We unaishi Moshi ipi? Hakuna mji umeme unasumbua kama Moshi na ArushaWakati mikoa mingine ikipambana na tatizo la mgao wa umeme,kwa wenzetu moshi hali ni tofauti kabisa
Huku umeme ni angalau 24 hrs 7 days kukatika kwa umeme ni nadra sana na ukikatika haizidi nusu saa usharudi
Unaweza kukaa wiki mbili mfululizo umeme usikatike hata sekunde
Kwa hili napongeza sana
Huku ndo pakuinvest maana hakuna tatizo la umeme ukiliganisha na mikoa mingine tz
Huko ni umeme wa kuazima Mimi nilikuwa naongelea ule umeme wa kwetu wenyeweUshawahi kaaa BUKOBA?
Mbona hapo juu kama comments 6 za wakazi wa moshi wanalalamika kuna mgao wa hatari huko moshi ?kama ndio hivyo unavyosemaHata bukoba hawana tatizo la umeme
Hujui business
Mikoa ambayo wananunua umeme kutoka grid za nchi jirani huwa haukatiki , pamoja na kwamba kule wanaponunua umeme unaweza kuta nchi zao zina shida ya umeme ila kwakuwa wanauza wanakuwa na priority kwa umeme wa ku export usikatike,
Ndo maana umeme wa kagera unaotokana na owen falls za uganda haukatiki lakin ukivuka ukaenda tu mtukula na kyotela upande wa uganda wanakuwa na shida ya umeme wakati wanaona nguzo kubwa za kupeleka Tz Umeme zikiwapita,
Hata uko msumbiji na Rwanda tunapouza umeme sisi tunaowapa haukatiki ila wa kwetu unakatika,
Logic kama mama anauza mandazi hawezi toa mazuri mazuri mnywee chai, atatoa masalia na kuwaheshimu wateja ,ila ninyi mnywee masalia, ili kuendelea kuvutia wateja,
Hivyo hata kwa moshi ni hivyo hivyo
Britanicca
kweli ila tatizo la umeme moshi si kama darMbona hapo juu kama comments 6 za wakazi wa moshi wanalalamika kuna mgao wa hatari huko moshi ?kama ndio hivyo unavyosema
Basi kuna wachaga wengi kama moshi [emoji16]Mbona huku kwetu masaki umeme ni 24/7 ,sijawahi kushuhudia ukikatika
Umeongea ukweliMoshi ni kamji kadogo! Hata ukitumia injini ya Bajaji yangu unaweza kuzalisha umeme wa kulisha Moshi nzima.🙄
Mbaya zaidi wachaga walivyo wabahili, nyumba ya vyumba saba inawashwa taa moja na kativii huwa ni kale kadogo ka nchi kumi na saba! Kwa hiyo hakuna matumizi makubwa ya umeme.
Umeomba kwa jina gani , lini na namba ya simu tafadhaliJaman tanesco naomba kuuliza swali. Mimi nipo wilaya ya karatu nmefanya utaratibu wakuunganishiwa umeme nyumbani ila naambiwa ili niunganishwe lazima nisubirie mita, Na wanasema mita lazima zitoke dar ndo mnaposajili hizo mita kitu ambacho naona sio sawa.
Je ni kweli mita za tanesco zinasajiliwa dar tu?
Alafu pia mbona mnakata umeme ivo mnatufanya wafanyabiashara wadogo tupate hasara mwisho wa siku TRA wanataka kodi yao bila kuangalia tumekosa huduma nyingi? Please fanyen mpango umeme uwe wa uhakika.
Heee kumbeStory za watu hapa jf na social media kulalamika umeme kukatikakatika ila kwa mwanza haikuwepo mpaka nikafikia hatua nikajua ni ya majizi,mapiga deal na yenye vyeti fake yanaongea uongo ili serikali hii inayojali wanyonge ionekane haifanyi kitu na kiuhakika niliungana na Rais wetu mpendwa,Musa wetu anayetupeleka Kanaani nchi ya ahadi katika ku ya enjoy hayo majizi yakilalamika
Sasa bwana,hii week iliyopita hadi leo ni timbwili katika jiji hili liliolompa DR JPM Urais,tunakatiwa umeme balaa,10 minutes ago wamekata,jana walikata asubuhi hadi jioni,siku tatu zilizopita mfululizo wanakata usiku kucha
TANESCO jamani,Hii ni Mwanza,hizo katakata zenu za umeme kafanyeni kimara na Moshi
Kuweni na human face pande hizi,eboooo.
Tunaomba namba yako ya simu mpendwa mtejaTANESCO mimi ni mkazi wa Mbeya Mjini, Kero yangu ni kuhusu mgao wa umeme ambao unaonekana una chembechembe za upendeleo, Karibu kila siku umeme unakatika kuanzia asubuhi hadi jioni maeneo ya BLOCK - T na Mwanjelwa lakini cha ajabu forest ya zamani maeneo ya kuanzia kule mitaa ya check-point umeme hamkati toka mgao uanze, Ninaongea kwa ushahidi na sio kwa maneno tu, Tunaombeni mtatue tatizo hili maana ni kero sana kwa wakazi wa BLOCK- T ambao kwa wiki 2 mfululizo lazima umeme ukatike asubuhi na unarudi usiku, Huo umeme ambao haukatikagi forest ya zamani tunaombeni nao uwe unagawika ili hata sisi wakazi wa block - t tuweze kunufaika na huduma yenu..NAWASILISHA