Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yaani ni shida tupu ndugu yangu!Hili shirika siku wakipata mshindani watabaki na taasisi za serikali tu ila si kwa wananchi kwan ttcl ilikuwa wapi Leo wanapambana kutafuta wateja kila uchao
Sent using Jamii Forums mobile app
Tunaomba namba yako ya simu mpendwa mtejaKuna tatizo la umeme limetokea katika mtaa wa Kimara- Stop over, panajulikana zaidi kama kwa Kapinga mtaa wa Mzazi mwisho kabisa chini kabla ya kuingia bondeni, na mjumbe wetu wa mtaa ni Noel Kessy. Nguzo imedondoka tokea Jumamosi, Tanesco mmetaarifiwa mkaja mkakata umeme mkaondoka (mimi nilitaarifiwa sikuwepo siku ya tukio) siku hiyo ya jumamosi kwa hilo tunawashukuru kwa uharaka huo na mliahidi kurudi jumatatu. Jumapili mmekuja (niliambiwa mmekuja asubuhi mapema) mkakata nyaya zinazounganisha nguzo iliyodondoka na nguzo nyingine mkaondoka.
Leo ni jumatatu nimeulizia kama mmeenda kukamilisha zoezi naambiwa bado hamjaenda mpaka muda huu ninaoandika sasa hivi. Mnataka watu watoe taarifa vipi? nyumba nyingi hazina umeme, kwa jinsi nilivyoangalia tukio lililvyo (kwa akili ya kawaida hata kama sio mtaalamu wa mambo ya umeme) sio nyumba zote hizo zilitakiwa kukosa umeme kama mlivyofanya, ni nyumba moja tu ingekosa umeme ( hapa siwafundishi kazi ila najaribu kuangalia uhalisia wa tukio lenyewe).
Kumbukeni tukio limetokea siku ambayo watu wameshafanya manunuzi ya majumbani kwao (mwisho wa mwezi huo kumbukeni) wamehifadhi vitu kwenye majokofu yao mnaweza kufikiria hata kidogo ni hasara gani watu wameipata mpaka leo, au mnadhani umeme ni kwa ajili ya kuleta mwanga tu? au mnajua hasara tunayoipata ndio maana mnafanya hivyo mlivyoamua kufanya halafu mkitegemea sisi tufanyeje sasa. Mmetutia hasara kubwa sana mpaka sasa, ipo siku tu nanyie hizo hasara mnazowasababishia watu zitawarudia. Ila kama kunamambo mengine muwe mnasema hapo hapo mnataka nini. Mnatia hasira sana nyie watu wakati mwingine. Mi nilifikiri TANESCO ya sasa imebadilika kumbe mnaendeleza mambo yale yale ya kizamani.
Haya bana nyie washindi.
Mimi nauliza kwa Nini Tukuyu umeme mnakata Mara kwa Mara na no muda mrefu kurudisha?????Pole mteja zinapatikana muda wote, pia tupo katika mitandao ya kijamii
Jamani toka Jana saa 10 jioni hakuna umeme eneo la Moshi Kata yote ya Rau.Joto la Dar nyuzi joto 30 tu unalalamika,njoo hapa Dubai uchezee 44 ndio utaacha kulalamika
Sent by Diaspora
Wilaya gani? Namba ya taarifa na namba ya simu tafadhaliEneo letu la Msongola (Yatima) nyumba kadhaa hazina umeme siku ya nne 4, kuna mtu alikata mti ukaangukia kwenye nguzo. Watu wenu wamekuja mara mbili wametazama tu na kuondoka, imeshakuwa kero sasa. Tafadhali mtusaidie sio mpaka kila kitu "tuwe na mashati ya mikono mirefu" hata huduma za dharura!
Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kweli mpendwa mteja mita zote zipo sawa na hupimwa kabla ya kufungiwa wateja wetu.Baadh ya mita zinakula Umeme kuliko kiwango kilichotumika, nini tatizo? Je mnaovercome vipi tatizo hili?
Sent using Jamii Forums mobile app
JinaMimi niko Soya Chemba nimelipia umeme kiteto tarehe 13 Jan 2019 mpaka Leo 28 march bado sijaunganishiwa umeme nikiuliza naambiwa nguzo ndy tatizo hivi nikweli au wanahitajirushwa maana nimesikia makampuni yakuzalisha nguzo yapo kumi Kutoka matatu ya awali naomba msaada wenu
Sent using Jamii Forums mobile app