Ombi langu ni maboresho kwenye teknolojia ya mita za luku
Kwamba niweze kutumia simu yangu kujaza umeme moja kwa moja bila mimi kuinuka na kwenga nje kubonyeza vitufe.
Vile vile hata kumjazia mtu alie mbali mf. Mama yangu anaishi kibiti na mie nipo Songea, ninunue umeme huku huku kwenye simu yangu na nitume moja kwa moja kwenye mita ya mama pale Kibiti
Yeye aone tu taa zinawaka bila yeye kuinuka na kwenda kujaza.
Wakati mwingine ni usiku na umeme umeisha, mita na yenyewe ipo nje na mama pale nyumbani hana vijana wa kumsaidia.
Ombi langu ni hilo yaani mama yeye awe anaona umeme upo tu muda wote bila kupanda kwenye stuli kujaza.