Kuna nguzo ziliangushwa na upepo mkuu wataalamuw wetu wanafanyia kazi
 
Hii ni kweli tupu. Hadi sasa saa11 alfajiri,Umeme haujarudi.
 
Ni utaratibu mzuri kutoa taarifa tatizo linapotokea ili wateja wajue namna ya kukabiliana na changamoto hiyo.

Hii ni Mara ya tatu napost juu ya tatizo lililopo Kijiji cha Mkata wilaya ya Mvomero mkoa wa morogoro tranfoma haifanyikazi wiki sasa na hakuna hatua wala taarifa zozote kwa watumiaji umeme unaopozwa na transfoma hii.Hii ni haki kweli?
 
Tunaomba namba yako ya simu
 
tafadhali naomba token zangu nimeshatuma taarifa mara mbili
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUREJEA KWA UMEME KATIKA MIKOA ILIYOUNGWA KATIKA GRID YA TAIFA

Tunawataarifu Wateja wetu na Wananchi kwa ujumla kuwa, baadhi ya Mikoa iliyounganishwa na Gridi ya Taifa imeanza kupata huduma ya umeme .

Mikoa iliyo kwisha pata umeme ni pamoja na Iringa , Mbeya ,Dodoma, Morogoro Pamoja na Baadhi ya Maeneo ya Mkoa wa Dar es Salam.

Mafundi na Wataalamu wa Shirika bado wako kazini Kuhakikisha kuwa Huduma ya Umeme inarejea mapema kadri iwezekanavyo.


Tutaendelea kutoa taarifa zaidi.

Uongozi wa Shirika unaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza.

Tafadhali usishike wa kukanyaga waya ulioanguka au uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo:

Kwa mawasiliano

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetu

IMETOLEWA NA:

OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU

MACHI 10, 2018
 
Tatizo LA kukatika katika Kwa umeme imekua kero Kwa nini wakati tunalipa kodi lukuki nazungumzia Kibaha mjini hadi Kwa mathiasi kila dakika umekatika Kwa nini mnafanya nini Sasa haya ndio maendeleo , mnakera mnon mno na cha ajabu tuliambiwa kuna gesi lakini hatuoni faida yake upuuzi mtupu
 
Tanesco tumewachoka .umeme unakatika kila Mara mnafanya nini kama hamuwezi kazi waitwe wageni nje ya tanzani watufanyie kazi mnabore mno mnooo
 
Halafu ndo tunapewa takwimu za kijinga eti nchi inasonga mbele yani aibu kila baada ya nusu SAA umekatika upumbavu
 
Wazee wa maandamano hamkosi sababu daah. Nasubiri mkipelekwa kisutu mkiwa mnachechemea huku waandishi wanawananga na mikamera yao.
 
Washafanya yao ubungo external yote ...


Jana usiku tena walikata hawa watu kipind cha mvua huwa bora sana kwao ....mana wanapata visingizio sasa sasa hiv kweli muda huu ni wa kukata umeme bila taarifa?
 
Sio huko tu jaman hapa Lindi ni Shiiidaaa ndani ya nusu Saa wameshakata na kurudisha mara nne
 
Wazee wa maandamano hamkosi sababu daah. Nasubiri mkipelekwa kisutu mkiwa mnachechemea huku waandishi wanawananga na mikamera yao.

Mimi nataka nione watu 4milioni wanadhibitiwa na jeshi la Askari laki tatu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…