wao ni kufungafunga tu?
 
JF ina taarifa muhimu za usitawi wa Taifa hili kwa miaka zaidi ya 20 sasa. Ni mtandao wenye rekodi ya utawala wote wa JK, utawala wote wa Magufuli, na utawala wote wa Samia hadi sasa katika nyanja nyingi za kisiasa, kiuchumi, kijamii n.k. Ni mwendawazimu pekee anayeweza kujaribu kuiua JF, maana yake anapoteza hazina yote ya maarifa ambayo taifa hili limeyakusanya kupitia mtandao huu kwa miaka yote hiyo. Leo huwezi kugoogle chochote kujusu Tanzania then usikute taarifa kutoka JF zikiwa top katika search.

Kama serikali ikizingua, basi wamiliki wa JF watafute buyer kutoka Kenya wamuuzie mtandao huu na information zake zote then tuje tuone ni Kenya au TZ itakayonufaika na vast information iliyomo ktk servers za JF.
 
Haya mambo ndiyo yanayodumaza ukuaji wa mawasiliano na habari, maana fikra tunduizi zinakuwa zimezimwa. Huu ni wendawazimu na ujuha kuzuia maendeleo katika mawasiliano na habari, ni kudumaza fikra za watu
 
​
TAARIFA KWA UMMA​


Mnamo Septemba 6, 2025, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilisitisha Leseni ya Maudhui Mtandaoni ya JamiiForums na kuzuia upatikanaji wa jukwaa kwa siku 90, kwa madai ya ukiukwaji wa Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta. Pamoja na kutambua athari kwa haki ya wananchi kupata taarifa na kutoa maoni, tulitii agizo hilo hadi huduma ziliporejeshwa Desemba 06, 2025.

Tangu kurejeshwa, tumepokea taarifa kutoka kwa watumiaji wetu wa Tanzania kuwa kuanzia Desemba 7, 2025 hawawezi kufikia jukwaa bila kutumia mbinu au nyenzo za ziada.

Tunapenda kuufahamisha umma kuwa hatuhusiki na hali hii, na tunalaani vikali kitendo cha kuzuia upatikanaji wa jukwaa bila taarifa rasmi kwa umma, kwani ni kinyume na ukiukwaji mkubwa wa haki ya kutafuta, kupokea na kutoa taarifa.

Tunatoa wito kwa yeyote au mamlaka yoyote inayohusika kuondoa mara moja vizuizi hivi na kuruhusu wananchi kupata huduma bila vikwazo.

Tutaendelea kusimamia haki za kidijitali na uhuru wa watu kujumuika mtandaoni, kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo, na kuhimiza uwajibikaji katika jamii.

Desemba 12, 2025​

View attachment 3514831
Poleni
 
Kiongozi wa taasisi yenye mamlaka ya mawasiliano anapokuwa hana maono ya kukuza wigo wa mawasiliano nchini hudumaza nchi katika sekta ya mawasiliano. Dunia inaenda kwa kasi kubwa sana katika nyanja ya mawasiliano, nchi itaachwa nyuma sana kimawasiliano kama kiongozi hana maono ya kuona ni kwa namna gani nchi isiachwe nyuma katika sayansi na teknolojia za mawasiliano na habari. Kiongozi wa namna hii huua ari na ubunifu wa wananchi wake
 
Mambo kama haya ndio maana watu wanagoma nakufanya maandamano!

Hili taifa lina viongozi washamba sijapata kuona sijui hata wanaogopa nini kusemwa kwenye uongozi kupo tu hata baba anasemwa kwenye familia sasa nyinyi ni kina nani...?

Kama hivi ndivyo mnavyoendesha mambo basi tarajieni migomo na maandamano zaidi na zaidi maana sikio la kufa halisikii dawa!.
Unaweza kugoma au kuandamana? au wewe hayakuhusu?
 
JF ina taarifa muhimu za usitawi wa Taifa hili kwa miaka zaidi ya 20 sasa. Ni mtandao wenye rekodi ya utawala wote wa JK, utawala wote wa Magufuli, na utawala wote wa Samia hadi sasa katika nyanja nyingi za kisiasa, kiuchumi, kijamii n.k. Ni mwendawazimu pekee anayeweza kujaribu kuiua JF, maana yake anapoteza hazina yote ya maarifa ambayo taifa hili limeyakusanya kupitia mtandao huu kwa miaka yote hiyo. Leo huwezi kugoogle chochote kujusu Tanzania then usikute taarifa kutoka JF zikiwa top katika search.

