Je zoezi LA REA kule chanika nyeburu limefika mwisho?
Naombeni kujulishwa tafadhali
 
Kuna tofauti gan ya kununua umeme kat ys mteja wa tarrif 0 na tarrif 1? Nawezaje uhama kutoka tarrif 1 to tarrif 0?

Ni kigezo gan mnatumia kuwagrade wateja wenu katika tarrifs 2 na 0?

NIPENI MAJIBU NINA HASIRA NA NYIE
 
Nawezaje kuwekwa kweny trf 1 mk 75 units
Maana nikinunua umeme 5000 napata unit 14, nina vyumba 6, TV, pas na radio
 
Mkuu lete fundi aangalie earthing yako kama haijakaa njema ni shida. Pia waya ulizotumia ni za kiwanda gani kama ni za kichina tegemea lolote, mwisho yawezekana mita ni mbovu so waje wakague mita kwanza.
 
Mkuu lete fundi aangalie earthing yako kama haijakaa njema ni shida. Pia waya ulizotumia ni za kiwanda gani kama ni za kichina tegemea lolote, mwisho yawezekana mita ni mbovu so waje wakague mita kwanza.
ok nitafanya hivyo
 
nishati ya Uhakika na viwango vya juu ni kichocheo muhimu sana ktk maendeleo ya viwanda.

Hivyo basi Tanesco mnao wajibu mkubwa wa kuboresha miundo mbinu ili kuwa na Umeme Wa uhakika na wenye nguvu.
 
Nimepewa karatasi ya kwenda kulipia bank kwa ajili ya kuunganishwa huu mwezi wa tatu sijaenda kulipa( hali ya maisha imekuwa ngumu), je nitapigwa penati?

Sidhani kama kuna penati kama siyo deni mkuu

Ok nashukuru kwa jibu.
Hakuna penalt yoyote hapo mkuu, ila nivizuri kabla ya kwenda kulipia ukarudi tena katika hizo ofisi kwa maelekezo zaidi, unajua mambo yanabadilika kila siku
 
Kuna tofauti gan ya kununua umeme kat ys mteja wa tarrif 0 na tarrif 1? Nawezaje uhama kutoka tarrif 1 to tarrif 0?
Ni kigezo gan mnatumia kuwagrade wateja wenu katika tarrifs 2 na 0?

NIPENI MAJIBU NINA HASIRA NA NYIE
Hakuna tarrif 0 mkuu, kuna Tarrif One, Two, Three na Four

Tarrif one na four ndio za watumiaji wa kawaida (majumbani) hizo nyingine mbili na tatu ni watumiaji wa viwanda na sehemu zenye mitambo mikubwa kiasi.

Tarrif one ni kwawatumiaji wadogo kabisa wa nishati ya umeme na mara nyingi hawa ni watu wa kijijini ambao huwa hawana matumizi makubwa, japo mijini wapo wasio na matumizi makubwa pia.

Hivyo basi, kama hutumii zaido ya unit 75 kwa mwezi unaweza kuhama tarrif one kwenda tarrif four, chakufanya ni kubalance matumizi yako usizidishe units 75 kwa mwezi ndani ya miezi mitatu, automatically system itakudetect na utabadalishiwa tarrif.

Utajuaje kama umehama tarrif? Ukienda kununua umeme kwa wakala itagoma na unatakiwa kufika office ya Tanesco kupata key change (nambari fulani za kuingiza kwenye meter yako) kisha unaweza kuendelea kutumia tarrif four ila unatakiwa ujichunge sana kwakuwa ukizidisha matumizi unapigwa penalt na utanunua kwa bei kubwa kuliko hata wa tarrif one.
 
Thanks!

Mkuu kwa wateja waliobadilishiwa mita za zamani inakuaje unapotaka kununua umeme kwa mara ya kwanza, wana charge kiasi gani mkuu
 
Thanks!

Mkuu kwa wateja waliobadilishiwa mita za zamani inakuaje unapotaka kununua umeme kwa mara ya kwanza, wana charge kiasi gani mkuu
Kubadilishiwa meter kivipi?

Kuna kubadilishiwa meter kutoka zile za kusoma bill kwenda za LUKU na kuna kubadilishiwa meter za LUKU kama uliyokuwa nayo imepata hitilafu.

Labda ungeeleza nijue situation.
 
Kubadilishiwa meter kivipi?

Kuna kubadilishiwa meter kutoka zile za kusoma bill kwenda za LUKU na kuna kubadilishiwa meter za LUKU kama uliyokuwa nayo imepata hitilafu.

Labda ungeeleza nijue situation.
Kutoka zile za kusoma bill kwenda LUKU mkuu! Asante
 
Jamani Tanesco mbona mnakera sana,Kwasie ambao tuna majengo huku maeneo ya Ilala ambao bili zetu zinaletwaga lakini matokeo yake mpaka leo tarehe 10 mwezi wa 5 bili zetu za mwezi wa 4 bado, kwanini jamani mnatufanyia ivyo hilihali waziri wa nishati alituaminisha yakuwa sasa tanesco ina mitambo ya kisasa ya usomaji wa bili za umeme, nitashangaa sana pindi nitakaposikia mapato yenu yameshuka ilihali hampo kibiashara.

Naombeni tanesco Ilala mbadilike jamani
 
Nimelipia nguzo toka mwezi wa 12 / 2016 hapa Sengerema - mwanza lkn mpaka leo hii hatujafungiwa nguzo eti nguzo zimeisha!!! Mara nyaya Hakuna!!! Je kwa namna hii kweli tutafika?
 
Jangwani feeder inayolisha kituo kipya cha Jangwani ilitoka saa 5 usiku, baada ya patrol tumekuta maeneo ya green acres nguzo ya chuma imegongwa na kupinda na waya kuchomoka na kujivingirisha.

Maeneo yanayokosa umeme ni Hoteli zote zilizopo upande wa packers, Kilongawima, baadhi ya maeneo ya Mbezi ya chini na Africana.Jitihada zinafanyika umeme urudi kwa haraka.
 
Kutoka zile za kusoma bill kwenda LUKU mkuu! Asante
Hizo unaandika barua Tanesco kuomba kubadilishiwa kutoka conventional meter kwenda kwenye meter ya LUKU.

Hii haina gharama, ila tu kama meter ina deni litahamishiwa kwenye meter yako ya LUKU hivyo kila utakapo nunua umeme utakuwa unakatwa percent kadhaa mpaka deni litakapoisha.
 
Mimi nipo Tanga jiji maeneo ya Makorora tatizo langu hii ni Mara ya pili sasa nikiingiza umeme unaingia na kwny remote inaandika good na nikiangalia salio inaonyesha umeme umeingia lakini hauwaki nilijaribu kuwaambia Mara ya kwanza wakasema mita imejilock wakanitumia namba za kuanlock mita na umeme ukawaka, sasa naona imekuwa ni Tabia ya hizi mita kwani hamuwezi kuondoa moja kwa moja tatizo hili maana likitokea najua tuu nitalala kiza siku Tatu au mbili ukiwapigia simu wanasema wanashughulikia
 
Mpendwa Raisi Magufuli.....Tunakuomba kwa heshma na taadhima sisi wananchi wako tuliokuchagua kwa hiyari yetu.....
Tuondolee hili LITANESCO hapa nchini¥^¥

Kwa maana tangu nizaliwe sijawahi kuona Watanzania wakitokwa
na ule ushamba wa kuushangilia umeme SAA 2 YA USIKU
{ everyday } I HATE YOU TNC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…