Kama mradi ulipita muda wake unapaswa kulipia kwa bei ya kawaida
 
Kama mradi ulipita muda wake unapaswa kulipia kwa bei ya kawaida
Mwambieni basi huyu Manager wa Wilaya moja huko Pwani. Nimeshapoteza muda saana, naimbiwa mapambio tu ya kusubiri awamu nyingine ya REA. Jibu lako ni zuri ila halina msaada Kama Manager wa Pwani hawatakua na Hii information. Tafadhali wajulisheni
 
Mwambieni basi huyu Manager wa Wilaya moja huko Pwani. Nimeshapoteza muda saana, naimbiwa mapambio tu ya kusubiri awamu nyingine ya REA. Jibu lako ni zuri ila halina msaada Kama Manager wa Pwani hawatakua na Hii information. Tafadhali wajulisheni
Tunaomba taarifa zifuatazo
Jina
Simu
Eneo
Tufatilie
 
Kwani na UBUNGO RIVERSIDE, KIBANGU NA VIUNGA VYAKE NAYO IKO NDANI YA MKOA WA TEMEKE AU NDO TUELEWE NINI?

Au mna wanafunzi wa field katika kipindi hiki mnawafundisha jinsi ya kuzima na kuwasha?
Mnakera sana haiwezekani umeme unakatika nusu saa unarudi tena dakika 10 unakatika tena saa nzima unarudi dakika 15 unakatika tena lisaa limoja na nusu unarudi tena dakika 5. Hii zima washa zima washa mnatutaka nini?
Kama kuna shida si bora mzime mazima mrekebishe likisha kamilika ndo muwashe mazima?
Au mnataka kututia hasara ya vyombo vyetu vya umeme??

TUTALALA NA NYINYI MBELE VYOMBO VYETU VIKIUNGUA NA HII TABIA YENU.

Toeni tangazo kama kuna shida ilitujiandae kwa kuchaji simu zetu za tochi!

Kingine cha mwisho!
SISI UBINGO UMEME HAUTAKIWI KUKATIKA HATA SEKUNDE MOJA KWA SABABU SISI NDO WAHANGA WA MAKELELE YA MITAMBO YENU. RUDISHENI FADHIRA KWA KUTOKUKATA UMEME UBUNGO!
 
Mita ya kwanza nililipa 15/02/2018,nyingine 10/03/2018,nikaahidiwa mita zote baada ya 2 week zitakuwa tayali, Sasa kila ninapowakumbusha wanasema mita nitatizo la taifa, mawasiliano ni 0713148453. nitashukuru endapo nitapatiwa utatuz wa issue hii.
Ni wilaya na mkoa gani
 
MNACHOSHA SANA, KILA MARA MPAKA NIWAAMBIE? HAMUWEZI KUSEMA BILA KULALAMIKIWA? JIPANGENI SANA
 
Tanesco mbona hamjibu ujumbe wangu???

Naanza kupata hasira sasa kama hakuna majibu ya moja kwa moja simseme????
 
Kuwa wakala ni mpaka tenda itangazwe na uwe na mtaji kuanzia 5000,000 kisha aombe na ushindanishwe ukishinda unapewa kazi hiyo
 
Kuwa wakala ni mpaka tenda itangazwe na uwe na mtaji kuanzia 5000,000 kisha aombe na ushindanishwe ukishinda unapewa kazi hiyo
Hapo ulivyoandika ni laki 5 au milion tano???
Sijaelewa vizuri.
 
*SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)*

*TAARIFA KWA WATEJA WETU WALIOUNGANISHWA KWENYE GRIDI YA TAIFA*

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake waliounganishwa na gridi ya Taifa kuwa, leo Aprili 12, 2018 majira ya saa 7:16 Mchana imetokea hitilafu katika mfumo wetu wa gridi.

Wataalamu wetu wanaendelea na jitihada za kuhakikisha umeme unarejea kwa haraka.

Tutaendelea kutoa taarifa zaidi.

Tafadhali Usishike, wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote unaojitokeza.

Kwa mawasiliano

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:

Mitandao ya kijamii

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook Tanesco Yetu

IMETOLEWA NA:

OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU

APRILI 12, 2018
 
*SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)*

*MAENDELEO YA UREJESHAJI UMEME WA GRIDI*

Wataalamu wetu bado wanaendelea na jitihada za kuhakikisha umeme unarejea kwa haraka, kwa hivi sasa umeme umerejea Mikoa ya Dodoma, Tanga pamoja na Wilaya ya Chalinze.

Tutaendelea kutoa taarifa zaidi.

Tafadhali usisogelee, usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote unaojitokeza.

Kwa mawasiliano

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:

Mitandao ya kijamii

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook Tanesco Yetu

IMETOLEWA NA:

OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU

APRILI 12, 2018
 
nyaya nzuri za kufanyia wiring ni aina gani? maana mnaweza mkanielekeza aina ili nikiingia dukani kununua rolu nami niwe na ufahamuu
 
Asanteni sanaaaa kwa Taarifa lakini ujumbe huu ulichelewa kutufikia.
Mmeuandika na Tatizo tayari lishatokea muda mrefu kidogo.
 
nyaya nzuri za kufanyia wiring ni aina gani? maana mnaweza mkanielekeza aina ili nikiingia dukani kununua rolu nami niwe na ufahamuu
Mkuu nyaya zipo nyingi ila ni bora zaidi ukawa karibu na fundi umeme huyo anayetaka akufanyie wiring ndo itakuwa vizuri.
Nunua nyaya zilizothibitishwa na Tbs...
 
Ni miezi mi nne sasa toka nilipie service line hapa nyakato mwanza, ila kila nikiuliza naambiwa nguzo hakuna wakati nilishasikia mtu akilipia nguzo anatakiwa awe amefungiwa umeme ndani ya wiki moja? embu mniweke sawa kuhusu hilo wanaojua[emoji41] kama haiwezekani mnirudishie hela yangu nikanunue solar
 
Mkuu bado wanafanya ukaguzi wa wafanyakazi wasio na vyeti wakimaliza ndo wanakuja kufunga umeme
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…