TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Kibaya Nyie Interview zenu ni za kubebana kama mlizozifanya Mtwara Juzi aisee dhahiri na waziwazi bora msingeita wengine mngesema tu mnawaweka watu wenu wa mikataba kazini.

Sio mnaitwa watu wanachoma nauli zao alafu mnachokifanya ni dhuluma ya wazi wazi.

Nawashauri wakati mwingine msiwaite watu wala msitangaze hata hizo nafasi waajiri hao mliowaweka kwa mikataba sio kuwachosha vijana wa masikini kwa dhuluma zenu.

Na kumbukeni Mungu yupo na anawaona ipo ck yenu
Habari,
Tumeipokea na tunaifanyia kazi
 
TANESCO IRINGA jamani naombeni jibu kijijini Igingilanyi ni lini mtasambaza nguzo za umeme kote maana tulidanganywa tutandaze nyaya majumbani matokeo yake wasambazaji wakasambaza sehemu chache wengine tukakosa tunaona miaka inaenda tumebaki na nyaya majumbani sasa hatuelewi kwanini tulitumia pesa zetu kwa kitu ambacho hakina maana? Maana tunaona miaka inaenda tu wenzetu wachache waliofungiwa wakifaidi maisha ya mwanga wa umeme sisi wengine tukibaki na vibatari. Tulipofuatilia mlisema mkandalasi aliyepaswa kusambaza nguzo hakumaliza. Sasa kama yule hakusambaza kote ndio sisi tuendelee kukaa gizani hadi lini wakati yeye kaishia na mlishamlipa. Sisi tunachotaka ni umeme hayo mengine mtajuana huko huko ofisini kama mlivyopeana kazi. Jamani tuleteeni umeme manavyokuwa na wateja wengi ndivyo mnavyopata pesa zaidi labda mtwambie umeme umekwisha!
Tunaweza kupata namba yako ya simu
 
Aisee mi mwezi uliopita nimekuta tanesco wamepitisha Umeme kwenye kiwanja changu katikati eti kwa sababu kuna mama Fulani pale mtaani alikua ana hitaji Umeme yani nilishangaa hawa tanesco sana nimesha peleka malalamiko yangu lakini huu ni mwezi wa 2 sasa sijasaidiwa na nahitaji kujenga kwenye kiwanja changu
Tunaweza kujuantatizo lipo wapi pamoja na namba yako ya simu
 
Eneo husika:Mbeya mjini, Block T, Transformer ya maeneo ya chuo cha teku mtaa wa memba

Kuna transformer yenu hapa inaweza kuanguka na kuleta tafrani kubwa, Mistimu ibayoishikilia imelegea sana na haijanyoka ipo mithiri ya kudondoka.
 
Tanesco natangulisha pongezi kwenu kwa kutufikia, Mimi nipo Iringa DC, naomba makadilio ya kuwekewa umeme.

Umbali wa nguzo ya mwisho mpaka kwangu ni metre 250. Je makisio itakuwa nguzo ngapi na ni bei gan.
 
Tanesco natangulisha pongezi kwenu kwa kutufikia, Mimi nipo Iringa DC, naomba makadilio ya kuwekewa umeme. Umbali wa nguzo ya mwisho mpaka kwangu ni metre 250. Je makisio itakuwa nguzo ngapi na ni bei gan.

wakikujibu unitag mkuu,I have the same problem!
 
Asante ndugu mteja, katika kupambana n hili tanesco tunawahimiza kila siku kuwa watejanwetu wafike wao wenyewe ofisi zetu na kupata huduma ndani ya ofisi bili kutumia mtu wa kati na malipo yote ya shirikamhutolewa na risiti ya tanesco ikionyesha kiasi alicholipia chote bila upungufu.

