TANESCO Tunawashukuru Sana Kwa kazi nzuri mnayofanya kuhakikisha huduma zinakuwa Bora zaidi.
Ingawa tunaamini changamoto nazo huwa hazikosekani hasa kwa kukosa umeme kwa maeneo mengi ya Dar es Salaam.
Binafsi naishi hapa DAR (Chanika), katika ENEO la Chambala. ENEO hili lina wakazi wengi mno, tupo katika eneo hili kwa zaidi ya miaka mitano sasa. Tumehangaika mno kuomba umeme kwa kufuata taratibu za kawaida lakini hadi sasa imekuwa hadithi. Tulilazimika hata kufika katika ofisi ya Kanda (Kibaha Pwani) mwaka Jana 2017, May. Lakini tukaahidiwa mwaka wa budget 2017/2018 basi huenda fungu litatoka, mwezi July 2017 ukapita. Then, mwaka huu 2018 mwezi nadhani June akaja Naibu waziri wa Nishati akatoa ahadi kuwa umeme utaletwa siku za karibuni, mwezi July 2018 wakaja wafanya TANESCO kuchukua alama za maeneo ambayo nguzo zitasimikwa (Kwa mujibu wa wao), waliongeza kwa kusema kuwa mkandarasi anatafutwa kwakuwa tayari fungu limetoka, tukaambiwa tuvute subira nguzo zinaletwa, lakini huu ni mwezi October sasa hakuna kitu.
Ingawa wenzetu Jirani kidogo na eneo tulipo (Yongwe) tayari wameshushiwa nguzo, labda pengine watapata umeme hivi karibuni. Ingawa Bwana mmoja alisikika akisema nguzo hizo zineletwa kwakuwa kulikuwa na uchaguzi, hivyo huenda umeme ukaletwa baada hata ya mwaka.
Sina hakika tufanye nini, au tukalalamike wapi? Maana inaonekana kama tunalilia umeme ambao tutatumia bure.
TANESCO naomba majibu Juu ya hilo tafadhali.