Hivi nguzo za umeme ni shida? Nimeomba kubadilishiwa nguzo ya umeme toka May 2017 leo Dec 2017 naambiwa nguzo hakuna. Iliyopo imeoza nimeripoti kwa meneja Tabata mpaka imekuwa kero nifanyeje?

Na iliyopo ikianguka nini kitatokea kwenye kibanda changu?
 
Arusha umeme ni kero asubuhi unakatika kurudi saa 12 jioni dah hii inchi badala twende mbele tunarudi nyuma
Bora nyie sisi kyela na tukuyu ni kurudi sa tano usiku.... Hapo kuanzia hasubuhi sa moja
 
Hii awamu ni awamu mbaya kuliko awamu zote maana sahivi ni genge la watu wachache ndio wapigaji Deal... Na ndio wanaogopwa nchi nzima... Ni ngumu sana kuwagusa melo kazungumza kitu kimoja cha maana kasema....
 
Naona tayari mshaukata hivi ndio mpaka saa mbili tena kama jana, hivi kwanini lakini kusingekuwa na mashirika mengine ya kutoa huduma hii kama nchi zingine zilivyo, kila siku kutumbua bandarini huku kwenye umeme hakufikiki?

Ndg John Pombe Magufuli si huwa unasoma magazeti na mitandao ya kijamii yasome na haya basi, au fanya ziara huku Kigamboni tukwambie kwa mdomo, tumechoka na hii hali, kama sera yako ni viwanda kwa huu umeme labda viwanda vya kushona nguo kwa mkono tu ndo vitafanikiwa, halafu kazi ya umeme siyo kwamba taa zitumulikie tu na kwamba tunaogopa kulala giza kutuletea usiku peke yake, bali umeme ni kwa ajili ya kazi na biashara, ikiwezekana kateni usiku na mchana kabisa.
 
Jana umekatika asubuhi umerudi majogo leo wameshauchukua yaani kero huwezi fanya shughuli za kukuingizia kipato na bado wanakukadiria kodi kubwa bila kuangalia mapato yanapungua. Hii nchi haiwajali wanyonge
 
Tanesco turudishieni umeme juice zangu zinaanza kuharibika, nitawalisha nn watoto jaman nioneeni huruma. Kivule shule
 
Bagamoyo nako nimeona jana usiku kupitia Clouds tv wananchi wanalalamika biashara zao zinaathirika kutokana na tatizo la umeme.

Sijui Lissu au CHADEMA ndio wanachochea TANESCO wakate umeme?!
 
dah tabu tupu usiku hakulaliki na joto la dar sasaivi balaa umeme unakatwa ovyo ovyo tulitegemea maisha bora ila day to day afadhali ya juzi
 
[QUOTE="Salary Slip, post: 24658611, member: 84376]

Sijui Lissu au CHADEMA ndio wanachochea TANESCO wakate umeme?![/QUOTE]

Kwani Da Mange anasemaje?
 
saa 4 kamili tabata ushakatika. ngoja tuone utarudi saa ngapi? mkurupukaji ni mkurupukaji sana...laiti kama angejua asingetafuta kiki kwa profesa muhongo. yule profesa kweli siyo profesa wa maganda ya korosho.
Hata Arusha wamekata mida hii!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…