TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Mkuu me naona mbezi kuna tatizo kubwa sio bure maana me nawapigia simu wk sasa kila siku naambiwa mafundi wanakuja inaingia wk ya pili sasa kwangu nipo kwenye giza
 
Jamani wanajamvi hebu niambieni, kuna mtu yeyote ambaye tatizo lake limetatuliwa kwa kuandika kwenye thread hii ? Nimeandika kuhusu TANESCO Mbezi, badala ya kufuatilia limefutwa, je TANESCO wanufurahia uzembe wa ofisi yao ya Mbezi ? Wanataka Raisi atatue matatizo mangapi ? Kama mnataka kila kitu kiende kwa Raisi sawa ila msitulilie baadaye.
Ndugu mpendwa mteja kwa mteja anayetoa taarifa kamili anapata huduma mapema iwezekanavyo
 
Ndugu, Huku Geita tunaambiwa mita za three phase hazipo, tumefanya malipo tokea mwezi February, hadi sasa hakuna huduma tuliyo patiwa, tunaomba Msaada, mtufikishie taatifa hizi Kwa wanaohusika ili tuletewe huduma.
Umelipa lini kwa jina gani na namba Yako ya simu
 
Tanesco nauliza nikitaka nibadilishe luku yangu kwenda taarif four mchakato wako upoje..je ni bure?
 
Tanesco nauliza nikitaka nibadilishe luku yangu kwenda taarif four mchakato wako upoje..je ni bure?
Uwe na matumizi yasiyozidi unit 75 kwa mwezi na unajaza fomu ofisi ya eneo lako kisha kama umekidhi vigezo unabadilishiwa bure
 
Ndugu mpemdwa mteja hatuuzi mita bali kuna gharama za kuunganishiwa umeme, chukua fomu tukupimie na kukupatia makadirio
Hii hoja yangu mbona haijajibiwa??
Yani nimelipia nguzo mbili toka mwaka jana lakini mpaka sasa kila nikiuliza naambiwa hakuna vifaa.. Huu sio uungwana kwa kweli mnatuumiza sana. Hela zenyewe tunazitafuta kwa shida tunawapa alafu tunaanza kuzungushw hivi.
 
Tanesco,
Habari zenu
Nahitaji kuwa wakala wa tanesco wa kuuza token za luku toka kwenu moja kwa moja.
Nipeni hapa mchanganuo mzima na namba za simu ili niwasiliane na ninyi moja kwa moja naombeni hapa vitu vinavyotakiwa n.k...
Asanteni.
N.B nipo eneo ambalo token za luku Za muhimu sanaa na baadhi ya watu wanapata shida.
 
Tunaomba TANESCO. muweke utaratibu wa mikataba na masharti ya mikataba haiwezekani kila siku mlete hasara alafu tunaendelea kuchekeana.

Fanyeni utaratibu kuwepo na mikataba.

Mtakapo leta hasara mlipe mara moja.
 
Ndugu mpendwa mteja kwa mteja anayetoa taarifa kamili anapata huduma mapema iwezekanavyo

Kwa nini tatizo lisishughulikiwe kwa ujumla wake wakati linawahusu watu wengi. Kwa nini mteja kwa mteja. Mbezi hawataki kwenda kufanya survey wakati watu wameshalipa ? Kisa hawana usafiri. Watu wako tayari kutumia usafiri binafsi hata kwa kuchanga, wanasema hairuhusiwi. Fungeni ofisi basi tujue hakuna huduma.
 
Tunaomba TANESCO. muweke utaratibu wa mikataba na masharti ya mikataba haiwezekani kila siku mlete hasara alafu tunaendelea kuchekeana.

Fanyeni utaratibu kuwepo na mikataba.

Mtakapo leta hasara mlipe mara moja.
Hahahaha mkuu umechoka na hasara za shirika letu.
Nafkr kwa utaratibu wa mfumo mpya wa malipo huu waloweka angalau mambo yatakwenda vizuri sanaaaaa.
Tuvute subra tutafika.
 
