TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Wakati mikoa mingine ikipambana na tatizo la mgao wa umeme,kwa wenzetu moshi hali ni tofauti kabisa
Huku umeme ni angalau 24 hrs 7 days kukatika kwa umeme ni nadra sana na ukikatika haizidi nusu saa usharudi
Unaweza kukaa wiki mbili mfululizo umeme usikatike hata sekunde
Kwa hili napongeza sana
Huku ndo pakuinvest maana hakuna tatizo la umeme ukiliganisha na mikoa mingine tz
We unaishi Moshi ipi? Hakuna mji umeme unasumbua kama Moshi na Arusha
 
Hata bukoba hawana tatizo la umeme

Hujui business

Mikoa ambayo wananunua umeme kutoka grid za nchi jirani huwa haukatiki , pamoja na kwamba kule wanaponunua umeme unaweza kuta nchi zao zina shida ya umeme ila kwakuwa wanauza wanakuwa na priority kwa umeme wa ku export usikatike,

Ndo maana umeme wa kagera unaotokana na owen falls za uganda haukatiki lakin ukivuka ukaenda tu mtukula na kyotela upande wa uganda wanakuwa na shida ya umeme wakati wanaona nguzo kubwa za kupeleka Tz Umeme zikiwapita,

Hata uko msumbiji na Rwanda tunapouza umeme sisi tunaowapa haukatiki ila wa kwetu unakatika,


Logic kama mama anauza mandazi hawezi toa mazuri mazuri mnywee chai, atatoa masalia na kuwaheshimu wateja ,ila ninyi mnywee masalia, ili kuendelea kuvutia wateja,

Hivyo hata kwa moshi ni hivyo hivyo

Britanicca
Mbona hapo juu kama comments 6 za wakazi wa moshi wanalalamika kuna mgao wa hatari huko moshi ?kama ndio hivyo unavyosema
 
huku kwetu kahama hatuna shida ya umeme kabsaa labda mvua ikinyesha ndo tanesco wanakata ikiisha wanarudisha tushazoea
 
Kuna sehemu/mikoa ukkata umeme unakua haujasave chochote. Unakuta matumizi yao ya umeme ni kidogo
 
Nimebahatika kupitia sehemu nyingi nyingi lakini nimegundua kati ya sehemu ambazo nimepitia na umeme haukatiki hovyo hovyo ni Bukoba Kagera, kwingine sijui
 
Wale ambao hawategemei Grid ya Taifa ambao wako mipakani wao frequently hawakumbani na tatizo la power outage or Shadow kuna line pia sensitive sana zinatoka bongo mpaka nje Rwanda and malawi Hazikatiki umeme pia
 
Moshi ni kamji kadogo! Hata ukitumia injini ya Bajaji yangu unaweza kuzalisha umeme wa kulisha Moshi nzima.🙄
Mbaya zaidi wachaga walivyo wabahili, nyumba ya vyumba saba inawashwa taa moja na kativii huwa ni kale kadogo ka nchi kumi na saba! Kwa hiyo hakuna matumizi makubwa ya umeme.
Umeongea ukweli
 
Kuna baadhi ya maeneo ya moshi yanatumia umeme kutoka nyumba ya mungu mojakwa moja ndio maana haukatiki ovyo
 
Jaman tanesco naomba kuuliza swali.

Mimi nipo wilaya ya karatu nmefanya utaratibu wakuunganishiwa umeme nyumbani ila naambiwa ili niunganishwe lazima nisubirie mita, Na wanasema mita lazima zitoke dar ndo mnaposajili hizo mita kitu ambacho naona sio sawa.

Je ni kweli mita za tanesco zinasajiliwa dar tu?

Alafu pia mbona mnakata umeme ivo mnatufanya wafanyabiashara wadogo tupate hasara mwisho wa siku TRA wanataka kodi yao bila kuangalia tumekosa huduma nyingi?

Please fanyen mpango umeme uwe wa uhakika.
 
Story za watu hapa jf na social media kulalamika umeme kukatikakatika ila kwa mwanza haikuwepo mpaka nikafikia hatua nikajua ni ya majizi, mapiga deal na yenye vyeti fake yanaongea uongo ili serikali hii inayojali wanyonge ionekane haifanyi kitu na kiuhakika niliungana na Rais wetu mpendwa,

Musa wetu anayetupeleka Kanaani nchi ya ahadi katika ku ya enjoy hayo majizi yakilalamika
Sasa bwana, hii week iliyopita hadi leo ni timbwili katika jiji hili liliolompa DR JPM Urais,tunakatiwa umeme balaa,10 minutes ago wamekata, jana walikata asubuhi hadi jioni,siku tatu zilizopita mfululizo wanakata usiku kucha
TANESCO jamani,

Hii ni Mwanza,hizo katakata zenu za umeme kafanyeni kimara na Moshi
Kuweni na human face pande hizi,eboooo.
 
Jaman tanesco naomba kuuliza swali. Mimi nipo wilaya ya karatu nmefanya utaratibu wakuunganishiwa umeme nyumbani ila naambiwa ili niunganishwe lazima nisubirie mita, Na wanasema mita lazima zitoke dar ndo mnaposajili hizo mita kitu ambacho naona sio sawa.
Je ni kweli mita za tanesco zinasajiliwa dar tu?
Alafu pia mbona mnakata umeme ivo mnatufanya wafanyabiashara wadogo tupate hasara mwisho wa siku TRA wanataka kodi yao bila kuangalia tumekosa huduma nyingi? Please fanyen mpango umeme uwe wa uhakika.
Umeomba kwa jina gani , lini na namba ya simu tafadhali
 
Story za watu hapa jf na social media kulalamika umeme kukatikakatika ila kwa mwanza haikuwepo mpaka nikafikia hatua nikajua ni ya majizi,mapiga deal na yenye vyeti fake yanaongea uongo ili serikali hii inayojali wanyonge ionekane haifanyi kitu na kiuhakika niliungana na Rais wetu mpendwa,Musa wetu anayetupeleka Kanaani nchi ya ahadi katika ku ya enjoy hayo majizi yakilalamika
Sasa bwana,hii week iliyopita hadi leo ni timbwili katika jiji hili liliolompa DR JPM Urais,tunakatiwa umeme balaa,10 minutes ago wamekata,jana walikata asubuhi hadi jioni,siku tatu zilizopita mfululizo wanakata usiku kucha
TANESCO jamani,Hii ni Mwanza,hizo katakata zenu za umeme kafanyeni kimara na Moshi
Kuweni na human face pande hizi,eboooo.
Heee kumbe
 
Kuna maeneo ambayo matatizo ni sugu, kwa mfano waya zimetepeta zinagusa mapaa ya nyumba na nguzo zimeinama zinakaribia kuanguka, ukipiga simu TANESCO, wanakuja wanatazama wanaondoka,

Je usalama wa mtoa taarifa juu ya uzembe wa wahusika unalindwaje?
 
Kwa hyo Leo mmeamua mtulaze na Giza tangu SAA 5 usiku mpaka sasa hivi SAA Saba.
MTAFIKIA KWELI

TANZANIA YA VIWANDA?
 
TANESCO mimi ni mkazi wa Mbeya Mjini, Kero yangu ni kuhusu mgao wa umeme ambao unaonekana una chembechembe za upendeleo,

Karibu kila siku umeme unakatika kuanzia asubuhi hadi jioni maeneo ya BLOCK - T na Mwanjelwa lakini cha ajabu forest ya zamani maeneo ya kuanzia kule mitaa ya check-point umeme hamkati toka mgao uanze, Ninaongea kwa ushahidi na sio kwa maneno tu,

Tunaombeni mtatue tatizo hili maana ni kero sana kwa wakazi wa BLOCK- T ambao kwa wiki 2 mfululizo lazima umeme ukatike asubuhi na unarudi usiku, Huo umeme ambao haukatikagi forest ya zamani tunaombeni nao uwe unagawika ili hata sisi wakazi wa block - t tuweze kunufaika na huduma yenu..NAWASILISHA
 
TANESCO mimi ni mkazi wa Mbeya Mjini, Kero yangu ni kuhusu mgao wa umeme ambao unaonekana una chembechembe za upendeleo, Karibu kila siku umeme unakatika kuanzia asubuhi hadi jioni maeneo ya BLOCK - T na Mwanjelwa lakini cha ajabu forest ya zamani maeneo ya kuanzia kule mitaa ya check-point umeme hamkati toka mgao uanze, Ninaongea kwa ushahidi na sio kwa maneno tu, Tunaombeni mtatue tatizo hili maana ni kero sana kwa wakazi wa BLOCK- T ambao kwa wiki 2 mfululizo lazima umeme ukatike asubuhi na unarudi usiku, Huo umeme ambao haukatikagi forest ya zamani tunaombeni nao uwe unagawika ili hata sisi wakazi wa block - t tuweze kunufaika na huduma yenu..NAWASILISHA
Tunaomba namba yako ya simu mpendwa mteja
 
Back
Top Bottom