Tanesco naomba kufaham ikiwa nimekosea kununua umeme nikaweka naomba ya mita tofauti lakini umeme nikapata je naweza kuweka kwenye mita yangu ukafanya kazi??
 
Tanesco naomba kufaham ikiwa nimekosea kununua umeme nikaweka naomba ya mita tofauti lakini umeme nikapata je naweza kuweka kwenye mita yangu ukafanya kazi??

asante,
huwezi kuweka umeme ambao sio wa mita yako na kuingia.
 
asante,
huwezi kuweka umeme ambao sio wa mita yako na kuingia.
Naomba kujua baada ya kukosea katika kuingiza namba ya mita wakati wa manunuzi kama nimenunua LUKU kupitia mtandao wa simu nasaidiwa vipi...
 
Naomba kujua baada ya kukosea katika kuingiza namba ya mita wakati wa manunuzi kama nimenunua LUKU kupitia mtandao wa simu nasaidiwa vipi...
Shilingi ngapi na mita namba ya uliokosea ili tuweze kujua mita ipo wapi. Kama tutapata namba ya simu ya mteja uliokosea namba yake baada ya kuiona kwenye system zetu tutawasiliana nae kama atakuwa tayari kulipia hicho kiasi ili akufidie wewe au kufanya utaratibu mwingine
 
Eneo lenu la kazi kimamlaka ni lipi? Maana mnachagua maeneo ya kutoa Maelezo.
Kama mko kwa majibu ya Tanzania nzima naombeni JIBU.
 
Eneo lenu la kazi kimamlaka ni lipi? Maana mnachagua maeneo ya kutoa Maelezo.
Kama mko kwa majibu ya Tanzania nzima naombeni JIBU.
Nchi nzima

MFUMO WA KUTUPATIA TAARIFA/LALAMIKO

1.JINA.....................................

2.SIMU....................................

3.MKOA...................................

4.WILAYA................................

5.MTAA/KIJIJI/KATA.........

6.JINSI YA KUFIKA................

7.KITU/ALAMA/MTU MAARUFU.............................

8.NAMBA YA MITA................

9.TATIZO LAKO.....................


"TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO"
 
Mfumo huu sins tatizo nao na ni bora kabisa. Tatizo langu.

Mimi naishi kitongoji cha MKOKOZI wilaya ya Mkuranga tumepakana na wilaya ya Temeke. Kuna nyumba ziko upande wa MKOKOZI kiramani lkn zimewekewa umeme toka Temeke sasa kwann eneo lots lisihudumiwe na Temeke ili kurahisisha Huduma kwa Wananchi?

Kuna gharama zingine uko uwezekano wakazi tukihamasishwa tukajitolea kwa hali na mali
 
Tunaweza kupata namba ya mawasiliano yako
 
Habari TANESCO ... Umeme Kigamboni umekua kero kwa miezi ya hivi karibuni. Umeme unakatika muda mrefu sana na pia ukirudi unacheza cheza au unakua mdogo then unakatika tena.

Sikumbuki siku ambayo nimekaa na umeme bila kukatwa kwa siku nzima katika miezi ya April, May na June...
 
Tanesco Iringa> Sisi wakazi wa kijiji cha Igingilanyi tunaomba Tanesco itusaidie kupata umeme baadhi ya maeneo wale wakandalasi walipokuwa wanasambaza hawakusambaza kote mfano upande wa juu kutokea mjini na baada ya kambi ya wachina hawakusamabaza nguzo wakati baadhi tulishafanya wiring na matokeo yake hatujafungiwa hadi leo.

Tunaomba jibu ni lini tunafungiwa kwani umeme. Asante
 
naomba msaada mtupatie umeme,sisi wakazi Wa kata ya Itende mbeya mjini,nyuma ya jeshi la Jkt-itende!

Nguzo zimesambazwa mtaa mmoja tu Wa kata hiyo!mitaa mingine nguzo hazijasambazwa kwenye makaz ya watu bali zmepita kando ya barabara kuu ya kata as if wananch wote tunaishi along the road!