Pia tunawahimiza sana kutojihusisha sana wizi wa umeme au miundo mbinu ya shirika kwani hatua kali dhiti yao zitachukuliwa ikigundulika,

Pamoj na hilo tunawaomba sana kutoa taarifa za wizi wa umeme katika ofisi ya tanesco iliopo karibu nayo au kwa namba ya simu 0768985100 ambapo taarifa yako itapokelewa kwa usiri mkubwa sana au unaweza kutumia ukarasa huu kutumanujumbe kwenye meseji au inbox na sisi tutaanza kuifanyia kazi mara moja

TANESCO
Je hizi mita zinazoibiwa kwa nini zisifungwe,na kutotumika tena mara tu itolewapo taarifa ili zisitumike tena?
 
nauliza ukweli wa vifaa vya kupima umeme unaotumika ndani ya vyumba vya kupanga....vinaukweli wowote?

Je ni kweli vinapima umeme wa chumba husika tu?

ufafanuz..kuna kidude cha kipimia ni kias gan cha umeme mpangaji mmoja anatumia...ili aweze kulipia umeme anaotumia ambapo kidude hicho kitakuwa kinarecodi.

Binasf sivielewi na siviamini. kama ni halali nikaweke...kama sio niwape ramani mje mtoe naona jirani sijui ananini ndani na ameweka eti wiki ya nne sasa kinasoma 1.3 units kwa mwezi alizitumia...apartment ya vyumba 4 haiwezekani. Ina maana yeye alipe... bei ya unit x 1.3?
 
Vifaa vipo sawa ila hatuwezi kusemea chako maana hakijapitia kwenye wataalamu wetu kama ambavyo mita huwa tunazipima kwenye maabara yetu kabla ya kufikisha kwa wateja. Aidha unaweza kufuata taratibu ya kuomba kichunguzwe na Tanesco itafanya hivyo.
 
nauliza ukweli wa vifaa vya kupima umeme unaotumika ndani ya vyumba vya kupanga....vinaukweli wowote?

Je ni kweli vinapima umeme wa chumba husika tu?

ufafanuz..kuna kidude cha kipimia ni kias gan cha umeme mpangaji mmoja anatumia...ili aweze kulipia umeme anaotumia ambapo kidude hicho kitakuwa kinarecodi.

Binasf sivielewi na siviamini. kama ni halali nikaweke...kama sio niwape ramani mje mtoe naona jirani sijui ananini ndani na ameweka eti wiki ya nne sasa kinasoma 1.3 units kwa mwezi alizitumia...apartment ya vyumba 4 haiwezekani. Ina maana yeye alipe... bei ya unit x 1.3?
Mkuu nimeku PM please ukipata time cheki.
 
Mradi wa REA katika Kijiji cha NAMWAWALA kata NAMWAWALA Wilaya ya KILOMBERO Kilometa 30 toka Ifakara kuelekea Mlimba. Line ya umeme mkubwa baadala ya kupitisha kando ya barabar wao wamepitisha mitaani kwenye Viwanja na Nyumba za watu je ni sawa?

Kuna dalili ya rushwa ilitembea ili kuepusha Nyumba na biashara za Wakubwa wa Kijiji zilizo kando ya Barabara kuu ya Ifakara -Mlimba zisibomolewe.

Mfano mmoja angalia hii nguzo ipo jirani kabisa na nyumba.
Je , si ni hatari kwa wakazi hizi nyumba? Ukizingatia nyaya zipo wazi ,halafu kila baada ya nguzo tatu kuna Transformer kwa ajili ya kusambaza mtaani.
20170116_105732.jpg
 
View attachment 526297
Unapotoa taarifa haswa yenye shutuma kama hii ni vema ukatoa taarifa nzima na namba yako ya simu ili tuifatilie kwa kuwasiliana na wewe.maana si rahisi sisi kujua hapo ni wapi haswa kwa kutumia picha tu.
 
TANESCO NAWAPONGEZA KWA KUWEZA KUWEPO HUMU,
Managers wenu wanaweza ku-handle customers kwa kiasi kizuri,tatizo hawa mafundi naona kuna haja ya kuwapa seminar za customer care ili wajue walipa luku ndo walipa mishahara wao,so wanapopewa kaz ya kufanya,lazima ifanyike.

