Mita 50 kutoka kwenye Nguo maana toka nilvyoomba imefika imefika mwezi sasa
Wanachofanya Tanesco ni kwamba ikiwa upo ndani ya mita 30 hakuna uhitaji wa nguzo kama miundo mbinu ya umeme ipo,kuhusu muda uliokaa kuwa ni mwezi wao huhesabu kwa siku za kazi tu ikiwa kuna sikukuu na wikiendi wao hawazihesabu kabisa.
 
Mita 50 kutoka kwenye Nguo maana toka nilvyoomba imefika imefika mwezi sasa
Upo zaidi ya mita 30 kwa mujibu wa mkataba wa huduma kwa wateja wateja utafungiwa umeme ndani ya siku 60 za kazi
 
Tunaomba namba yako ya mita na ya simu tupitie manunuzi yako.Swala la tariff ni la mtumiaji wa umeme wa mita husika hivyo tunataraji mtu akilet ombi au lalamiko liwe la mita yake
Mita number 24219180114
Majibu yenu yale ya magumashi upo kundi sahihi sitaki kuyasikia

Nataka majibu sahihi
Nipo chini ya matumizi unit 40 kwa mwezi ayazidi hapo wala kupungua nina mwaka naaa kila siku naitaji ufanunuzi tu
Kwa nini bado nipo tarif 1 nataka majibu

Namba ya sim leo siweki hapa
Jibuni humu humu kwa faida yangu na wateja wengine wa Tanesco
Longo longo atutaki fungukeni tujue moja sio majibu ya shortcut ndugu mteja upo kundi sahihi !!!!
Sahihi hiyo kivipi? wakati mimi nipo chini ya matumizi tajwa unit 75
Mimi hata 40 kwa mwezi sifikishi kabisa..
 
Tanesci mmetukatili kukatiwa umeme bila taarifa na kutunyima kuangalia mpira wa simba leo. Baadhi ya sehemu ya Arusha wanao umeme
 
Sisi tumehamia nyumba ya serikali tumekuta Deni la umeme sio letu, tufanyeje?
 
Mkuu kunasiku nilikuuliza process za mtu kuhama na mita yake ya luku... Ukanieleza kuwa natakiwa kuwa na barua ya mjumbe... Naomba uniainishie the whole process.... Nataka kuondoa mita yangu niende nikaifunge napo kwenda kuhamia
 
Mpendwa mteja kama tulivyojibu hapo hawali mita ikifungwa haihamishwi nje ya eneo husika labda ndani ya nyumba hiyo hiyo.nayo unajaza fomu na tutakupatia gharama halisi
 
Sisi tumehamia nyumba ya serikali tumekuta Deni la umeme sio letu, tufanyeje?
Ndugu mpendwa mteja deni hilo ni la mmiliki kama mmelikuta mlipaswa kukubaliana naye maana sisi ni wajibu kukata pesa ya mita husika
 
J
Tanesci mmetukatili kukatiwa umeme bila taarifa na kutunyima kuangalia mpira wa simba leo. Baadhi ya sehemu ya Arusha wanao umeme
Ndugu mpendwa mteja tulitoa taaarifa ya kazi iliyokuwa inafanyika tunakuomba radhi sana kama hauikuipata
 
TANESCO Tunawashukuru Sana Kwa kazi nzuri mnayofanya kuhakikisha huduma zinakuwa Bora zaidi.

Ingawa tunaamini changamoto nazo huwa hazikosekani hasa kwa kukosa umeme kwa maeneo mengi ya Dar es Salaam.

Binafsi naishi hapa DAR (Chanika), katika ENEO la Chambala. ENEO hili lina wakazi wengi mno, tupo katika eneo hili kwa zaidi ya miaka mitano sasa. Tumehangaika mno kuomba umeme kwa kufuata taratibu za kawaida lakini hadi sasa imekuwa hadithi. Tulilazimika hata kufika katika ofisi ya Kanda (Kibaha Pwani) mwaka Jana 2017, May. Lakini tukaahidiwa mwaka wa budget 2017/2018 basi huenda fungu litatoka, mwezi July 2017 ukapita. Then, mwaka huu 2018 mwezi nadhani June akaja Naibu waziri wa Nishati akatoa ahadi kuwa umeme utaletwa siku za karibuni, mwezi July 2018 wakaja wafanya TANESCO kuchukua alama za maeneo ambayo nguzo zitasimikwa (Kwa mujibu wa wao), waliongeza kwa kusema kuwa mkandarasi anatafutwa kwakuwa tayari fungu limetoka, tukaambiwa tuvute subira nguzo zinaletwa, lakini huu ni mwezi October sasa hakuna kitu.

Ingawa wenzetu Jirani kidogo na eneo tulipo (Yongwe) tayari wameshushiwa nguzo, labda pengine watapata umeme hivi karibuni. Ingawa Bwana mmoja alisikika akisema nguzo hizo zineletwa kwakuwa kulikuwa na uchaguzi, hivyo huenda umeme ukaletwa baada hata ya mwaka.

Sina hakika tufanye nini, au tukalalamike wapi? Maana inaonekana kama tunalilia umeme ambao tutatumia bure.

TANESCO naomba majibu Juu ya hilo tafadhali.
 
Tumelipokea kwa ufatiliaji mpendwa mteja
 
Tanesco kwangu luku ina waka na ina.umeme lakini ndani hauwaki?
Kama umeme unafika kwenye mita ndani hauwaki unashauriwa kumuita fundi wako aliyesajiliwa kukufanyia uchunguzi au angalia main switch kama.ipo chini inapaswa kuwa juu
 
sijapokea token
mita:24218229599
trh: 02/10/218
namba:0626620789
kiasi:19780
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…