Tunaomba msaada wenu,tumejikussanya tumefika wananchi 102,tunaohitaji nguzo ili tufungiwe umeme!

kata IPO km 3 from mbeya city center ukipita jkt-itende
 
Tumeipokea mpendwa mteja
 
Aisee mi mwezi uliopita nimekuta tanesco wamepitisha Umeme kwenye kiwanja changu katikati eti kwa sababu kuna mama Fulani pale mtaani alikua ana hitaji Umeme yani nilishangaa hawa tanesco sana nimesha peleka malalamiko yangu lakini huu ni mwezi wa 2 sasa sijasaidiwa na nahitaji kujenga kwenye kiwanja changu
 
TANESCO IRINGA jamani naombeni jibu kijijini Igingilanyi ni lini mtasambaza nguzo za umeme kote maana tulidanganywa tutandaze nyaya majumbani matokeo yake wasambazaji wakasambaza sehemu chache wengine tukakosa tunaona miaka inaenda tumebaki na nyaya majumbani sasa hatuelewi kwanini tulitumia pesa zetu kwa kitu ambacho hakina maana?

Maana tunaona miaka inaenda tu wenzetu wachache waliofungiwa wakifaidi maisha ya mwanga wa umeme sisi wengine tukibaki na vibatari. Tulipofuatilia mlisema mkandalasi aliyepaswa kusambaza nguzo hakumaliza. Sasa kama yule hakusambaza kote ndio sisi tuendelee kukaa gizani hadi lini wakati yeye kaishia na mlishamlipa.

Sisi tunachotaka ni umeme hayo mengine mtajuana huko huko ofisini kama mlivyopeana kazi. Jamani tuleteeni umeme manavyokuwa na wateja wengi ndivyo mnavyopata pesa zaidi labda mtwambie umeme umekwisha!
 
Kibaya Nyie Interview zenu ni za kubebana kama mlizozifanya Mtwara Juzi aisee dhahiri na waziwazi bora msingeita wengine mngesema tu mnawaweka watu wenu wa mikataba kazini.

Sio mnaitwa watu wanachoma nauli zao alafu mnachokifanya ni dhuluma ya wazi wazi.


Nawashauri wakati mwingine msiwaite watu wala msitangaze hata hizo nafasi waajiri hao mliowaweka kwa mikataba sio kuwachosha vijana wa masikini kwa dhuluma zenu.

Na kumbukeni Mungu yupo na anawaona ipo ck yenu
 
Asante sana kwa uzi huu,kuna shida sana ya wizi wa mita za LUKU unaofanywa na vishoka cha kushangaza hizi mita hufungiwa wateja wengine hii inamaanisha kuna baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco wanashiriki hushiriki ndio maana huingizwa kwenye mfumo na kuendelea kutumika je Tanesco mnatueleza nini kwenye hili?

kwa nini mita iliyoibiwa ikinunuliwa umeme mhusika asikamatwe either kwa details zilizotumika kununulia umeme?
 

Asante ndugu mteja, katika kupambana n hili tanesco tunawahimiza kila siku kuwa watejanwetu wafike wao wenyewe ofisi zetu na kupata huduma ndani ya ofisi bili kutumia mtu wa kati na malipo yote ya shirikamhutolewa na risiti ya tanesco ikionyesha kiasi alicholipia chote bila upungufu.

Pia tunawahimiza sana kutojihusisha sana wizi wa umeme au miundo mbinu ya shirika kwani hatua kali dhiti yao zitachukuliwa ikigundulika,

Pamoj na hilo tunawaomba sana kutoa taarifa za wizi wa umeme katika ofisi ya tanesco iliopo karibu nayo au kwa namba ya simu 0768985100 ambapo taarifa yako itapokelewa kwa usiri mkubwa sana au unaweza kutumia ukarasa huu kutumanujumbe kwenye meseji au inbox na sisi tutaanza kuifanyia kazi mara moja


TANESCO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…