Jamani Tanesco wenye kuhudumia mbezi louis mbona mnanifanya nilale giza?

Nimekuja hapo ofisini kwenu mbezi mwisho tokea mwezi wa kumi na mbili na mkanipanga 8 January kuwa surveyor atakuja kwangu kwa ajili ya kutathmini gharama za kuingiza umeme hivyo nikae nisubiri kupigiwa simu.

Mpaka tarehe inafika sikumuona huyo surveyor wala kupigiwa simu. tarehe 9th january nikawafungia safari mpaka ofisini kwenu, mkaniambia kuna foleni nisubiri. nikarudi kusubiri baada ya kimya kirefu nikarudi tena.

Yaani kwa ajili ya surveyor tu nimeshakuja hapo ofisini kwenu mara tatu? kupata huduma ya kufanyiwa survey its take more than a month now then tunaongea Tanzania ya Viwanda. Period!

wahusika tunaomba tusaidiwe maana nimechoka kulala kiza mimi na familia yako, huu ni kutokuwajibika vema kwa baadhi ya watu.
 
Baada ya Muhongo kuondoka mgao wa umeme Umerudi tena, why??
 
Namba yako ya simu, jina tafadhali na eneo lako
 
NASHUKURU SANA. LEO NIMEPIGIWA SIMU NA SURVEYOR KASHAFANYA KAZI YAKE. NAWASHUKURU MMNO.
 
TANESCO
Kwa faida ya Wananchi
Itakuwa vyema zaidi ukaijulisha jamii HATUA kwa HATUA ili kuweza kufungiwa umeme wa nyumba.

Assume eneo Lina umeme kwa nyumba za majirani, na Mwananchi anahitaji kufunga umeme kwenye nyumba mpya ya kuishi Familia...

Ahsante.
 




kwa upande wa dharura nawapa pongezi mmeboresha sana, ila huduma zenu bado za kupigana tarehe sana,mita yangu ime expire tangu wiki sasa,umeme unaingia lkn hautoi kuingiza ndani,naenda pale mbezi tanesco waje wabadilishe wanasema ngoja tukuandalie mpaka wiki ijayo ,kweli kitu cha kuchukua tu ofisini unasema ngoja tukuandalie mpaka wiki ijayo? ingekuwa private sidhani kama wangetumia lugha hii,halafu mzee mwenyewe anavyojibu eti nimesema mm kama hutaki nenda popote!!!!!!!!!!
 
MFUMO WA KUTUPATIA TAARIFA/LALAMIKO

1.JINA................................

2.SIMU...............................

3.MKOA.............................

4.WILAYA..........................

5.MTAA/KIJIJI/KATA.........

6.JINSI YA KUFIKA................

7.KITU/ALAMA/MTU MAARUFU.............................

8.NAMBA YA MITA................

9.TATIZO LAKO/UNACHOHITAJI....................

10.NAMBA YA TAARIFA ULIYOPEWA.................

*Zingatia*
-kama ni manunuzi ya umeme onyesha mtandao na ujumbe unauopata ukinunuaumeme

-Kama ni kushindwa kuingiza umeme onyesha unachokiona kwenye mita yako unapoweka umeme

-Kama umeshatoa taarifa ofisi yeyote onyesha namba ya taarifa uliyopewa


"TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO"
 



Wameshakuja wa dharura wakasema mita hii muda wake umeisha unatakiwa ubadilishiwe mita...kwenda mbezi ndio wakajibu hivyoo,narudia tena kuwapongeza wa dharura
 
Wameshakuja wa dharura wakasema mita hii muda wake umeisha unatakiwa ubadilishiwe mita...kwenda mbezi ndio wakajibu hivyoo,narudia tena kuwapongeza wa dharura
Tunaomba taarifa hizo mkuu tuzifanyie kazi
 
 
naomba kujua hii mita na 24213512213 iko kwenye tariff ngapi na matumizi yake ni Tariff ipi???
Natanguliza shukrani
 
Tanesco ni wiki sasa hapa Dar mnakata umeme aidha asubuhi mpaka jioni au mnakata ikifika saa moja usiku mpaka saa sita usiku.

Kama kuna mgao wa umeme basi toeni taarifa wanainchi tujue ili tujiandae na huo mgao kwa kuweka bajeti ya mafuta ya majenereta yetu.
 
Wanaboa mpaka basi,waseme tu ukweli shirika ni letu wenyewe ya nini kufichana?shirika la umma lafaa kuwa wazi zaidi hasa mipango na utekelezaji wake kwa umma.Sasa wao yakuficha wanaweka wazi na yakuweka wazi wanaficha.
 
Dah kumbe mpaka huko Tanzania iliko nanyi ni kama sisi huku wa mchoteka,likweso,nalasi,mbesa na mkandu,,kodi zetu zinabomolea jengo lile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…