Msaada namna ya kusahihisha jina lililokosewa wakati wa usajili wa mita. Mfano Kennedy ikawa Kenneth
Andika barua kwenda kwa manager wa mkoa wako huku uiiambatanisha copy ya kitambulosho kinachotambulika.uonyeshe sababu inayopelekea kunadili jina
 
Mpendwa mteja yote hayo yapo kwenye mikakati ya shirika muda muafaka utakapofika utashuhudia huduma hizo
 
Mimi nataka niwapongeze kwa kunipa huduma iliyopitiliza matarajio yangu,kwani kwangu umeme ulikuwa umekatwa baada ya kutokea hitilafu kwenye armored cable.

Hivyo mkaniambia mara fundi wangu wa umeme atakapokamilisha ufungaji nije niwataarifu.

Tulipokamilisha tukawaletea barua saa sita mchana tukiomba mje kurudisha umeme ndani ya masaa mawili tu mkawa mmefika na kurudisha umeme.

Mimi nilidhani mtachukua wiki nzima big up sana meneja wa Tegeta. Mimi nipo Tegeta karibu na canosa sekondari.
 
Kazi nzuri TANESCO. Mumekuwa responsive sana katika swala nililoripoti humu. Niliwatumia ujumbe jana asubuhi na jana hiyo hiyo mlinipigia na mafundi wakafika na kurekebisha tatizo. Nawapa 5 stars. Endelezeni huo utamaduni.
 
Tunashhukuru sana mpendwa mteja
 
Asante mkuu na karibu TANESCO
 
Kazi nzuri TANESCO. Mumekuwa responsive sana katika swala nililoripoti humu. Niliwatumia ujumbe jana asubuhi na jana hiyo hiyo mlinipigia na mafundi wakafika na kurekebisha tatizo. Nawapa 5 stars. Endelezeni huo utamaduni.
Aaante sana mkuu na pole sana kwa usumbufu wa uliopata
 
Nipo Maeneo ya kigamboni, kibada mtaa wa uvumba.

Nimelipia umeme tangu April 25 2017 yaani mwaka huu. Niliahidiwa kuwekewa huduma ya umeme ndani ya siku 60. Lakini mpaka muda na tarehe ya leo 27/6/2017 majibu yenu hayaeleweki na yanatia hasira sana. Mara nguzo zimeisha, nguzo zikipatikana kwangu hamleti mpaka muda huu.

Juzi mnatoa majibu eti nyaya ni tatizo maana zimeisha.

Sasa kama hamjajiandaa kwa nini mchukue pesa ya wateja wakati uwezo hamnao?

Hakuna madhirika yanachefua Kama Tanesco hapa nchini.

Nimedai nirudishiwe pesa yangu nikanunue umeme wa jua na hata hiyo mnajiumauma pesa yangu hamtaki rudisha.

Mnataka tuwafanyeje?
 
Reactions: ADK
Mkuuusijali maana wamepewa dead line ya mwezi mmoja na naibubwaziri wao wawe wamewamaliza matatizo ya wateja wao wote.

Tena wakaambiwa kwa wateja wapya wakilipia kuwekewa umeme waupate ndani ya wiki 2.
 
Nyumbani kwangu natumia umeme wa Luku ambayo ukiweka umeme usiku inagoma hadi uishe kabisa.

Sasa jana nilijaribu kuweka uneme ikanigomea na hadi leo hii muda huu nimeuweka inakuwa kama imekubali baadaye inaandika Err_1 na umeme hauwaki, kinawaka kitaa kikoja hapo kwenye mita basi.

Najiuliza nifanyeje wakuu?
 
Jaribu kuwapigia simu huduma kwa wateja.
Wakati mwingine ni matatizo ya luku yenyewe tu.
 
mi niliweka umeme wa elfu 30 last yr, hadi leo unit hazijapungua,ila umeme napata kama kawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…