Kuna watu kila wakinunua umeme wanakatwa 50% kama deni walilokuwa wakidaiwa. Mteja atajuaje kuwa anadaiwa kiasi gani na balance yake ni kiasi gani kwa njia hiyo hiyo anayotumia kununulia umeme??
Anaweza kutupatia namba ya simu na namba ya mita
 
Tumepokea taarifa mpendwa mteja
Tunakujulisha kuwa hakuna utaratibu wa kufanya ulivyodai bali transfoma huzimwa pale ambapo kuna kazi maalumu
Sawa....toeni taarifa sasa, sio mnajiamulia tu zima washa. Watu wamejiajiri wanatumia vifaa vya moto mnawaharibia sana...bora kutoa taarifa mapema watu wajue ili wazime vifaa vyao. Fanyeni kama professional yenu basi
 
Napenda kuwapongeza Tanesco kwa kuwa karibu na wateja wenu,Mie ni mkazi wa Twangoma kijiji cha malela.Tulikuwa na shida sana ya kupata umeme na bahati nzuri mwaka jana kupitia mradi wa REA mlituwekea nguzo za umeme na hatimaye umeme unawaka.Ombi lenu kwenu ni kuwa ule mradi ulitekelezwa nusu kwa maana baadhi ya nyumba ambazo zipo chini karibu na nyumba za NSSF hatukupata huduma hiyo,Ni takribani nguzo kumi na tano mpaka kutufikia,tulijiorganise watu kadhaa tuweze kuvuta umeme lakini tulishindwa kwani tathimini iliyofanywa na mkandarasi gharama nzima ilifika mil 24.hiyo ni pesa nyingi sana kwa watu ambao wapo tayari kuchangia.Tupo tayari kuchangia maendeleo ila tunaomba backup yenu hata nusu ya nguzo nyingine sisi wakazi wa malela tugharamie.Haipendezi kuona upande wa pili kuna umeme na takribani hata nusu km toka umeme ulipo sie hatuna.Tunawakiisha ombi kwenu Tanesco kupitia REA mtusaidie baadhi ya gharama nasi tupo tayari kufanya costsharing.Wenu Mteja.
 
Tunaomba namba yakomya simu mpendwa mteja tutawasiliana na wewe mara baada ya kupata taarifa kamili za eneo lako
 
Ø Namba yangu ya metre ni 37142130279

Ø Matumizi yangu kwa mwezi hayazidi unit 75

Ø Nanunua umeme tsh 292ts kwh

Ø Tofauti na maelezo yenu kuwa mtu anayetumia chini ya unit 75 atanunu umeme kwa bei tofauti na hiyo

Ø NAOMBA MSAADA , AIDHA NAMBA YANGU YA SIMU 0738262024.
 
Tanesco huenda mmefanya vizuri kuweka uzi huu hapa ili kupata maoni ya wananchi kwa Lengo la kuboresha huduma.
Tukizingatia ukongwe wa shirika na upeke wake katika kutoa huduma siamini kama hamjui matatizo mnayoyasababisha kwa wananchi /wateja wenu!!
1.Je!? Mnasuasua na kuringa kwa kuwa hamna mshindani wa kibiashara?
2. Je, Mmeweka uzi huu kinafiki kujifanya mnajali wateja kwa uoga baada ya kusoma alama za nyakati na utawala tulio nao?
Endapo tutapata mshindani bila Shaka mjindae kufa kama mwenzio wa TTCL, nyakati hubadilika endeleni kutuingizia umaskini kwa kuunguza vitu vyetu, unyonge una kikomo, kamwe hauwezi dumu milele.
 
Fika ofisi za eneo lako ujaze fomu mpendwa mteja
 
Habari Jf.
Hawa watoa huduma mhimu wamekosa kazi hadi wameamua kukata umeme muda huu.

Watu tumekaa sebuleni mara paa giza,washeni umeme haraka basi.
 
Sehemu kubwa ya nchi haina umeme tangu saa kumi na mbili jioni huku wahusika wakiwa hawana habari wako Dodoma wakiendekeza mipasho!CCM na serikali yenu tokeni huko Dodoma shughulikieni tatizo la umeme mnaua uchumi was nchi,hivyo vikao mnavyofanya huko vya kusikiliza vijembe vya kina Kafulila na Katambi havina umuhimu wowote kwa Taifa.CCM tuoneeni huruma watanzania.
 
Mara ingine tunajipa kazi zisizo tuhusu !! Umeme toka saa12.... Mpaka saiv bado Kweli ????



Mko busy kuoambana na Upinzani kuliko kufanya mambo ya Msingi
 
Saiv Wanaita Ku Shade line sio Ku kata umeme lakin Maana halisi ni ile ile ya kukata umeme !!


Tanzania ya Viwonder
 
Nimenunua umeme leo tarehe 12/12 /2017
Saa 7;36 pm
Mbaka muda 20:44 sijapata token Voda imethibitisha umetuma imetumwa kwa LUKU 2 ~TANESCO
Kiasi sh 10,000

Mita no 24219180114

Sim 0754 569799
Dar ~bubju
 
Tar...4/12/2017 nilinunua umeme kupitia nmb mobile meter no...07068234553 umeme Wa sh 7000 token sikupata nilijaribu tena kununua mpesa umeme Wa 2000 tuu token nilipata baada ya kupita mda mrefu Leo nikanunua tena kwa kutumia mpesa umeme Wa 5000 nashangaaa napata units 12 wakati awali nilikuwa napata units 41.9 kwa 5000/= ndiyo nauliza kwanini nitolewe kwenye tariff niliyokuwepo ilikhali token za sh elf7 hadi sasa sijazipata na pesa ilikatwa kwenye akaunti?
 
Sasa hii biashara gani
Pesa kwenye akaunt mnakomba
Token amleti au ndio mnatushangisha pesa kinguvu za kubomolea jengo lenu
Leo ninalala giza kwa uzembe wenu mnilipe fidia.
 
Ahsante niliisha ongea na callcentre yenu. Nashukuru maelekezo niliyopata. Kesho ntayafanyia kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…