NIna swali moja tuu. Mimi niko eneo ambalo linahudumiwa na umeme wa REA. Nyumba yangu nimefanya wiring kila kitu tayari, wakaja watu wa Tanesco kupima, wakaondoka na vipimo vyao, baada ya wiki nikatumiwa ujumbe nikalipie. Nikaenda nimelipia ili kuwekewa huduma ya umeme ambapo haihitajiki nguzo. Ni waya tuu kutoka kwenye nguzo na kuingiza kwangu.

Leo ni siku kumi zimepita tangu nilipie naona kimya, nikiwafuata maofisini huko naambiwa kisheria ni ndani ya siku 30. Sasa nauliza hizo siku 30 ndo tuseme mnatafuta nini ambacho hamna nyie? Yaani waya wa mita 30 tuu na mita ndo nisubiri siku 30? Nina hasira mimi. Nikadadisi kwa wenzangu mtaani ndo nikachoka kabisa, yaani naambiwa kuna watu wamekaa miezi miwili baada ya kulipia bado hawajawekewa umeme. Huu ukiritimba utaisha lini?

Au tutoe taarifa kwa viongozi wa kisiasa kama mawaziri na wakuu wa mikoa ndo mje mtuhudumie?
 
Tanesco, nimekosea kuandika namba ya mita yangu wakati wa kununua umeme, na nimeshapewa unit ambazo haziingii kuingia kwenye mita yangu, utaratibu wa kupata unit zinazoweza kuingia kwenye mita yangu upoje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu

Bora ww siku kumi.. Sisi Wengine tokea tumefanyiwa survey ni wiki nne zimepita...

Hatujui ni lini tutaambiwa tukalipe na Hatujui ni lini tutawekewa umeme


Tanesco Kisarawe imezidiwa kabisa... Inahitaji kusaidiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari,mimi mkazi wa Mbezi-Mpiji Magohe -Kibesa naomba kuuliza je lini TANESCO mtatuletea umeme katika kijiji chetu ukitazama idadi ya wakaazi inaongezeka kwa kasi na ni miaka imepita tokea TANESCO wapite kufanya survey ya mahitaji katika kijiji chetu. Kwa sasa umeme unaishia Mpiji Magoe mwisho na ni takribani kilometers 2 toka unapoishia umeme na upande wa Mabwepande unapoishia umeme(transformer-HT) ni 1km.Kwa sasa idadi ya nyumba zenye kukaliwa na watu si chini ya 1200.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dawati la Dharura Temeke wafanyakazi wengi ni wapuuzi sana,yaani unawapigia simu nyumba ina tatizo la umeme wanakuuliza maswali wakiona hawawezi kupata posho kutoka kwa mteja hawaji lakini kuna maeneo kama vile Bar,Lodge na maeneo mengine yanayofanana na hayo wakiitwa wanaenda haraka sana coz huwa wanapigwa bia mbili tatu.
Kuna dada mmoja yupo dawati la dharura huyu akiwa zamu ni kheri usipige simu maana ana maswali ya kipuuzi kweli kweli ukiwa na roho ndogo unaweza kumtukana.Nyumba yetu inatatizo la umeme lakini leo ni siku ya tano hawataki kuja.Unapewa namba ya kupata huduma lakini ukiwapigia ukiwaambia mbona hamji wanakwambia fundi yuko njiani atakupiagia mnasubiri weee mpaka saa tano usiku mkiona maumivu ya kuliwa na mbu yanaongezeka mnaingia ndani kupambana na joto.Siwatukani ila dawati la dharura wilaya ya temeke limejaa wapuuzi
 

Mkuu kwa hiyo na mimi nijiandae kisaikolojia kusota kumbe? Looooh, yaani nilivyojipinda kufanya wiring na kupiga mbao za dari mpaka tunashindia milo miwili badala ya tatu nimeshawishi familia kuwa mwezi hauishi tutakuwa na umeme. Kweli walihamasika ila kwa mwendo huu naanza kujuta kiaina
 
Ukitaka kuwajua tanesco ni waksti huu wa kuomba kuvuta umeme. Mi nimechoka hata kwenda kwenye ofisi zao hawana customer experiance kwa wateja wao kila anayeomba ndo uwa nafasi ya kuteseka kisaikolojia. Zimepita siku za huduma lakini sijafungiwa umeme. Tanesco hii takukuru wakae karibu wachunguze.
 

Tafuta elfu 50 alafu uone kama kuna mkate mgumu mbele ya chai.
Kuna mtu ameniambia hivyo leo mpaka imebidi nikae kitako kwanza.
 
