TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Tanesco vipi zoezi lakubadilisha tarif bado ukaguzi unaendelea?,maana mmetuweka tarif kubwa mkidai mnafanya ukaguzi from Agust/ 26/2018,hadi leo ? Jee huu ni uungwana? Kilimanjaro
 
Kuna tatizo la umeme limetokea katika mtaa wa Kimara- Stop over, panajulikana zaidi kama kwa Kapinga mtaa wa Mzazi mwisho kabisa chini kabla ya kuingia bondeni, na mjumbe wetu wa mtaa ni Noel Kessy. Nguzo imedondoka tokea Jumamosi, Tanesco mmetaarifiwa mkaja mkakata umeme mkaondoka (mimi nilitaarifiwa sikuwepo siku ya tukio) siku hiyo ya jumamosi kwa hilo tunawashukuru kwa uharaka huo na mliahidi kurudi jumatatu. Jumapili mmekuja (niliambiwa mmekuja asubuhi mapema) mkakata nyaya zinazounganisha nguzo iliyodondoka na nguzo nyingine mkaondoka.
Leo ni jumatatu nimeulizia kama mmeenda kukamilisha zoezi naambiwa bado hamjaenda mpaka muda huu ninaoandika sasa hivi. Mnataka watu watoe taarifa vipi? nyumba nyingi hazina umeme, kwa jinsi nilivyoangalia tukio lililvyo (kwa akili ya kawaida hata kama sio mtaalamu wa mambo ya umeme) sio nyumba zote hizo zilitakiwa kukosa umeme kama mlivyofanya, ni nyumba moja tu ingekosa umeme ( hapa siwafundishi kazi ila najaribu kuangalia uhalisia wa tukio lenyewe).
Kumbukeni tukio limetokea siku ambayo watu wameshafanya manunuzi ya majumbani kwao (mwisho wa mwezi huo kumbukeni) wamehifadhi vitu kwenye majokofu yao mnaweza kufikiria hata kidogo ni hasara gani watu wameipata mpaka leo, au mnadhani umeme ni kwa ajili ya kuleta mwanga tu? au mnajua hasara tunayoipata ndio maana mnafanya hivyo mlivyoamua kufanya halafu mkitegemea sisi tufanyeje sasa. Mmetutia hasara kubwa sana mpaka sasa, ipo siku tu nanyie hizo hasara mnazowasababishia watu zitawarudia. Ila kama kunamambo mengine muwe mnasema hapo hapo mnataka nini. Mnatia hasira sana nyie watu wakati mwingine. Mi nilifikiri TANESCO ya sasa imebadilika kumbe mnaendeleza mambo yale yale ya kizamani.
Haya bana nyie washindi.
 
Tunaomba namba yako ya simu mpendwa mteja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani Tanesco umeme shida huwezi ukafanya ujasiriamali kwa kutumia umeme kwa maeneo ya Tukuyu,unakatika mara kwa Mara kwa imekuwaje?mkurugenzi Tanesco hebu tuonee huruma,Kama Kodi zinatolewa shida Nini????
Ukiweka mayai kwenye mashine lazima uwe na generator.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani kwa upande wetu sisi wakazi wa Moshi Mjini kata ya Kiboriloni mtaa wa Forest, hawa Tanesco wamekuwa kama kuna sababu flani inayowalazimisha kufanya kazi chafu ili kila baada ya siku kama mbili au ikizidi sana siku tatu ni lazima tuwapigie simu umeme umekata chanzo ni nini? Hatujui! Sasa kwenye kuwasili kwao ni baada ya siku kadhaa au masaa yasiyopungua 10 ndipo wawasili.
Jamani wadau hebu naombeni ushauri nini kifanyike ili tuweze kukabiliana na hii changamoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi niko Soya Chemba nimelipia umeme kiteto tarehe 13 Jan 2019 mpaka Leo 28 march bado sijaunganishiwa umeme nikiuliza naambiwa nguzo ndy tatizo hivi nikweli au wanahitajirushwa maana nimesikia makampuni yakuzalisha nguzo yapo kumi Kutoka matatu ya awali naomba msaada wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
*TAARIFA KWA WATEJA WETU WA MLANDIZI NA BAGAMOYO*

*Machi 30, 2019*

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake wa Mlandizi na Bagamoyo kuwa leo Machi 30, 2019 majira ya Saa 1:50 asubuhi, Transfoma katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mlandizi imelipuka na kusababisha Mlandizi na baadhi ya maeneo ya Bagamoyo kukosa huduma ya umeme.

*MANEO YALIYOATHIRIKA NI*
Mlandizi na baadhi ya maeneo Bagamoyo.

Wataalamu wetu na mafundi wanaendelea na kazi ili umeme urejee katika hali yake.

Aidha, uchunguzi unafanyika kubaini chanzo cha mlipuko huo.

Tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza

Kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100

Tovuti: www.tanesco.co.tz,

*Mitandao ya kijamii*

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/

*IMETOLEWA NA:*

OFISI YA UHUSIANO

TANESCO MAKAO MAKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eneo letu la Msongola (Yatima) nyumba kadhaa hazina umeme siku ya nne 4, kuna mtu alikata mti ukaangukia kwenye nguzo. Watu wenu wamekuja mara mbili wametazama tu na kuondoka, imeshakuwa kero sasa. Tafadhali mtusaidie sio mpaka kila kitu "tuwe na mashati ya mikono mirefu" hata huduma za dharura!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwanza tu nikiri kuwa hakuna watu ninaowachukia kama tanesco kwa huduma mbovu wanazoto na kutudharau wananchi......
TULIKUA NA TATIZO LA SHOTI AMBAPO NYAYA ZILIKUA ZINAHATARISHA UHAI, TUKAWAJULISHA TOKA JANA JIONI HAWAKUJA NA NI ENEO TU HAPA MWENGE, tuliendelea kuwasumbua hadi asubuhi kwa zamu kutokana na eneo lenye shida tulivyo wengi, eti cha kushangaza wapumbavu hawa wanakuja baada ya 24hrs, sasa najiuliza nn inafanya wachelewe, kama ni hatari si itakua ishapata wananchi kwa jinsi walivyochelewa?
Sijajua usumbufu wao kwa sehemu ingine ila hivi ndivyo walivyotufanyia
 
Eneo letu la Msongola (Yatima) nyumba kadhaa hazina umeme siku ya nne 4, kuna mtu alikata mti ukaangukia kwenye nguzo. Watu wenu wamekuja mara mbili wametazama tu na kuondoka, imeshakuwa kero sasa. Tafadhali mtusaidie sio mpaka kila kitu "tuwe na mashati ya mikono mirefu" hata huduma za dharura!

Sent using Jamii Forums mobile app
Wilaya gani? Namba ya taarifa na namba ya simu tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi niko Soya Chemba nimelipia umeme kiteto tarehe 13 Jan 2019 mpaka Leo 28 march bado sijaunganishiwa umeme nikiuliza naambiwa nguzo ndy tatizo hivi nikweli au wanahitajirushwa maana nimesikia makampuni yakuzalisha nguzo yapo kumi Kutoka matatu ya awali naomba msaada wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
Jina
Namba ya simu
Wilaya tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom