TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Nio tandahimba mkoani mtwara nafuatilia makopa ya mihogo.hamna umeme siku tatu mfululizo!!!!sijajua
 
Imeshasemwa hakuna mgao, hivyo vumilia tu ni hali ya mpito hiyo.
 
TANESCO ili ifanye vizuri nafasi ya Director General inabidi waitanganze kwa publically halafu kigezo kiwe mtu mwenye uzoefu wa kuongoza private sector.

Watapata mtu mwenye mtizamo wa kibiashara zaidi na siasa kidogo sana.shirika linaweza kujiendesha kibiashara kabisa bila madhara kwa wananchi.

Halafu ajira iwe ya mkataba wa miaka mitano mitano based on performance wataona mayokeo.sasa wao kigezo kikubwa wanataka awe mhandisi wa umeme.tena aliyewahi kufanya tanesco.kiasi kwamba hawawezi fikiri nje ya box
 
Yaani kama kuna shirika ambalo wakisema livunjwe hata leo nitashangilia ni Tanesco!
Mtu hata kama umeamua kupumzika na kumalizia weekend nyumbani watakulazisha tu utoke, imagine weekend kama hii unaangalia mpira man utd vs brighton huku unasubiria liverpool vs chelsea jamaa wanakata umeme? Mnasababisha twende bar bila kupenda na vyuma vimekaza!
Kazi mnayoweza tanesco ni kukata umeme tu.
Kwanza nilisikia waziri mpya kasema umeme kukatika ni marufuku...vipi mbona ndio anachochea umeme kukatika?!
Hamna shirika nalichukia kama Tanesco maanake hawapitishi siku bila kuniharibia siku!
Ndiyo
Ipo Inaitwa jeshi la polisi baada ya hapo ndo inakuja tanesco
 
Hilo ni tatizo la kuingiza siasa kwenye mambo ya utalaam, huyo waziri mpya wa nishati na mkwara wake wa kuwasha umeme ndani ya siku 10 yuko wapi? Ni aibu sana kwenye chanzo cha gesi umeme hakuna!
 
Poleni...hata mimi naangalia mpira huku nasubiri ukatike! Maisha gani haya....!
Wanakera mnoo kuna kipindi dogo alikua na mitihani ya Necta nilipata shidaa basi tu
Siwapendi tanesco Mimi acha tu

Wanakulazimisha kuvaa nguo usioitaka
 
Back
Top Bottom