TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Nyumbani kwangu natumia umeme wa Luku ambayo ukiweka umeme usiku inagoma hadi uishe kabisa.Sasa jana nilijaribu kuweka uneme ikanigomea na hadi leo hii muda huu nimeuweka inakuwa kama imekubali baadaye inaandika Err_1 na umeme hauwaki,kinawaka kitaa kikoja hapo kwenye mita basi.Najiuliza nifanyeje wakuu?
Upo mkoa gani?
 
0784 768 584 head Ofice Tanesco
 
Mimi kero yangu kwa shirika lenu ni kupokea malipo ya kuwekewa umeme halafu unakaa zaidi ya miezi sita bila kuwekewa huduma hiyo.

Nina kibanda changu Tanga mjini eneo la kange nimelipia umeme tarehe 20/3/2017 ila mpaka mda huu sijaunganishiwa bado.Likizo hii nimefika ofisini kwao na majibu yao hakuna nguzo.

Sasa unapokeaje pesa ya mteja halafu miezi 5 huna huduma?Huu ni ubabaishaji.
 
Nataka nijue je tatizo la nguzo ni la kitaifa au Tanga tu mbona mikoa mingine si kama tanga!
 
Kwanza nianze tu kwa kusema shirika la tanesco ni shirika ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa Tanzanian kushindwa kundelea kwa haraka.

Mm hapa nyumbani nimefuata taratibu zote za kuingiza umeme. Na nimejaza fomu nimemleta mkandarasi
Na hatua ya tatu wakaniambia wataniita niende nikalipie na saizi huu ni mwezi wa tatu sijaona mesiji wala nini.

Juzi nikaamua kuwafuata lakini kabla sijaingia ndani nikakutana na msululu mrefu wa watu.
Kila mtu analalamika kivyake

Mwingine analamika amelipia umeme toka waka jana mwezi wa 8 lakini mpaka leo hawajamletea.

Sasa nikajiuliza swali moja hawa Tanesco wao wanafanyaje kazi?

Na kwanini wanachelewa hivyo kuleta huduma na wakati huo wanatumia mtaji wa mteja?

Akili ikanijia kwamba huenda ukilipia nguzo leo inabidi uisubulie hiyo nguzo ije ikue ikomae waikate waikaushe ndio waje wakuletee.

na ndio mm wameogopa kuchukua pesa yangu kwasababu labda hiyo nguzo ambayo inatakiwa nije niwekewe mm bado hata haijapandwa kwahiyo wakisha ipanda ndio inabidi waniite niende nikalipie ili niendelee kuisubiria hadi ije ikuwe ndio waje wanikatie na waniwekee.

Na hapa wameniambia niende nikalipie juma tatu na sijui huo mti ambao wataniwekea ndio watakuwa wameisha panda au vipi.

Na kivyovyote vile itakavyo kuwa sawa na ni lazima nisubirie hata kama ni miaka minne sawa hii ndio nchi yangu.
 
tanesco jengeni utaratibu wa kukagua miundombinu yenu mara kwa mara, sio kufuatilia madeni tu, pia mkikuta tatizo mlitatue sio kusubiria mpigiwe simu.
 
tanesco jengeni utaratibu wa kukagua miundombinu yenu mara kwa mara, sio kufuatilia madeni tu, pia mkikuta tatizo mlitatue sio kusubiria mpigiwe simu.
Utaratibu huu upo ndio maana ni kitengo cha ukarabati mpendwa mteja
 
Back
Top Bottom