TANESCO kuzima Umeme siku 2 kwa saa 12 (Agosti 26 -28 2023), Mikoa 15 gizani

TANESCO kuzima Umeme siku 2 kwa saa 12 (Agosti 26 -28 2023), Mikoa 15 gizani

Shirika hilo la Umeme limesema njia ya umeme itakayozimwa ni kutoka Kidatu kwenda Kihansi kwa siku mbili kuanzia Agosti 26 hadi 28 2023

Umeme utakuwa wa mgawo kwa Saa 12 kuanzia Saa 1 Jioni hadi 12 Asubuhi huku Mikoa ya Njombe, Ruvuma na Mbeya ikitarajiwa kuathirika

Mikoa mingine ni Dodoma, Singida, Manyara, Arusha, Shinyanga, Kilimanjaro, Simiyu, Tabora, Mwanza, Geita na Iringa

Vipi Mdau, umejiandaaje kukabiliana na Mgawo huo?
Kalemani yuko wapi siku hizi!
 
Mtanikumbuka Hayati Magufuli
 
Wanavyotoa taarifa unaweza kusema kama vile huwa hawakatagi umeme, et tahadhali ya umeme kukatika siku mbili wakat kila siku wanakata hata hiyo tabadhari wasingeitoa wala tusingeuliza chochote maana imekua kawaida umeme kutokuwepo
 
Hivi hii nchi inaendeshwa na watu/binadamu au inaongozwa na mashetani ktk sura ya binadamu lengo kubwa likiwa ni kutesa na kuhangaisha watu?

Unawezaje kuzima umeme (nyenzo kuu ya uzalishaji mali) kwa siku mbili mfululizo kwa karibu ¾ ya eneo la nchi yote kwa wakati mmoja na wakati huohuo serikali ikitaka kodi na matozo yalipwe na wananchi haohao wasiozalidha kwa siku hizo huku serikali hiyo hiyo ikiwa ime - shutter nguvu yao ya uzalishaji?

Na ina maana nchi haina alternative power kabisa kiasi kwamba kukitokea dharula ya siku mbili au tatu kama hii alternative hiyo itumike kwa wakati ambapo suluhu ya tatizo ikitafutwa.?

Hizi ndizo akili za watu wa serikali ya CCM..
 
Mwanzo walisema Magufuli aliharibu miundombinu kwa kutokufanyika repair,wakakodi mtambo toka india kwa ghar bilioni60kila mwezi kwa madai yao ya uongo kuwa suluhisho la matatizo ya umeme kumbe hamna kitu.Umeme unaendesha uchumi,unapoweka watu incompetent unakuwa unahujumu uchumi wa nchi
 
Back
Top Bottom