TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Yaani kama kuna shirika ambalo wakisema livunjwe hata leo nitashangilia ni Tanesco!
Mtu hata kama umeamua kupumzika na kumalizia weekend nyumbani watakulazisha tu utoke, imagine weekend kama hii unaangalia mpira man utd vs brighton huku unasubiria liverpool vs chelsea jamaa wanakata umeme? Mnasababisha twende bar bila kupenda na vyuma vimekaza!
Kazi mnayoweza tanesco ni kukata umeme tu.
Kwanza nilisikia waziri mpya kasema umeme kukatika ni marufuku...vipi mbona ndio anachochea umeme kukatika?!
Hamna shirika nalichukia kama Tanesco maanake hawapitishi siku bila kuniharibia siku!
Polisi na ile ya makumbusho pale
 
Kwetu sisi hakuna shida ya umeme..........
Lakini hii idara ya police me nadhani ndiyo lijipu kuliko majipu yote nchi hii
 
Labda huko kwenu, hapa kwetu mbona tunashirikiana nao vizuri tu...jana wamekuja kufyeka Maharage yangu wamesema yapo kwenye eneo lao la akiba.
 
Labda huko kwenu, hapa kwetu mbona tunashirikiana nao vizuri tu...jana wamekuja kufyeka Maharage yangu wamesema yapo kwenye eneo lao la akiba.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Aiseee yaan huku umekata hapa ubungo tangu sa 12 nadhan hapa kurud Paka sa6 usiku daah yaani ndani hakukariki

Hivi kama Jijin Hali iko hivi hivi huko kwingine Hali ikoje

Mliopo nje ya dsm hebu mtujuze Hali ikoje ya kukatika katika kwa umeme
 
Kutoa namba yangu ya simu ni hatari kwa usalama wangu kwa sababu mimi ni mwanachama ambae mara kwa mara naikosoa serikali inapokosea, Namba yangu ikijulikana naweza kutafutwa na kupewa kesi ya uchochezi kama mnavyojua.

Kama kawaida ninapokaa BLOCK - T mitaa ya chuo cha teku umeme umeshakatwa tangu saa tatu asubuhi ila cha ajabu nipo hapa forest ya zamani umeme upo kama ilivyo kwa kila siku tangu mgao uanze na ndio naoutumia kutype hapa, Tafadhalini sana nawaombeni mfanye huu mgao uwe wa haki, pia wafanya biashara wa mwanjelwa stendi ya kabwe nao hakuna umeme kila siku kuanzia asubuhi wanapoingia kufanya shughuli zao mpaka usiku wanapomaliza shughuli zao, Nawaombeni sana mfanye haki katika huu mgao, Block -t specifically maeneo ya chuo kikuu cha teku na sisi pia tunahitaji umeme unaokatwa kila siku kama wanavyouhitaji wakazi wa forest ya zamani ambao nahisi hata hawajui kwamba kuna mgao.

NAWASILISHA
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji1] daahhh!
 
Aiseee yaan huku umekata hapa ubungo tangu sa 12 nadhan hapa kurud Paka sa6 usiku daah yaani ndani hakukariki

Hivi kama Jijin Hali iko hivi hivi huko kwingine Hali ikoje

Mliopo nje ya dsm hebu mtujuze Hali ikoje ya kukatika katika kwa umeme
Najaribu kufikiria flyover ya ubungo sijui itakuwa ya ghorofa bila umeme huko juu giza lake litakuwaje?!
 
Back
Top Bottom