Kama serikali ikizingua, basi wamiliki wa JF watafute buyer kutoka Kenya wamuuzie mtandao huu na information zake zote then tuje tuone ni Kenya au TZ itakayonufaika na vast information iliyomo ktk servers za JF.
hoja nzito sana mkuu ,ni wachache watakuelewa kwa hili,

Ni kweli jf sio jukwaa la mchezo kama wengi wetu tunavyochukulia poa , badala serikali kujifunia kuwa na watu madhubuti ,mfano founder wa jukwaa hili , ila ndo wanaweka mitego kuwaangamiza , serikali kwao wawekezaji ni wale wa kutoka nje sio wazawa sio.


Bila uchawa nilitegemea jf serikali kutoa mpaka ruzuku pale ili kiwe jukwaa kubwa bila kulingilia , maana pale wapo watu wameajiliwa .

Hivi nchii hii akili kubwa iliondoka na baba yetu Nyerere au ,mbona sielewi wakuu,

Mfano tumezoea imani za dini anzia nje na kuletwa kwetu, ila yupo mchungaji akaanzisha imani na ndani ya nchi yetu na kupeleka kataika mataifa mengine , leo tunambagaza , na kuishi kama digidigi katika nchi yake kweli.

Nachoka sana wapendwa
 
Msiangalie upande mmoja tu

Ukweli ni kwamba kuna watu wanatukana sana humu hadi kupitiliza kisa tu unatumia fake ID

Siitetei serikali ila na nyinyi pia kuna umhimu wa kubadilika mnatukana sana bila mipaka wala staha
 
Hivi kwani JF si Ina wanasheria wake. Wao uibukaga siku uongozi wa JF ukiburuzwa mahakamani tu.

Binafsi sijawahi hata siku moja kusikia wanasheria wa JF walau wakifungua miscellaneous application zidi ya TCRA (though not expecting the court to decide in their favour).

Lakini it’s time to check these lazy JF lawyers too, TCRA ni taasisi iliyoanzishwa na yenye miongozo ya kazi kisheria.

Jamaa huko TCRA wamekuwa ni watu wa kujiamulia tu kwa sababu most times being unchallenged kwa wao kutofuata sheria na kanuni za nchi.

Sasa ndio kama hii mada ni kama vile uongozi wa JF unatuambia kinachoendelea ni hewala tu. Zero attempts to fight for their entitlement by law.

Hata kama ushindi shauri (we get it, mahakama zipo compromised) chachafya basi kidogo utoke hata kwa makeke. Siku nyingine jamaa kabla hawajafungia JF wafikirie mara mbili, kuna kwenda mahakamani, sijui media attention kwa serikali on gagging order free speech, limiting social interaction and so forth na pressure ya wanasheria wa JF.

Let’s face it watu wanaochangia forums nyingine nje ya siasa ni wengi kuliko mambo ya siasa surely the law protects their right to socialise.

Sio JF utasikia tumefungiwa that’s it, hawa challenge hayo maamuzi kwa taratibu za legal process (on dispute resolution) zilizowekwa.

Fire the lawyers unless they are working on ‘zero hours contract’. Otherwise these people don’t deserve a monthly check.
 
JF ina taarifa muhimu za usitawi wa Taifa hili kwa miaka zaidi ya 20 sasa. Ni mtandao wenye rekodi ya utawala wote wa JK, utawala wote wa Magufuli, na utawala wote wa Samia hadi sasa katika nyanja nyingi za kisiasa, kiuchumi, kijamii n.k. Ni mwendawazimu pekee anayeweza kujaribu kuiua JF, maana yake anapoteza hazina yote ya maarifa ambayo taifa hili limeyakusanya kupitia mtandao huu kwa miaka yote hiyo. Leo huwezi kugoogle chochote kujusu Tanzania then usikute taarifa kutoka JF zikiwa top katika search.

Kama serikali ikizingua, basi wamiliki wa JF watafute buyer kutoka Kenya wamuuzie mtandao huu na information zake zote then tuje tuone ni Kenya au TZ itakayonufaika na vast information iliyomo ktk servers za JF.
Mkuu wewe ni mzalendo wa Taifa lako , nimesoma andiko lako hili mara kumi kwa mara ya kwanza hapa jf ,mtu wa maana sana , Mwigulu nchemba , vyovyote vile hawezi helewa umeandika nini, mkuu Mungu akutunze
 
Cha ajabu machawa yamejaa humu JF yanapandisha nyuzi kila sekunde

Na yanatumia VPN Kuja kuchawia na yanalipwa buku 7

Ushauri
viongozi wa JF Muwe mnafuta nyuzi zote za machawa na serikale yao ya bi chura

Unampaje airtime pimbi aliyekufungia mtandao?!
 
Back
Top Bottom