TANESCO: Hatuhusiki na kukatika umeme kwa Mkapa. Alaumiwe waziri wa Utamaduni na Michezo
Nashangwaza kwamba pamoja na mvua kuebdelea kunumyesha still kuna migao ya umeme, sasa kama Masika hii kuna migao ya umeme vipi kiangazi kikianza? Ni vitu vya kushangaza sana kwa kweli.

Mfano kwa Arusha huku kuna maeneo mfano Monduli walichukua umeme saa 1 hadi sasa hivi hawajarudisha, na Arusha mjini ndio wamerudiaha imepita kama nusu saa hivi.
 
Makamba makamba makamba kama unakata umeme mara mbili kwenye mechi kubwa ,vipi huko Maswa watakuwa na hali gani?
 
Makamba ni manager wa uwanja wa taifa? Tangu lini?
Tuache upumbavu ndugu watanzania mnaojiita wazalendo wa kisukuma
 
IMG_5691.jpg
 
Hilo jenereta litakuwa limetengebezwa China. Yaani mamlaka ya uwanja wa Taifa wanashindwa kununua jenereta la ihakika la kitoka Germany au Italy?

Chinese products are the most expensive items ina this globe when you consider efficiency, time and productivity.
 
Waziri wa nishati mh Makamba amesema leo iliamuliwa Umeme wa Tanesco usitumike litumike Jenereta lakini kwa bahati mbaya limefeli lakini Umeme wa Tanesco upo

Mungu ni mwema Wakati wote!
Endelea tu kututia aibu mtoto wa mlamba asali, kwanini litumike jenereta ilihali umeme upo, aibu mpaka lini? halafu ndio anataka awe raisi.
 
Huyu jamaa kiukweli amerudishwa na kupewa madaraka ila mmh hapana

Anaemwamini amwamini tu kivyake😎
 
Ulikuwa ni uzembe sana manager wa uwanja lazima awajibishwe kwakweli. Mbona chamanzi hakuna haya mambo????
 
Yaani waliogopa umeme kukatika, wakaamu kutumia jenereta likazingua, wakaona Bora watumie umeme
Akili za wapi hizi Sasa ? Yaan unawasha jenereta unaacha umeme wa tanesco are you serious Marope ?
 
Utasikia zinahitajika trilioni 1 kujaza maji bwawa la Nyerere.

I don't trust this guy.
 
Wanafiki wanaumbuka, haya handshake leta umeme
 
TANESCO wameruka mbali tukio la kuzimika umeme Taif wakati MECHI ikiendelea. Taarifa Yao ina leta maswali yenye viashiria vya wizi kama ifuatavyo

1. Kwanini uwanja wa Taifa waliamua kutumia umeme wa jenereta badala ya umeme wa TANESCO?

2. TANESCO na Uwanja wa Taifa yote ni serikali, kwanini wanarushiana lawama?

3. Hii Hali mbona tulikuwa hatuisikii awamu iliyopita?

4. Fedha za mapato ya uwanja zinatumika kufanya KAZI gani?

5. Nani mtaalam wa ufundi? NI Watanzania au kuna kampuni ya kichina inalipwa kuwasha na kuzima jenerator?

6. Hakuna wanufaika nyuma ya hizi hujuma? Kwamba wanaonyesha kuna hitilafu ili walipwe au watengewe fedha au wapata njia ya kuanzisha mchakato wa kumpa MTU tenda?
Aingii akilini kuwa jenereta zimezimika, na umeme wa TANESCO upo, usipokee mara moja? AIBU au kama ulivyohoji ni mbinu ya kumpa mtu tenda ya kuleta jenereta mpya au kutengeneza, kwani imetokea tena kwenye mechi ya kimataifa
 
Back
Top Bottom