Huku Arusha napo ni shida, yani wanakata mara kwa mara. hapa wameurudisha dakika 40 zilizopita. Hili jambo la kukata bila taarifa siyo zuri hata kidogo.
Mfano mimi laptop yangu imekufa betri yani kila wakikata nayo inazima, wananirudisha nyuma katika kazi zangu🙁. ishu ya nishati ya uhakika ni ya muhimu sana kwa nyakati hizi!! HALAFU HUWA NAJIULIZA ILE GESI YA MTWARA ILIISHIA WAPI? MAANA TULIHAKIKISHIWA UMEME WA UHAKIKA KIPINDI KILE, AU BADO WANAICHIMBA!!! Pengine wenzetu wa Dar mtakuwa mnajua ilipofikia maana si mbali na Ntwara!!!