Kuna tatizo la umeme limetokea katika mtaa wa Kimara- Stop over, panajulikana zaidi kama kwa Kapinga mtaa wa Mzazi mwisho kabisa chini kabla ya kuingia bondeni, na mjumbe wetu wa mtaa ni Noel Kessy. Nguzo imedondoka tokea Jumamosi, Tanesco mmetaarifiwa mkaja mkakata umeme mkaondoka (mimi nilitaarifiwa sikuwepo siku ya tukio) siku hiyo ya jumamosi kwa hilo tunawashukuru kwa uharaka huo na mliahidi kurudi jumatatu. Jumapili mmekuja (niliambiwa mmekuja asubuhi mapema) mkakata nyaya zinazounganisha nguzo iliyodondoka na nguzo nyingine mkaondoka.
Leo ni jumatatu nimeulizia kama mmeenda kukamilisha zoezi naambiwa bado hamjaenda mpaka muda huu ninaoandika sasa hivi. Mnataka watu watoe taarifa vipi? nyumba nyingi hazina umeme, kwa jinsi nilivyoangalia tukio lililvyo (kwa akili ya kawaida hata kama sio mtaalamu wa mambo ya umeme) sio nyumba zote hizo zilitakiwa kukosa umeme kama mlivyofanya, ni nyumba moja tu ingekosa umeme ( hapa siwafundishi kazi ila najaribu kuangalia uhalisia wa tukio lenyewe).
Kumbukeni tukio limetokea siku ambayo watu wameshafanya manunuzi ya majumbani kwao (mwisho wa mwezi huo kumbukeni) wamehifadhi vitu kwenye majokofu yao mnaweza kufikiria hata kidogo ni hasara gani watu wameipata mpaka leo, au mnadhani umeme ni kwa ajili ya kuleta mwanga tu? au mnajua hasara tunayoipata ndio maana mnafanya hivyo mlivyoamua kufanya halafu mkitegemea sisi tufanyeje sasa. Mmetutia hasara kubwa sana mpaka sasa, ipo siku tu nanyie hizo hasara mnazowasababishia watu zitawarudia. Ila kama kunamambo mengine muwe mnasema hapo hapo mnataka nini. Mnatia hasira sana nyie watu wakati mwingine. Mi nilifikiri TANESCO ya sasa imebadilika kumbe mnaendeleza mambo yale yale ya kizamani.
Haya bana nyie washindi.