Jamani Tanesco sina huduma ya umeme siku tatu ,nimenunua Luku lakini kuingiza kwenye mita inasoma rejected,nikiwapigia wanasema watakuja lakini mpaka sasa hivi sioni mtu namba ya mita ni 24213776032,msaada tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu mpendwa mteja tunaomba maelezo ya ziada ya fidia ya nin? Wilaya? Eneo na namba yako ya simu
TANESCO MAKAO MAKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni fidia ya short ya umeme iliyotokana na Tanesco kuzidisha umeme toka 240v za Kawaida mpaka zaidi ya 300v iliyo pelekea kuunguza vifaa ndani ya nyumba na balbu kupasuka.kata ya sombetini ,na sehemu zingine mbali mbali .katika jiji la Arusha .na kwamba tumipitia hatua zote za madai na kudhibitishwa na Tanesco .tatizo lipo kwenye malipo mara cheque aija sainiwa Dar es salaam mkurugenzi kasafiri .mara waziri kaondolewa tusubiri ajae ,mara cheque zimekuja ila figure za pesa zimekosewa hivyo zimerudishwa Makao makuu Dar ,Na haya majibu tumekuwa tukipewa kwa miaka mitatu sasa inafika.na jibu la sasa hivi tuliopewa baada ya kuitwa tanesco tarehe 26/8/2018 kuchukua malipo yetu .tumeambulia kuulizwa kama tuna kubali kuingiziwa pesa bank moja moja kwa moja badala ya kulipwa kwa cheque au cash.cha ajabu tulipo rudi kutoa majibu .afisa mahusiano akapotea na meneja ofisi.ata hivyo baada ya kumvizia na kumpata afisa mahusiano .akatutaka radhi kuwa meneja hayupo na kwamba yupo likizo ya wiki moja .(ukiacha maajabu meneja likizo za wiki kama za raisi ) afisa uhusiano ametutaka turudi tarehe 5/9/2018 meneja atakua likizo imeisha ,hivyo hali ndio hiyo .ila pia kwa umoja wetu tumeamua tarehe 5 ni mwisho .tutatuma ujumbe wa wazi kupitia akaunti ya Facebook ya naibu Waziri wa nishati Mh Subhira Mgalu ,na kuhusu namba yangu ya simu hili jambo sio binafsi kiasi hicho ni jambo la wengi na kubwa tuu hapo Tanesco Arusha sio Private kiasi cha kuwasiliana na mtu moja .ila labda baada ya kuchaguliwa na wenzangu kuwakilisha baada ya hiyo tarehe 5/9/2018 .Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanesco wilaya ya kigamboni mbona mmetelekeza mradi wa U meme mchikichini kata ya somangira. Mradi ulianza tangu 2015 nguzo ziliwekwa zikachimbiwa 2016, kisha baadae 2017 nyaya zikatandazwa na wananchi tukaambiwa tujiandae kufanya wiring na kujaza fomu za maombi lkn mpaka Leo kimya. Tumesubiri zaidi ya mwaka sasa na tunaona miradi mingine ikitekelezwa na U meme kuwashwa lkn huku kwetu kimya. Kuna tatizo gani??????


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka miaka ya nyuma Tanesco mlikuwa na kitengo cha security na ninaamini malengo ya kuwepo kitengo maalumu cha security ni kulinda miundombinu ya shirika na kuwasimamia waajiliwa (staff) ambao wanajishughulisha na ukishoka (kusimamia nidhamu kwa waajiliwa pia).Shirika kama tanesco linatakiwa liwe na macho yanayoona mbali zaidi iwe kwa waajiliwa na vishoka wa nje ya shirika,na muache tabia ya kusubili mpaka mteja au mwananchi aje alalamike kwenu ktk mambo mf: lushwa/ubabaishaji/udalali yani muajiliwa kuchukua tenda ya et kumfatilia upatikanaji umeme mteja,nje ya maadili ya ajira yao kabisa, je tanesco aina macho binafc ya kuyaona haya?, Pia ninakuomba sana ww unaejibu malalamiko ya wateja.Mwananchi/mteja anatoa lalamiko lake mf kuhusu ukishoka wa staff wenu,alafu et unajibu oo tumekusikia ila tunaomba ushirikiano wako japo kwa kututajia ili tupate pa kuanzia,.kwa majibu kama haya kujibiwa na shirika kubwa kama tanesco ni uzembe sana, yani mnasaidiwa mnapewa picha michezo ilivyo bado unataka et usaidiwe zaidi ili kum baini staff ambae anajihusisha na ukishoka kazini,aisee da!! kweli tanesco mnafeli kila cku, Shirika linamtandao wa uongozi toka juu mpaka chini (wilayani) viongozi wameshindwa kabisa kuwabaini staff wanaojiucsha na ukishoka bila woga,au manufaa mnapata wote? ya ukishoka?.udalali kwenye application form costamer care zote za dar .Badilikeni plz hili shirika lina heshima sana ila waajiliwa chanzo cha kulichafua shirika.By Mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reactions: ADK
Mimi nauliza tena kwa mara ya mwisho,huduma ya kuhamishwa tariff kwa wakazi wa Dar bado lipo au limesitishwa?maana sipati majibu ya uhakika kwenye ofisi zenu,natumaini hapa leo nitapata jibu la uhakika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na maelezo mazuri hapo juu ndugu mheshimiwa unaehusika na Mahusiano napenda pia kuuliza vipi tayari mmekwishawalipa IPTL pamoja na HSCB zile pesa zao (ikiwa ni garama ya kuvunja mkataba,kuendesha kesi pamoja na riba zake) kama ilivyoamriwa na MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA USULUHISHI NA UAMUZI WA MIGOGORO YA KIBIASHARA?
 
Reactions: ADK
Jaman samahani.....nyumba ninayoishi inatatizo tunanunua umeme kila week........wanasema et tupo kweny system ya matumizi makubwa, tufanyeje ili tujinasue hapa.???.....Mana nlipokua naishi mwanzo ilikua ni unit 75 mwezi mpka mwezi.!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANESCO Ukonga. Nimepeleka maombi ya kuunganishiwa umeme tangu mwezi June mwaka huu, nikapewa account ya kulipia shilingi laki nane. Nikalipa, kisha nikaambiwa nisifike tena TANESCO kwani kuna foleni kubwa ya wateja, nitapigiwa simu. Mpaka leo ni kimya.

Je, inachukua miezi mingapi kwa mteja kuunganishiwa umeme?
 
Umeme ni viwanda, umeme ni maendeleo lipi mtashusha gharama za umeme?
 

Leo tarehe 6/9/2018 ndio tunakwenda Tanesco Arusha .fuatilia kwa habari zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…