Amalinze
JF-Expert Member
- May 6, 2012
- 6,780
- 5,305
Hawa TANESCO wazushi tu,issue serious hawajibu kabisa,wanazipita kama hawaoni, wanawajibu wale walionunua luku kwa simu bila kupata tokens tu hili tuone wanafanya Kazi ukiwauliza issue global hawajibu zaidi ya kukuambia tuma Jina,namba ya simu na bla bla kibao,wewe ushaambiwa mf TEMEKE nzima hakuna umeme sasa namba ya simu ya nini? Si ilitakiwa wapige SUBSTATION ya temeke kuconfirm?Mbona Wengine Hatujibiwi
TANESCO tuliomba umeme toka mwaka 2016 January wakazi wa SACCOS Mabwepande karibu na Chuo cha kilimo, Nguzo zilipo mpaka SACCOS hazizidi 7 lakini mpaka Leo hakuna kitu,nilifika ofisi za Tegeta mkasema mshaleta Nguzo 200 mshamkabidhi contractor na mchoro tayari, hilo jibu ni la mwaka Jana October,cha kushangaza mpaka Leo hakuna cha Nguzo wala contractor.
TANESCO mnafanya hivyo kwa sababu mpo peke yenu kwenye game la kusupply umeme lakini ipo siku mtakufa natural death...Alternative ni Solar ila figisufigisu kodi Kubwa hivyo kupelekea Gharama ya vifaa iwe Kubwa otherwise hakuna angehangaika na nyinyi kabisa.
Usije kuniambia nikupe namba sijui jina sina mda huo tena maana nilishakupa tangia mwaka jana mwezi wa 9,nimeandika tu kuwapa black and white, huo umeme wenu leteni mtapojisikia hata 2030 poa tutakaa giza tu,kila sehemu madudu tu,Watanzania wanakatwa fedha kuchangia REA kwa ajili ya kuwahudumia watanzania wenzao ,Nguzo 7 mpaka kwenye makazi ya SACCOS miaka miwili bado hamjapata fedha??? Really? Like seriously? Na unajisikia comfortable kabisa unaamka asubuhi unaenda kazini?? Upinzani/Wanaharakati ni mda muhafaka wa kupinga monopoly ya TANESCO maana Kazi imewashinda.