Mimi ni mteja wenu wa Arusha tarehe mwenye Luku 37142673112 wiki iliyopita nimenunua umeme wa elfu ishirini na kukatwa elfu kumi eti nina deni. Nilipouliza nikajibiwa kuwa ninakatwa deni nililokuwa nadaiwa kabla ya kufungiwa luku. Sikubaliani na deni hilo kwani kabla ya kuwekewa luku TANESCO walihakiki akaunti yangu na sikuwa na deni lolote ndipo nikafungiwa luku. Nashangaa deni limetoka wapi? Nahitaji maelezo kuhusiana na deni hilo la kiasi cha T.sh. 155,000 kwani luku niliwekea tangu mwaka 2013 leo ndo wanakuja kukata fedha zangu eti ninadaiwa hii siyo haki tafadhali shughulikieni suala hili.