TANESCO

Hii meter/ remote ya ndani inanisumbua sana kuweka umeme.

Uliisha kabisa nimenunua lakini kila nikijaribu kuweka inakataa.
Inaweka 30.
Nifanye nini umeme uingie?
Leo ni siku ya nne niko gizani.
 
Tanesco kahama cjui mna nn, kuna nguzo imelipiwa toka mwez wa kwanza hapa kagongwa,

Nguzo imekuja kuwekwa mwezi wa tatu mwanzon, baada ya hapo mka kaa kimya kama hamjui kuwa kuna watu wanashida na umeme...

Mbaya zaidi Wale surveyors wanapita kila jmoc, lakin Wale wanaohusika na kuweka umeme mmekaa kimya utadhan maji mtungini.

Jirekebishen haiwezekan watu wasubiri umeme utadhan hawajalipia ilihali kila kitu tayari.

Au kuna issue nyingne extraordinary inahitajika ili hiyo service ifanyike?????

Majibu tafadhali.
 
Siyo fair mnakata umeme tangu asubuhi had saa 4 usiku.... Mambo yetu, biashara zet zote znakwama !
 
Kwann mnawekea watu nguzo za umeme lakin kuja kiwawekea umeme iwe ni story isiyo isha???

Au tanesco nayo inaendeshwa kwa siasa nn....

Kagongwa mmechomeka nguzo tiuiuuuuuu mkasepa

Daaah mnaboa Sana.
 
Ndugu mpendwa mteja
Tunaomba taarifa kamili ya eneo gani? Namba yako ya simu tafadhali
 
Kwann mnawekea watu nguzo za umeme lakin kuja kiwawekea umeme iwe ni story isiyo isha???

Au tanesco nayo inaendeshwa kwa siasa nn....

Kagongwa mmechomeka nguzo tiuiuuuuuu mkasepa

Daaah mnaboa Sana.
Ndugu mpendwa mtejaTunaomba taarifa kamili ya eneo gani? Namba yako ya simu tafadhali
 
Siyo fair mnakata umeme tangu asubuhi had saa 4 usiku.... Mambo yetu, biashara zet zote znakwama !
TUPATIE TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA.

NDUGU WAPENDWA WATEJA WETU MNAOTOA TAARIFA KUPITIA MITANDAO YETU YA KIJAMII TUNAWAOMBA MZINGATIE YAFUATAYO ILI KURAHISISHA UFAFANUZI NA UFUMBUZI WA TATIZO AU TAARIFA HUSIKA

1.ENEO HUSIKA

(Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti)

2.NAMBA YA SIMU

(Wakati mwingine umeme upo kote isipokuwa kwako hivyo na rahisi kuwasiliana na wewe)

3.KARIBU NA NINI

(Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk)

4.JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO

(Toa ufafanuzi wa jinsi ya kufika makazi yako,chukulia unamuelekeza mtu ambaya hajawahi kufika kabisa)

5.MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI

(Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.)

6.KAMA NI TATIZO LA MITA NINI KINATOKEA UKIWEKA UMEME

(Kila mita ina ujumbe wake unaoashiria kitu fulani hivyo kubainisha ujumbe kunamsaidia mpokea taarifa kukupatia maelezo sahihi mfano mita namba 24339173921 inaonyesha error 77)

7.KAMA NI KUSHINDWA KUNUNUNUA UMEME UNAPATA UJUMBE GANI NA UNANUNUA KWA NJIA GANI

(Ujumbe huu ni muhimu sana kuweza kubaini chanzo cha tatizo pamoja na njia iliyotumika kununulia umeme mfamo Mpesa, Tigopesa, Maxcom nk)


TUNAENDELEA KUWASIHII WATEJA WETU KUZINGATIA UTOAJI WA TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA ZAIDI KUTOKA TANESCO.

ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA KUTOKA TANESCO
 
Ndugu mpendwa mteja
Tunaomba jina ukilolipia au namba yako ya form au namba ya simu
 
TANESCO

Hii meter/ remote ya ndani inanisumbua sana kuweka umeme.

Uliisha kabisa nimenunua lakini kila nikijaribu kuweka inakataa.
Inaweka 30.
Nifanye nini umeme uingie?
Leo ni siku ya nne niko gizani.
Ukiingiza umeme inaandika nini?namba yako ya simu tafadhali
 
Nililipia kuungañishiwa umeme tarehe 19/4 na sijaambiwa kitu chochote,,,nini tatizo?nililipia na nguzo
 
Jamani tanesco huku salasala kwa mrope umeme ni mdogo cna wakati mwingine hata radio ina shindwa kuongea yaan makelele ya IPTL mtupigie sisi na bado umeme mtupunje liangalie upya hili eneo mnatutesa cna
 
mimi ni mkazi wa kigamboni, nmelipia umememn toka tr 11 mwez wa kwanza mwaka huu 2017 lakin mpka sasa nnaishi gizani? hivi kwann mnatufanyia hivi jaman? ukienda unaambiwa nguzo hakuna wakat ukienda yombo pale yunakuta minguza zaid ya eflu imelalal tu usku kucha.
 
TANESCO TAFADHALI NAOMBA MNISAIDIE NATUMIA UMEME UNIT NDOGO SANA KWA MWEZI HATA 65 HAZIFIKI KWA MWEZI LAKINI NAONA BEI YA MANUNUZI WA UMEME BADO NI YA WATUMIAJI WAKUBWA MLISEMA HUA INABADILIKA AUTOMATICALLY HAMNA KITU. METER NO. NI 24217491554
 
Tanesco mmenikera kiukweli, mmenifungia luku mwez wa 11 mpka leo hamtaki kunitoa kwenye tariff. Miezi mitatu ya maangalizi imepita, nmeandika barua toka mwez wa tatu ili nitolewe ila hamjanitoa.

Naombeni mnitoe kwenye tariff, vigezo nmeshatimiz shida ni nn?. Mi. Nko monduli.... Meneja tawi la. Monduli tutatulie hili tatizo.

Afu yule dada maulizo ananyodo sana monduli
 
Reactions: ADK
Unit hazipunguzwi bali huhamishwa kutoka mita moja kwenda nyingine mwa maombi kutoka kwa mteja na yawe kwa maandishi
TANESCO mtupe maelezo kidogo huku kijichi kwanini kila siku ya Mungu umeme lazima ukatike?

Shida huwa ni nini at least tupate maelezo tujiandae kisaikolojia kma ni matengenezo yasiyoaisha au mitambo imechoka maana its too much mtusaidie jamani
 
Habari zenu wakuu wa jf,mie ni fundi mzuri tu wa Umeme wa Majumbani,nafanya wiring katika nyumba na pia narekebisha hitilafu za kiumeme ndani ya nyumba,na pia natoa ushauri bure wa maswala ya kiumeme.

Aliye tayari ani Pm,napatikana ilala ila maeneo ya dar nafika kote
 
Habari zenu wakuu. Tatizo ni kukatikatika kwa umeme huku sengerema mkoani mwanza. Hili tatizo limedumu kwa muda mrefu sana.

Shida ni nn? Kwa nn tatizo hili lisirekebishwe sababu ni tatizo ni la muda mrefu. Nawasilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…