Napenda kuwapongeza Tanesco kwa kuwa karibu na wateja wenu,Mie ni mkazi wa Twangoma kijiji cha malela.Tulikuwa na shida sana ya kupata umeme na bahati nzuri mwaka jana kupitia mradi wa REA mlituwekea nguzo za umeme na hatimaye umeme unawaka.Ombi lenu kwenu ni kuwa ule mradi ulitekelezwa nusu kwa maana baadhi ya nyumba ambazo zipo chini karibu na nyumba za NSSF hatukupata huduma hiyo,Ni takribani nguzo kumi na tano mpaka kutufikia,tulijiorganise watu kadhaa tuweze kuvuta umeme lakini tulishindwa kwani tathimini iliyofanywa na mkandarasi gharama nzima ilifika mil 24.hiyo ni pesa nyingi sana kwa watu ambao wapo tayari kuchangia.Tupo tayari kuchangia maendeleo ila tunaomba backup yenu hata nusu ya nguzo nyingine sisi wakazi wa malela tugharamie.Haipendezi kuona upande wa pili kuna umeme na takribani hata nusu km toka umeme ulipo sie hatuna.Tunawakiisha ombi kwenu Tanesco kupitia REA mtusaidie baadhi ya gharama nasi tupo tayari kufanya costsharing.Wenu Mteja.