Najua mlishatoa ratiba ya kukata na kurudisha umeme kwenye baadhi ya maeneo ya tabata na gongo LA mbota,tatizo ni kwamba hiyo latiba imeshaisha muda wake ila kwa bahati mbaya nyinyi bado nmakati umeme tatizo ni nini mipango yetu inakwama big time wakuu..twambieni kwa uhakika mwisho Wa katakata hii ni lini?
*TUNAKUMBUSHA TUNAKUMBUSHA*
*SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)*
*TAARIFA YA MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA UMEME*
Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa mkoa wa ilala kuwa, kutakuwa na kazi ya maboresho ya miundombinu ya umeme ili kuendana na ongezeko la matumizi ya umeme, ili kupisha maboresho hayo umeme utazimwa kama ifuatavyo;
*Muda:* 01:30 asubuhi mpaka 12:00 jioni
*Tarehe:*
*Novemba- 13, 14, 20 na 21/11/2018*
SABABU: *Kuvuta waya wa umeme wa msongo wa kilovolti 132 kutoka kituo cha ubungo mpaka kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Kipawa*
*MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI;*
Gongo la mboto yote, namera group of industries, Kampala university, Mombasa, Mazizini, Moshi bar, ukonga yote, kitunda yote, kivule yote, Msongola yote, Mongola, Ulongoni yote, stakishari, Said Mwema, Gongo zembe, Kisarawe yote, Majohe, FQ hotel, na maeneo jirani.
Tafadhari usisogelee, usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka, toa taarifa kwenye Dawati la dharura mkoa wa ILALA: 0784768586,0715768586,022-2133330,Viwandani 0684001066,0715768587 ,Tabata 0684001068 0715768589 , Gongo la Mboto- 0688001071, 0715 768 584
au kituo cha miito ya simu makao makuu:+255768985100
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
*Imetolewa na:* Ofisi ya uhusiano na huduma kwa wateja.
TANESCO- ILALA