TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Kabisa kabisa
Hii kiu ya viwanda aliyonayo Mh Rais, haiweze kukatwa na kiwango cha umeme tulionao. Nipo huku Kibamba yaani hali ya ukatikaji wa umeme ni ya hali ya juu sana. Ndani ya masaa 24 yaliyopita Nafikiri ni masaa 3 tu ndo yalikuwa na umeme mengine ni hola.
Kiwanda gani kitahimili na kuweza kujiendesha kibiashara.
Embu TANESCO toeni mkono wa shirika kwa Mh Rais ili njozi ya viwanda iwezekane.
 
Habari, WanaJF Leo ni siku Ya 3 Kimara Mwisho njia ya Kwenda Bunyokwa, Matonya! Hakuna Umeme!

Haieleweki Tatizo kubwa nini Maana hata Habari Hatujapewa! Tunashindwa Kufanya Kazi Kwa Muda Mkubwa Mno! Tanesco wameangazia sana

Kuhudumia Mijini Ila Humu Ndani ndani wanafanya kazi wakijisikia! Kama Nyie Tanesco Mnaona Hamuwezi Kuhudumia maeneo yaliyojificha si Mje mnyofoe manguzo yenu Tujue Moja, Tutumie Solar Tu! Maisha gani Haya!
Tunaomba Rais Magufuli

Uwatumbuetumbue Tanesco Maana naona Wameshaizoea Kazi wanafanya wanavyojisikia.[emoji34]
 
Habari Wakuu

Leo ni siku ya tatu toka umeme ulipokatika huku kwetu na haujarudi tena

Nmeshapiga sana simu makao makuu lakini line yao iko busy muda wote. Nimejaribu pia kupiga Tawi lao la kimara simu either haipokelewi au iko busy (pengine wengine wanapiga bila mafanikio)
0768 985 100 Tanesco makao makuu
0717 379 696 Tanesco kimara

Si mara ya kwanza hii kitu kutokea, miezi kadhaa iliyopita kulikuwa na tatizo kama hili ulikuja umeme mkubwa ukaunguza vitu.. na ni eneo hilihili

Kama kuna namna yoyote ya hawa jamaa kupata huu ujumbe naomba uwafikie.

Nawasilisha
 
Pole sana ndugu,najaribu kuvuta kumbukumbu ya maneno ya mawaziri wa nishati naona kauli zao zilikuwa za kisiasa sana,Umuhimu wa gesi tuliyoambiwa sijauona kabisa
 
Sijui kama Tanesco bado mko humu ? Kama mpo naomba kuuliza. Kwa wilaya ya Kibaha mtu akishalipia connection fees. Hua anaungiwa umeme baada ya siku ngapi
 
Aisee nyie jamaa siku mbili nzima hamna umeme ni halali kweli?!
 
Habari Wakuu

Leo ni siku ya tatu toka umeme ulipokatika huku kwetu na haujarudi tena

Nmeshapiga sana simu makao makuu lakini line yao iko busy muda wote. Nimejaribu pia kupiga Tawi lao la kimara simu either haipokelewi au iko busy (pengine wengine wanapiga bila mafanikio)
0768 985 100 Tanesco makao makuu
0717 379 696 Tanesco kimara

Si mara ya kwanza hii kitu kutokea, miezi kadhaa iliyopita kulikuwa na tatizo kama hili ulikuja umeme mkubwa ukaunguza vitu.. na ni eneo hilihili

Kama kuna namna yoyote ya hawa jamaa kupata huu ujumbe naomba uwafikie.

Nawasilisha
Bora umesema mkuu hasara niliyopata siyo mchezo
 
Kuna Tatzo la umeme hawezi kuwasha fridge Wala microwave nimetoa tarifa a mkoa wa kinondoni ni Kapewa kumbukumbu no Hadi Leo cjawaona, yatakiwa nifanyaje
 
Back
Top Bottom