NAMBA ZA MADAWATI YA DHARURA -TANESCO DAR ES SALAAMJina.sylivanus msanje
Simu.0717599264
Mkoa.dar es salaam
Wilaya.ubungo
Mtaa.Malamba mawili mpakani
Kitu,Bar kwa tesha
Mita no.54172211200
Toka Jana mita imekata umeme umeme auingii ndani lkn pale kwenye mita upo sina namba za imejens mtanisaidiaje.
Tafadhali fika ofisini tukusikilize na kukuelewesha vizuriMimi ni mteja wenu wa Arusha tarehe mwenye Luku 37142673112 wiki iliyopita nimenunua umeme wa elfu ishirini na kukatwa elfu kumi eti nina deni. Nilipouliza nikajibiwa kuwa ninakatwa deni nililokuwa nadaiwa kabla ya kufungiwa luku. Sikubaliani na deni hilo kwani kabla ya kuwekewa luku TANESCO walihakiki akaunti yangu na sikuwa na deni lolote ndipo nikafungiwa luku. Nashangaa deni limetoka wapi? Nahitaji maelezo kuhusiana na deni hilo la kiasi cha T.sh. 155,000 kwani luku niliwekea tangu mwaka 2013 leo ndo wanakuja kukata fedha zangu eti ninadaiwa hii siyo haki tafadhali shughulikieni suala hili.
Duuuuuuuuuh polen sanaaaaaJamani kimara mavurunza toka jana mnakata umeme asubuh na kurudisha jion ila leo mpaka sasa hamjarudisha na hakuna taarifa zozote kutoka kwenu. Je tatizo ni nini?
Tunaomba namba yako ya simu, eneo, namba ya taarifa tukupatie ufafanuzi na kutatua tatizo lako mpendwa mtejaHabari za alfajiri, nimekua na subira kuandika hapa baada ya kuona ufanisi wa kazi za dharura sio mzuri na hakuna plan B. Ipo hivi usiku wa kuamkia jana kuna nguzo za high tension zilizokua na Transformer zimeanguka, hili nadhani kwa asilimia kubwa ni ubovu wa nguzo zenyewe kuwa zilikua tayari zimepekechwa vya kutosha na mchwa maana ni za siku nyingi kwa hiyo na kwa mvua zinazoendelea kikomo chake ikawa ndio hivyo kuanguka chini pamoja na transformer lake. Sasa hoja yangu ni hii umeme unakotokea kwenye substation sisi tungekua na uwezo wa kubakia na umeme maana Transformer yetu siyo iliyoanguka. Endapo Tanesco walipaswa kusimamisha nguzo nyingine kwa jana ili warejeshe waya kwenye position yake wakati wanajipanga kutafuta muda wa kurejesha huduma kwa wale ambao transformer yao imeanguka na kumwaga mafuta. Plan B ninayoongelea ni afadhali kuweka jumper kwenye nguzo za high tension kila baada ya umbali fulani ili kurahisisha kutenganisha eneo lenye tatizo na wateja wengine kuendelea na huduma maana tumeamka na giza jana na hadi sasa tumo ndani ya kiza totoro na leo hii ni Jumapili watakuja na sababu kuwa teamwork inahitajika kubwa kwa hiyo sioni ajabu kubakia kizani hadi kesho huku vitu vinavyohitaji umeme vikiendelea kuharibika. TANESCO HIMO KILIMANJARO ndio wahudumu wangu, je kama ni nguzo mbili zimewatesa siku nzima itakuaje ikitokea tatizo la line ya nguzo 5?
Tumepokea taarifa kwa hatua zaidi mpendwa mtejaMi sylivanus msanje
0717599264
Dar es salaam
Wilaya ya kibamba
Malamba mawili
Toka alhams nilipoti tatizo mita kutozalisha umeme kuingia ndani ya nyumba lkn mpaka sasa sijaona watu wa tanesco kila nikipiga simu wanasema wanakuaja wanakuja sioni fundi yoyote kufika nilipewa namba ya taarifa 3561 sijui wanasubiri nyumba iwake moto ndo watakuja nashindwa kuelewa naomba maada kutoka tanesco makao makuu.
Tunapigwa na Tanesco! Kwa lipi hasa tulilowakosea?Lazima mtakubali mapigo daaadeki
Mkuu. Nafurahi kusikia kwamba umepokea taarifa. Lakini sioni hatua ulizochukua hadi muda huu.Tumepokea taarifa kwa hatua zaidi mpendwa mteja
Tunaomba namba yako ya simu mpendwa mteja wetuHii ni wiki ya pili hapa kwetu hatuna umeme, sisi wakazi wa Nyamakendo kata ya Machochwe, wilayani Serengeti .
Kusema kweli ni ajabu sana, kwa sababu wakinamama badala ya kushughulika na kilimo wakati huu wa masika; eti sasa wanashinda wakihangaika kutafuta Mashine za kusaga nafaka ili familia ziishi.
Ni kweli huko nyuma tulikuwa na mashine zilizotumia mafuta, lakini baada ya serikali kutuletea umeme, ziling"olewa na kuhamishiwa kwingine. Sasa tunajiuliza naswali magumu bila kupata hata majibu mepesi.
Sijui tuwaombe wenye nazo wazirudishe kama watatuhurumia, au turudi kusaga kwa kutumia mawe na vinu ilihali hatunavyo kwa sasa?
Tusaidieni jamani ili tusijekuwa ombaomba.
Au hamulioni hili kama ni jambo mtambuka?
Mkuu nasikitika huko serious.Thread namba ngapi mpendwa mteja