Hahaha yaan huku shinyanga ndio usiseme hadi tulishachoka na kuuliza. Umeme unakatwa tu bila hata mpangilio yaan vululu vululu.
Hata kama ni matengenezo, hayo ni matengenezo gani yasiyoisha?
 
Tunaomba namba yako ya simu mpendwa mteja
Kutoa namba yangu ya simu ni hatari kwa usalama wangu kwa sababu mimi ni mwanachama ambae mara kwa mara naikosoa serikali inapokosea, Namba yangu ikijulikana naweza kutafutwa na kupewa kesi ya uchochezi kama mnavyojua.

Kama kawaida ninapokaa BLOCK - T mitaa ya chuo cha teku umeme umeshakatwa tangu saa tatu asubuhi ila cha ajabu nipo hapa forest ya zamani umeme upo kama ilivyo kwa kila siku tangu mgao uanze na ndio naoutumia kutype hapa, Tafadhalini sana nawaombeni mfanye huu mgao uwe wa haki, pia wafanya biashara wa mwanjelwa stendi ya kabwe nao hakuna umeme kila siku kuanzia asubuhi wanapoingia kufanya shughuli zao mpaka usiku wanapomaliza shughuli zao, Nawaombeni sana mfanye haki katika huu mgao, Block -t specifically maeneo ya chuo kikuu cha teku na sisi pia tunahitaji umeme unaokatwa kila siku kama wanavyouhitaji wakazi wa forest ya zamani ambao nahisi hata hawajui kwamba kuna mgao.

NAWASILISHA
 
Tafadhali tunaomba maelezo zaidi namba ya simu na eneo unalotaka kuweka umeme linanumbali gani kutoka kwenye nguzo
Eneo kutoka kwenye nyumba yenye umeme ni kama mita 250 hadi 300 kwa makadirio kutoka kwangu ila katikat ya huo umbali zimekatiza hizi series za towers mpya zinazosafirisha umeme wenye 400,000 volt sasa kikubwa nachotaka kujua ili nguzo za kawaida zipite chini ha huu umeme wa masafa nini kinahitajika maana naambiwa sijui mpk ifungwe ttansformer hvyo naomba mnihakikishie hilo
 
Yaani kama kuna shirika ambalo wakisema livunjwe hata leo nitashangilia ni Tanesco!

Mtu hata kama umeamua kupumzika na kumalizia weekend nyumbani watakulazisha tu utoke, imagine weekend kama hii unaangalia mpira man utd vs brighton huku unasubiria liverpool vs chelsea jamaa wanakata umeme? Mnasababisha twende bar bila kupenda na vyuma vimekaza!
Kazi mnayoweza tanesco ni kukata umeme tu.

Kwanza nilisikia waziri mpya kasema umeme kukatika ni marufuku...vipi mbona ndio anachochea umeme kukatika?!

Hamna shirika nalichukia kama Tanesco maanake hawapitishi siku bila kuniharibia siku!
 
Huwa wanafanya nini ofisini kama hawawezi kutuletea umeme wa uhakika? Ukiwa ofisini wanakata umeme, ukiwa nyumbani wanakata umeme!
Wanaperuzi internet tuu kusoma umbea

Nguzo yangu ilikua mbovu nimeandika barua 3times holaaa hawajaja

Line yangu ilikua inasumbua daily umeme unakatika nkaandika barua holaaa nkaona isiwe shida nikamtafuta kishoka nkahama line shauri yao
 
Wanaperuzi internet tuu kusoma umbea

Nguzo yangu ilikua mbovu nimeandika barua 3times holaaa hawajaja

Line yangu ilikua inasumbua daily umeme unakatika nkaandika barua holaaa nkaona isiwe shida nikamtafuta kishoka nkahama line shauri yao
Inasikitisha sana. Kitu basic kama umeme kuwa ni luxury!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…