Above all kuanzia maguf kaingia naona mnajitahid kubadilika ukilinganisha na miaka mingne,keep it on
 
TANESCO NAWAPONGEZA KWA KUWEZA KUWEPO HUMU,
Managers wenu wanaweza ku-handle customers kwa kiasi kizuri,tatizo hawa mafundi naona kuna haja ya kuwapa seminar za customer care ili wajue walipa luku ndo walipa mishahara wao,so wanapopewa kaz ya kufanya,lazima ifanyike.Above all kuanzia maguf kaingia naona mnajitahid kubadilika ukilinganisha na miaka mingne,keep it on
It's a new era,wacha wapige kazi..
 
Asante sana mkuu na pia tumeipokea hio na tutajitahidi kuongea na kutoa semina kwa mafundi mkuu
TANESCO
 
Tanesco natangulisha pongezi kwenu kwa kutufikia, Mimi nipo Iringa DC, naomba makadilio ya kuwekewa umeme. Umbali wa nguzo ya mwisho mpaka kwangu ni metre 250. Je makisio itakuwa nguzo ngapi na ni bei gan.
Tanescoooooooo
 
Tunaweza kupata namba yako ya simu
Namba ya simu humu tena? Kutoka hapo ofisini kwenu ni karibu sana sio zaidi ya km 25 ukiwa Dar ni sawa utoke Mbezi kwenda Kariakoo. Ni vizuri mkafika sehemu ya tukio mkaonana hata na vion
Tunaweza kupata namba yako ya simu
Mimi nawashauri mfike tu hapo kijijini muangalie maeneo au nyumba ambazo wamefanya wiring na kujaza fomu za maombi lakini hawajafungiwa umeme. Diwani wetu yupo hapo mkifika atawasaidia sana kwani amejitahidi kufuatilia atawapa msaada lakini tutafurahi sana kama mkifuatilia hapo sio mbali na hapo ofisini kwenu kwani ni hapo jirani tu (mwisho wa uwanja wa ndege) sawa na kutoka Mbezi kwenda Kariakoo.

Nawatakia kazi njema na nawapongeza sana kwa jinsi mnavyojitahidi kusambaza umeme kwani sasa hivi hamkai ofisini kila siku mnaonekana mkizunguka na nguzo na kufunga na kufanya matengenezo
 
Shirika la Umeme Tanzania - (Tanzania Electric Supply Company Limited - TANESCO), Tunaomba mtupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri kupitia huu uzi nasi tutawajibu.

Tunawaomba mzingatie yafuatayo ili kurahisisha ufafanuzi na ufumbuzi wa tatizo au taarifa husika;

1.ENEO HUSIKA

(Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti)

2.NAMBA YA SIMU

(Wakati mwingine umeme upo kote isipokuwa kwako hivyo na rahisi kuwasiliana na wewe)

3.KARIBU NA NINI

(Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk)

4.JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO

(Toa ufafanuzi wa jinsi ya kufika makazi yako,chukulia unamuelekeza mtu ambaya hajawahi kufika kabisa)

5.MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI

(Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.)

6.KAMA NI TATIZO LA MITA NINI KINATOKEA UKIWEKA UMEME

(Kila mita ina ujumbe wake unaoashiria kitu fulani hivyo kubainisha ujumbe kunamsaidia mpokea taarifa kukupatia maelezo sahihi mfano mita namba 24339173921 inaonyesha error 77)

7.KAMA NI KUSHINDWA KUNUNUNUA UMEME UNAPATA UJUMBE GANI NA UNANUNUA KWA NJIA GANI

(Ujumbe huu ni muhimu sana kuweza kubaini chanzo cha tatizo pamoja na njia iliyotumika kununulia umeme mfamo Mpesa, Tigopesa, Maxcom nk)

TUNAENDELEA KUWASIHII WATEJA WETU KUZINGATIA UTOAJI WA TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA ZAIDI KUTOKA TANESCO.

ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA KUTOKA TANESCO

Kw mawasiliano Kituo cha Miito ya Simu (+255) 22194400 or (+255) 768 985 100 Mitandao ya kijamii Tanescoyetu (@tanescoyetu) | Twitter Facebook: Tanesco Yetu

HAPA CHINI NI NAMBA ZA SIMU ZA MIKOA

Ofisi ya Mkoa wa Mbeya Simu ya Mkononi (+255) 757 529 380 ya Mezani (+255) 252 504 219

Ofisi ya Mkoa wa Ilala Simu ya Mkononi (+255) 784 768 586 ya Mezani (+255) 222 133 330

Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni Kusini (Magomeni) Simu ya Mkononi (+255) 715 271 461/ (+255) 784 271 461

Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni Kaskazini (Mikocheni) Simu ya Mkononi (+255) 784 768 584 / (+255) 716 768 584 ya Mezani (+255) 222 700 367/ (+255) 222 701 602 / (+255) 222 774 098

Ofisi ya Mkoa wa Temeke Simu ya Mkononi (+255) 712 052720 / (+255) 758 880155 / (+255) 732 997361

Ofisi ya Mkoa wa Pwani Simu ya Mkononi (+255) 78 5122020 / (+255) 65 7108782ya Mezani (+255) 23 2 402 386

Ofisi ya Mkoa wa Arusha Simu ya Mkononi (+255) 75 8 174 343 Mezani (+255) 272 506 110

Ofisi ya Mkoa wa Tanga Simu ya Mkononi (+255) 658 122 412/ (+255) 687 677 667 Mezani (+255) 27 2 646 779

Ofisi ya Mkoa wa Kilimanjaro Simu ya Mkononi (+255) 765 397 925/ (+255) 682 771 310 Mezani (+255) 272 755 007/8

Ofisi ya Mkoa wa Manyara Simu ya Mkononi (+255) 689 795 599 / (+255) 75 9 534 130 Mezani (+255) 272 530 590

Ofisi ya Mkoa wa Mwanza Simu ya Mkononi (+255) 759 777 786 / (+255) 687 910 202 Mezani (+255) 282 501 060 / (+255) 282 500 090

Ofisi ya Mkoa wa Geita Simu ya Mkononi (+255) 744 085 696 Mezani (+255) 28 2520330

Ofisi ya Mkoa wa Kagera Simu ya Mkononi (+255) 78 5 787 898 / (+255) 75 3 120 701 Mezani (+255) 282 220 061

Ofisi ya Mkoa wa Mara Simu ya Mkononi (+255) 762 165 087 / (+255) 732 985 672

Ofisi ya Mkoa wa Simiyu Simu ya Mezani (+255) 282 700 180

Ofisi ya Mkoa wa Dodoma Simu ya Mkononi (+255) 782 161 643 Mezani (+255) 262 321 728

Ofisi ya Mkoa wa Morogoro Simu ya Mkononi (+255) 68 4889272 / (+255) 65 4829046 Mezani (+255) 232 613 501/2

Ofisi ya Mkoa wa Singida Simu ya Mkononi (+255) 71 4 477 445 / (+255) 732 960 924 / (+255) 689 373 757 Mezani (+255) 262 502 133

Ofisi ya Mkoa wa Tabora Simu ya Mkononi (+255) 786 558 510 / (+255) 763 162 868

Ofisi ya Mkoa wa Shinyanga Simu ya Mkononi (+255) 754 521 070 Mezani (+255) 28 2762120

Ofisi ya Mkoa wa Kigoma Simu ya Mkononi (+255) 78 3720598 Mezani (+255) 28 2802668

Ofisi ya Mkoa wa Katavi Simu ya Mkononi (+255) 68 8345200

IMETOLEWA NA:- Ofisi ya Uhusiano

TANESCO Makao Makauu.

Vilevile pitia threads hizi kupata Maelezo ya ziada;

LUKU:Mfumo wenye Tija kwa Wateja na TANESCO

Fahamu mita za LUKU zinazofungwa majumbani

Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO
Nasikitika sana emergency tabata wanachofanya hakuna maana ya kujiita Emergency, nilipiga simu juzi jumamosi mpaka Leo hawajafika kucheki tatizo langu na kuna Cheche zinatokea kwenye mita,inabidi tu nitafute kishoka, kweli Tanesco mnatakiwa kutumbuliwa mnatengeneza rushwa!
 
Back
Top Bottom