Kwa nini tatizo lisishughulikiwe kwa ujumla wake wakati linawahusu watu wengi. Kwa nini mteja kwa mteja. Mbezi hawataki kwenda kufanya survey wakati watu wameshalipa ? Kisa hawana usafiri. Watu wako tayari kutumia usafiri binafsi hata kwa kuchanga, wanasema hairuhusiwi. Fungeni ofisi basi tujue hakuna huduma.
Wateja wetu wato watafanyiwa vipimo kama mkataba wa huduma kwa wateja unavyotaka, tunawaomba radhi sana
 
Thread namba 4057 hamjanijibu
Mimi ni mpangaji wa muda mrefu hapa kwenye hii nyumba... Nilikuta nyumba haina umeme na mwaka 2004 niliweka umeme... Sasa miaka hii ya karibuni ilivyokuja kuenea luku nimepewa mita ya luku ambayo kila nikinunua umeme nakatwa asilimia Fulani ya deni la zamani Sasa nimejenga nyumba yangu.. Nataka kuhamia bado sijaweka umeme.. Na siwezi kumwachia mwenye nyumba deni hilo.. Je naweza kuhamisha deni kutoka mita ya mama mwenyenyumba na kulihamishia kwenye mita yangu????

Kwa swala hili leta barua kwa mahandishi huku ukiwa na ridhaa ya mwenye nyumba kutekeleza hayo
 
Tanesco,
Habari zenu
Nahitaji kuwa wakala wa tanesco wa kuuza token za luku toka kwenu moja kwa moja.
Nipeni hapa mchanganuo mzima na namba za simu ili niwasiliane na ninyi moja kwa moja naombeni hapa vitu vinavyotakiwa n.k...
Asanteni.
N.B nipo eneo ambalo token za luku Za muhimu sanaa na baadhi ya watu wanapata shida.
Tanesco naombeni mnipe majibu ya hili ombi langu.
 
TANESCO Nina kiwanda changu kidogo, kwa mujibu wa Wanasiasa kiwanda kidogo hata saluni ni kiwanda, sasa Nimenunua Mashine Za Kusaga na kukoboa mahindi ili niuze unga, kwa bahati mbaya nilijaza Maombi ya umeme wa REA, Wakafika mafundi wa REA nikawa sijamaliza baadhi ya mambo, siku ambayo naenda kulipia, nikaambiwa siwezi kulipia tena kwakua REA imeshaisha hadi awamu nyingine, nikaomba niwekewe umeme ambao hauko chini ya REA ili uzalishaji uanze, jamaa wamegoma hadi Leo. Kwahio shughuli zangu zimesimama. Je? Ni lini hio REA itaanza ili "kiwanda" changu kianze kazi? Je Kwanini siruhusiwi kufungiwa umeme wa kawaida kisa tu nimejaza form za REA?? Eneo ni mkoa wa Pwani
 
TENESCO KUNA SHIDA GANI TEMEKE?
NDO NIMERUD SAIVI SIMU YANGU INA 5% HAKUNA UMEME, NATAKA KUANGALIA MPIRA...mnarudisha naa ngapi?
 
TENESCO KUNA SHIDA GANI TEMEKE?
NDO NIMERUD SAIVI SIMU YANGU INA 5% HAKUNA UMEME, NATAKA KUANGALIA MPIRA...mnarudisha naa ngapi?
*SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)*

*TAARIFA YA KUOMBA RADHI WATEJA WETU WA MKOA WA TEMEKE*

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi Wateja wake wa maeneo ya Chang'ombe, Keko, Nyerere Road, Quality Plaza, Viwanda Base, Uniliver, Bakhresa, Jamana, MSD na maeneo jirani kwa katizo la umeme lililotokea leo Aprili 11, 2018.

*SABABU * Ni kutokea kwa hitilafu katika waya unaopitisha umeme wa msongo wa kilovolti 33 unaopeleka umeme katika kituo cha kupokea na kupoza cha TOL na kusababisha Wateja wanaopata huduma kutoka kituo hicho kukosa umeme.

Wataalamu wetu na mafundi wanaendelea na kazi ya kurejesha umeme katika hali yake ya kawaida kwa haraka.

Tutaendelea kutoa taarifa zaidi ya kazi

TANESCO inaomba radhi kwa usumbufu umaojitokeza

Kwa mawasiliano

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:

Mitandao ya kijamii

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook Tanesco Yetu

IMETOLEWA NA:

OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU

APRILI 11, 2018
 
Back
Top Bottom