*SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)*
*TAARIFA YA KUOMBA RADHI WATEJA WETU WA MKOA WA TEMEKE*
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi Wateja wake wa maeneo ya Chang'ombe, Keko, Nyerere Road, Quality Plaza, Viwanda Base, Uniliver, Bakhresa, Jamana, MSD na maeneo jirani kwa katizo la umeme lililotokea leo Aprili 11, 2018.
*SABABU * Ni kutokea kwa hitilafu katika waya unaopitisha umeme wa msongo wa kilovolti 33 unaopeleka umeme katika kituo cha kupokea na kupoza cha TOL na kusababisha Wateja wanaopata huduma kutoka kituo hicho kukosa umeme.
Wataalamu wetu na mafundi wanaendelea na kazi ya kurejesha umeme katika hali yake ya kawaida kwa haraka.
Tutaendelea kutoa taarifa zaidi ya kazi
TANESCO inaomba radhi kwa usumbufu umaojitokeza
Kwa mawasiliano
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100
Tovuti:
www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:
Mitandao ya kijamii
Twitter,
www.twitter.com/tanescoyetu,
Facebook
Tanesco Yetu
IMETOLEWA NA:
OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU
APRILI 11, 2018