Tunaomba namba yako ya simu tafadhali na nani amekuomba rushwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunaomba namba yako ya simu tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari nilinunua umeme kwa mara ya kwanza meter namba 54182472701 Sasa unit zangu 40 bado sijapewa mpk leo nilikuwa naomba msaada wa kuzipata. eneo kibamba hondogo jina Bernard Bakari Lingowe
 
Habari nilinunua umeme kwa mara ya kwanza meter namba 54182472701 Sasa unit zangu 40 bado sijapewa mpk leo nilikuwa naomba msaada wa kuzipata. eneo kibamba hondogo jina Bernard Bakari Lingowe
Kwani hizo Unit 40 Zinatolewa Burr Mkuu? Maelezo Tafadhali.
 
hahahahahaha siyo bure mkuu ukinunua umeme kwa mara ya kwanza wanakata unit 50 sasa wakati wananiunganishia walinipa unit 10 hivyo katika 50 nawadai unit 40 sasa walisema watanitumia baada ya wiki moja lakini wapi siku zinasonga tu mpk nimechoka kusubiri.
 
Tupende kufata taratibu mpendwa mteja wetu hakuna kutoa rushwa

Sent using Jamii Forums mobile app

Acheni kujishebedua huku mitandaoni na kwenye TV kusema hakuna kutoa rushwa, mandumilakuwili nyie. AU mnataka tuanze kuwaanika tena kwa majina ili mtumbuliwe? Leo hii nimeongea na fundi wangu aliyenifanyia wiring tena ni miongoni mwa mafundi ambao ni recognized contractor na Tanesco. Alinipigia simu kuuliza kama nimewekewa umeme? Nikajibu hapana, bado hawajaja. Akaniambia you cant be serious. Maana kuna mtu amelipia umeme juzi, leo ameshawekewa.. Nilipomdadisi akaniambia ila inabidi kama una chochote kesho tukafanyie kazi, kesho kutwa utapata umeme.

Tunajua picha kamili inayochezwa... msidhani watanzania ni wajinga kiasi hicho. Huyo mteja aliyewekewa ndani ya siku 2 amefuata taratibu zipi ambazo mimi sijafuata? Haki ya nani natafuta namba ya waziri mkatumbuliwe mmoja baada ya mwingine. Naongea kwa uchungu kwa sababu ya ubaguzi wa dhati unaofanyika Tanesco, mabosi wote na maengineer wao lao moja.
 
Tupende kufata taratibu mpendwa mteja wetu hakuna kutoa rushwa

Sent using Jamii Forums mobile app


Mteja ambaye eneo lake halihitaji nguzo, yaani yupo ndani ya mita 30. kinachohitajika ni mita, na waya tu mje kuunganisha, mnamwambia asubiri siku 30, kama siyo kutengeneza mazingira ya rushwa ni nini? Hiyo sheria ya kusema ndani ya siku 30 tafsiri yake siyo baada ya siku 30. Ni ndani ya siku 30, ikiwemo hata kesho yake mara baada ya kulipa. Sasa panafanyika delay techniques za makusudi. Kuna rafiki yangu aliambiwa eti mita zimeisha, imebaki moja tuu na inatakiwa iende sehemu nyingine. Jamaa kwa pressure akaingia kingi kwa kutoa rushwa ili hiyo mita ipelekwe kwake na ikawa hivyo. Japo hakuna ushahidi kama kweli mita imebaki moja.

Nyie ngojeni tu mimi nitawapa hela za moto
 
Hivi kwanini nguzo za umeme msiwe mnaziweka bure kupeleka umeme kwa wateja wenu?

Sent using Jamii Forums mobile app

Hiyo ni disaster. Kuna mtu aliweka umeme katumia nguzo 9. Mbaya zaidi wakamfanyia uhuni wanaweka zig zag ili nguzo ziwe nyingi kuliko umbali. Mwisho wa siku watu wengine wakija kujenga eneo husika zile nguzo ulizoweka ni mali ya tanesco siyo mali yako. Yaani utawaona majirani zako wanasherehekea kuweka umeme bila kutumia nguzo, na hakuna utakachoambulia.


Ingekuwa akili yangu, wateja wanaohitaji umeme wangewekewa hiyo huduma bure alafu baada ya mteja kupata hiyo huduma, akawa analipa deni la hizo gharama kidogo kidogo kwa mfumo ambao tanesco watakuwa wametengeneza. Mbona bodi ya mikopo inasomesha wanachuo na baadaye inarejesha fedha zake tena kwa riba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…